Serikali imeshindwa kabisa kusimamia sekta ya usafiri wa pikipiki (bodaboda)!

Serikali imeshindwa kabisa kusimamia sekta ya usafiri wa pikipiki (bodaboda)!

Mkuu wewe kubali tu kuwa serikali legelege haisimamii sheria ipasavyo.
Hili la bodaboda hata wasomi wenye PhD za mbinguni wameshindwa kulitatua.
Tulete tu vijana kama wale walio mzodoa yule Profesa wa madini, waje wawaelekeze na kuwafundisha Polisi, TRA, LART na hata sheria za Usafiri mijini jinsi ya kutumia boda boda kistaarabu mijini..
Siye tumeshindwa.
Inabidi kucheka sasa tra na boda boda tena kwenye usalama? haya
 
kuna Bodaboda wana master's.
Kama ni kweli basi hajitambui huyo msomi!! Yaani una masters unafanya kazi ya kuingiza elfu 5 wakati hiyo elimu yake tu inatosha hata kujitolea kufundisha part time vyuoni akalipwa 30k kwa kipindi kimoja tu.
 
Maisha yasikie hivyo hivyo kaa wewe una kazi!
 
Mkuu wewe kubali tu kuwa serikali legelege haisimamii sheria ipasavyo.
Hili la bodaboda hata wasomi wenye PhD za mbinguni wameshindwa kulitatua.
Tulete tu vijana kama wale walio mzodoa yule Profesa wa madini, waje wawaelekeze na kuwafundisha Polisi, TRA, LART na hata sheria za Usafiri mijini jinsi ya kutumia boda boda kistaarabu mijini..
Siye tumeshindwa.
Inaonekana lengo la kuweka hii changamoto ya bodaboda ni kuonyesha sisi ni duni hatuwezi kusolve matatizo yetu na unaifurahia hiyo hali..si kweli kwamba hakuna mapendekezo yoyote yametolewa kujibu changamoto za bodaboda..lakini usitizame bodaboda as if wako mijin tu..tena pengine hao wa vijijin ni wengi zaidi ya hao wa mjini, fikiri sehem ambazo usafiri wa kutoka point A kwenda point B gari lipo moja tu, linapita asubuhi na kurudi mchana hadi kesho tena..uwepo wa boda boda umeondoa tatizo kama hili wafanyabiashara wadogo wanaweza kusafiri wakati wowote kufata bidhaa zao..lakin hata wale wanaoshuka kwenye vituo vya barabara kuu, km ya Dar-Mbeya, muda wowote akishuka within 10 mnts anapata boda boda anampeleka kijijini kwao hata kama ni saa 3 usiku..msitizame bodaboda km ishu ya dar peke yake, pengine role ya uwepo wa bodaboda kiuchumi na kijamii ni kubwa zaidi vijijini na hivyo inahitaji regulation kuondoa changamoto na kuifanya ikue zaidi ya hivyo ilivyo.
 
5. CCM- Sasa watambue kuwa mtaji wa bodaboda kisiasa umekuwa kero kuwa katika jamii. Lazima hatua za kisiasa zitumike kuwadhibiti na kuratibu kistaarabu.
Hawa ccm ndyo wanastahili laamazote kuhusu utitiri wa bodaboda na vurugu zao. Hao wengine umewaonea tu.
 
Wa kulaumiwa ni serikali na polisi.
Nilimshangaa igp sijui ikizugumzia ajali ya bodaboda na mwendokasi eti bodaboda alipita wakati taa hazimfuhusu bila kuwa mwangalifu wakati hakutakiwa kupita.
Hawa ataendelea kufa au kulemaa kwa uzembe wao na polisi.
Mbona Zanzibar wameweza?
 
Maisha yasikie hivyo hivyo kaa wewe una kazi!
Hapana mnalea ujinga sana, hivi una masters unashindwa kufundisha tuition mtaani? Unashindwa kuwa editor wa journals? Unashindwa kuandika research za watu wa PhD? Hizo sio ajira ila unajiajiri kwa elimu Yako huu upuuzi wa mtu una masters alafu unashindwa kutumia elimu Yako kujiajiri kitaaluma unaenda endesha boda boda naupinga kwa nguvu.

