Kwa sasa makato ya kodi unaponunua LUKU yameongezeka kutoka TZS 1,000 mpaka TZS 2,000.
Tunaomba maelezo kwanini gharama hizi zineongezeka? Kuna sababu gani ya kuendelea kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu ili hali mabwawa ya umeme yaliyotumia matrilioni ya kodi za wananchi yameshafunguliwa?
Je, kodi wanazotozwa wananchi bado hazitoshi? Je, mmeshindwa kutumia rasilimali zilizopo nchini, kuna madini, maliasili na vivutio mbalimbali vya utalii n.k pamoja na vyanzo hivi vya mapato, serikali imeshindwa kuwa bunifu na kutegemea tozo na kuendelea kunyonya na kufanya maisha ya watanzania yazidi kuwa magumu?
Hali hii itaendelea mpaka lini?
View attachment 3030797
======
View attachment 3030953