Ndugu yangu unaweza ilaumu serikali bure. Serikali haikuambii ukiuke taratibu na sheria, Serikali haijakutuma ufanye ujinga au ucheze na kifo.
Tujiulize umshaona hawa wenzetu mfano wazungu hapa hapa Dar es salaam wanapata ajali za kizembe za piki piki? Tena wanatumia piki piki kubwa mno kuliko hizi za kichina. Achia wao hata wenzetu wenye asili ya kiasia ( wahindi) ushakuta wapi wanakumbana na adha za ajali za kijinga. Ndiyo ajali haina kinga ila umeshawahi ona ajali kwa mifano hiyo miwili za kijinga jinga.
Shida ni wao wenyewe waendesha boda boda ndiyo shida. Ujeuri ,ujuaji,ushamba kila kitu. Hakuna mtu atakulazimisha ujikinge na maisha yako kama siyo moyo wako mwenyewe. Polisi wamejitahidi sana kitengo cha trafiki kupambana nao lakini wapi hawasikii hapa nawatetea sana trafiki wamefanya jitihada sana.
Fikiria mtu unaona kabisa gari linakuja unakatiza mbele yake unataka serikali ukuambie subiri kweli?
Tujiulize Tanga, Mtwara, Shinyanga, Kigoma, Kahama, Tabora, Mwanza huwezi sikia haya? Kwa nini Dr es salaam zaidi? Najua unaweza singizia Magari Mengi ila huko kwengine ni hatari zaidi sababu mwendo utakuwa ni speed zaidi.Shida Dar boda boda wajuaji na waharibifu wa magari kupita na kuyakwangua. Dar na Arusha ni balaa.