A
Anonymous
Guest
Wilaya ya Manyoni mkoani Singida inakabiliwa na tishio kubwa la kiusalama na kiuchumi kufuatia kushamiri kwa mtandao hatari wa wizi wa mafuta unaofanywa na baadhi ya madereva wa magari makubwa ya masanduku na yale ya kusafirisha mafuta kuelekea mikoa ya jirani na nchi za nje.
Uchunguzi na taarifa kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo zinaonyesha kuwa maeneo ya Sukamahera, Mwalala, na Kintinku yamegeuka kuwa vituo vikuu (vitiu bubu) vya unyonyaji na biashara haramu ya mafuta, huku mamlaka zikilaumiwa kwa kulegalega kuchukua hatua.
Inasikitisha kuwa wahalifu hao wamebuni mbinu za kisasa za kutoa vizibo maalum vya usalama (seals/silly) vilivyowekwa kwenye matenki ya mafuta, kisha wananyonya mafuta hayo na kuvirudishia vizibo hivyo kama kawaida bila kuacha alama yoyote ya uharibifu. Inaripotiwa kuwa gari moja la kusafirisha mafuta nje ya nchi (Transit) lina uwezo wa kunyonywa zaidi ya Lita 600 kwa awamu moja.
Hali hii inatengeneza bomu linalosubiri kulipuka wakati wowote, kwani hatari ya kutokea kwa majanga ya moto na milipuko ni kubwa mno, jambo linalohatarisha maisha ya familia zisizo na hatia na mali zao.
Suala linaloumiza zaidi ni kwamba wote wanaohusika na biashara hii haramu—kuanzia madereva, wamiliki wa sheli bubu, na nyumba zinazohifadhi mafuta hayo—wanafahamika waziwazi katika jamii hiyo.
Uchunguzi na taarifa kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo zinaonyesha kuwa maeneo ya Sukamahera, Mwalala, na Kintinku yamegeuka kuwa vituo vikuu (vitiu bubu) vya unyonyaji na biashara haramu ya mafuta, huku mamlaka zikilaumiwa kwa kulegalega kuchukua hatua.
Mbinu Hatari Inayotumiwa na Wahalifu
Mtandao huo unafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu kati ya madereva wasio waaminifu na wamiliki wa vituo bubu vya mafuta (sheli bubu) vilivyopo pembezoni mwa barabara kuu.Inasikitisha kuwa wahalifu hao wamebuni mbinu za kisasa za kutoa vizibo maalum vya usalama (seals/silly) vilivyowekwa kwenye matenki ya mafuta, kisha wananyonya mafuta hayo na kuvirudishia vizibo hivyo kama kawaida bila kuacha alama yoyote ya uharibifu. Inaripotiwa kuwa gari moja la kusafirisha mafuta nje ya nchi (Transit) lina uwezo wa kunyonywa zaidi ya Lita 600 kwa awamu moja.
Nyumba za Makazi Zageuzwa Maghala ya Mafuta
Moja ya mambo yanayotishia usalama wa raia wa Manyoni ni ukweli kwamba mafuta hayo ya wizi hayahifadhiwi kwenye bohari rasmi. Badala yake, hufichwa na kuhifadhiwa kienyeji kwenye madumu makubwa ndani ya nyumba zinazotumiwa kama makazi ya kawaida ya watu.Hali hii inatengeneza bomu linalosubiri kulipuka wakati wowote, kwani hatari ya kutokea kwa majanga ya moto na milipuko ni kubwa mno, jambo linalohatarisha maisha ya familia zisizo na hatia na mali zao.
Serikali Ikikosa Mamilioni ya Mapato
Mbali na tishio la usalama, mtandao huu ni pigo kubwa kwa uchumi wa nchi. Kwa kuwa biashara hii inafanyika "kichini chini," hakuna ushuru wala kodi yoyote inayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wala kusimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Serikali inapoteza mapato makubwa sana ambayo yangetumika kujenga miundombinu na miradi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi.Kilio cha Wananchi: Mbona Wahalifu Wanafahamika lakini Hawakamatwi?
Kero hii sio ngeni masikioni mwa viongozi na mamlaka za usalama za Wilaya ya Manyoni. Wananchi wanalalamika kuwa changamoto hii imesharipotiwa mara nyingi, lakini hadi sasa hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa.Suala linaloumiza zaidi ni kwamba wote wanaohusika na biashara hii haramu—kuanzia madereva, wamiliki wa sheli bubu, na nyumba zinazohifadhi mafuta hayo—wanafahamika waziwazi katika jamii hiyo.
Wito kwa Serikali na Mamlaka za Ulinzi
Kutokana na viambatanisho vya picha, video, namba za usajili za magari yanayohusika, na maeneo halisi ya hifadhi hizo haramu yaliyopo mikononi mwa raia wema, ni wakati sasa kwa:- Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida (OCD na RPC): Kuanzisha oparesheni maalum ya kushtukiza kukamata mitandao hii.
- EWURA na TRA: Kuingilia kati kuzuia vituo hivi bubu na kupotea kwa kodi ya serikali.
- Uongozi wa Wilaya ya Manyoni (Mkuu wa Wilaya): Kusimamia usalama wa raia wake kabla maafa makubwa ya moto hayajatokea kwenye makazi ya watu.