Dr. Zakir Naik ni muhubiri muoga sana akipigwa maswali magumu kama alivyopigwa maswali hapo Nairobi.
Na kizuri nchini Kenya lugha waliyotumia katika mdahalo ni kiingereza na hadhira inafahamu kiingereza pia jukwaa walilotumia ni la eneo local siyo kitaifa kupitia kituo cha televisheni cha kitaifa kama Azam TV.
Lakini kwa Tanzania kuna ajenda maalum kuzidi zile za Sheikh Mazige, Sheikh Mwaipopo n.k sasa kundi la Dr. Zakir Naik badala ya kutumia jukwaa online TV au ukumbi wa Diamond Jubilee au uwanja wa Benjamin Mkapa huyu muhubiri anataka kwa udi na uvumba kutumia jukwaa la kitaifa la Kituo tajwa cha televisheni kuingia katika kila sebule ya nyumba ya raia mtanzania kupitia kituo kikubwa kabisa cha kurushia matangazo ya televisheni cha Azam TV.
Nadhani haijawahi kutokea Tanzania kituo kikubwa kabisa cha Televisheni nchini ngazi ya taifa kikatumika ku test ukweli ya mitume, imani, biblia, Quran, Hadithi n.k kwa upande mmoja wa imani kujikita kusema kuwa kuna mapungufu kati imani inayotumika msikitini, kanisani, hekaluni au katika kusanyiko lao.
Siku zote katika jukwaa la kitaifa kupitia chombo cha umma kikubwa kama Azam TV, ITV n.k hutumika kuswalia, kusali, kuhubiri yale ya imani zao na siyo mashambulizi kuelekezwa imani nyingine.
Hii ni historia au precedent mpya inajaribu ku najengwa kwa chombo umma cha kitaifa kutumika kushambulia imani ya dini, dhehebu na mitume yao pia vitabu vya imani nyingine.
Kufanyika mdahalo Diamond Jubilee, online TV isiyo ya kitaifa, uwanja wa wazi Benjamin Mkapa hiyo siyo shida ila serikali kuruhusu vyombo vikubwa vya umma vya kitaifa kama Azam TV kuwa jukwaa la imani mmoja kushambulia imani nyingine siyo sawa.
Hii ya chombo cha mawasiliano cha kitaifa Tanzania kutumika kushambulia imani nyingine, ni sawa na Radio ile ya Rwanda radio
RTLM ilipotumika vibaya WaTutsi kushambuliwa kwa propaganda na Wahutu au wengine kisha historia ikatuambia 1994 ilifikia hitimisho jamii hizi za Rwanda kupata mihemuko na kuleta Maafa ya 'vita ya makundi' ikaishia Mauaji ya Kimbari.
Radio Télévision Libre des Mille Collines (RTLM) nicknamed "Radio Genocide" or "Hutu Power Radio", was a Rwandan radio station
26 December 2024
AZAM MEDIA LTD PAMOJA NA THE ISLAMIC FOUNDATION …
UJIO WA DR ZAKIR NAIK TANZANIA - RATIBA YAKE YOTE
View: https://m.youtube.com/watch?v=PLO0zcQm7ok
KWA MARA YA KWANZA TANZANIA WANAKULETEA MHADHIRI MASHUHURI WA KIMATAIFA , DKT ZAKIR NAIK AKIAMBATANA NA MWANAE SHEIKH FARIQ NAIK KATIKA MDAHALO WA MASWALI NA MAJIBU :
TAREHE 31/12/2024 MSIKITI ZINJIBAR, UNGUJA ZANZIBAR KUANZIA SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 7 MCHANA
TAREHE 2/01/2025 DIAMOND JUBILEE DAM KUANZIA SAA 1 USIKU HADI SAA 6 USIKU
TAREHE 5/01/2025 BENJAMIN MKAPA STADIUM UWANJA WA TAIFA KUANZIA SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 7 MCHANA
MATANGAZO HAYA YATAKUJIA LIVE - MUBASHARA KUPITIA CHANEL YA ZBC2 WEMA UNAOENDELEA
PIA TUTAKUWA MUBASHARA KATIKA DUA TV AOMBWAE NI MOLA PEKEE JESUS AND MUHAMMAD PEACE BE UPON THEM BROTHERS IN FAITH
View attachment 3187702
View attachment 3187703
View attachment 3187705