Twende taratibu bwana mkubwa;
Tanganyika uislam ule uliokomaa kabisa Upo mikoa hii;
Lindi,Mtwara,Pwani,Tanga na Dar japo kwa mbali sana……..Maana kwa sasa Dar Wakristo ni wengi sana kuliko Waislam kutoka na uvamizi mkubwa sana wa wageni toka mikoa mingine
Kanda ya Ziwa yote ni ukristo umeenea Tena kuna sehemu ukienda unaweza usikute msikiti ata mmoja
Kanda ya Magharibi pia hali ni hiyo hiyo,Ukristo ni mkubwa sana kuliko ata Uislam
Kanda ya kaskazini ukiiondoa Tanga ukristo umetamalaki kila sehemu na kuna sehemu ukifka ukasema wewe Muislam wataanza kujitenga na wewe kuwa una majini
Kanda ya Nyanda za Juu kusini,huku ndipo Ukristo umepanda juu sana………huku ukiwa Muislam wanakuona wewe kama gaidi tu