Wanaaibisha sana academicians
 
Wa kulaumiwa ni serikali na polisi.
Nilimshangaa igp sijui ikizugumzia ajali ya bodaboda na mwendokasi eti bodaboda alipita wakati taa hazimfuhusu bila kuwa mwangalifu wakati hakutakiwa kupita.
Hawa ataendelea kufa au kulemaa kwa uzembe wao na polisi.
Mbona Zanzibar wameweza?
kwani polisi ndiyo walimwambia pita chini ya basi? Hebu tusiwe wepesi kulaumu serikali wakati mwingine ni sisi wenyewe. Zimewekwa taa ili kila mmoja aweze pita kwa wakati mtu kaamua pita muda si wake na bahati mbaya basi limefika halafu unasema serikali ilaumiwe. hivi serikali kila kitu ikae inakushika mkono kweli? yaani unataka kila boda boda iwe inatembea na polisi kuchunga? Umetoa mfano mzuri zanzibar sijui ungejiuliza kwanini wao boda boda hawapati ajali za kijinga. Hata Mtwara,Lindi,Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Kagera,Ruvuma mbona hakuna ajali kama Dar ?
 
Ndugu yangu unaweza ilaumu serikali bure. Serikali haikuambii ukiuke taratibu na sheria, Serikali haijakutuma ufanye ujinga au ucheze na kifo.

Tujiulize umshaona hawa wenzetu mfano wazungu hapa hapa Dar es salaam wanapata ajali za kizembe za piki piki? Tena wanatumia piki piki kubwa mno kuliko hizi za kichina. Achia wao hata wenzetu wenye asili ya kiasia ( wahindi) ushakuta wapi wanakumbana na adha za ajali za kijinga. Ndiyo ajali haina kinga ila umeshawahi ona ajali kwa mifano hiyo miwili za kijinga jinga.

Shida ni wao wenyewe waendesha boda boda ndiyo shida. Ujeuri ,ujuaji,ushamba kila kitu. Hakuna mtu atakulazimisha ujikinge na maisha yako kama siyo moyo wako mwenyewe. Polisi wamejitahidi sana kitengo cha trafiki kupambana nao lakini wapi hawasikii hapa nawatetea sana trafiki wamefanya jitihada sana.
Fikiria mtu unaona kabisa gari linakuja unakatiza mbele yake unataka serikali ukuambie subiri kweli?

Tujiulize Tanga, Mtwara, Shinyanga, Kigoma, Kahama, Tabora, Mwanza huwezi sikia haya? Kwa nini Dr es salaam zaidi? Najua unaweza singizia Magari Mengi ila huko kwengine ni hatari zaidi sababu mwendo utakuwa ni speed zaidi.Shida Dar boda boda wajuaji na waharibifu wa magari kupita na kuyakwangua. Dar na Arusha ni balaa.
We jamaa hauko serious rais anapoapa anakabidhiwa mamlaka ya nchi juu ya vyombo vyote vya nguvu ili kuhakikisha ikiwa ni Kwa hiyari au kwa lazima sheria za nchi zinafuatwa na Kila mtu aliyepo Tanzania.

Ikitokea mtu yeyote anavunja sheria anatakiwa kushughulikiwa Kwa mujibu wa sheria.
Ndio maana kukiwa na uvunjifu wowote wa sheria lazima serikali ibebe huo wajibu Kwa sababu ipo hapo Kwa kazi hiyo
 
kwani polisi ndiyo walimwambia pita chini ya basi? Hebu tusiwe wepesi kulaumu serikali wakati mwingine ni sisi wenyewe. Zimewekwa taa ili kila mmoja aweze pita kwa wakati mtu kaamua pita muda si wake na bahati mbaya basi limefika halafu unasema serikali ilaumiwe. hivi serikali kila kitu ikae inakushika mkono kweli? yaani unataka kila boda boda iwe inatembea na polisi kuchunga? Umetoa mfano mzuri zanzibar sijui ungejiuliza kwanini wao boda boda hawapati ajali za kijinga. Hata Mtwara,Lindi,Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Kagera,Ruvuma mbona hakuna ajali kama Dar ?
Mleta mada kaongea kama great thinker kama hauna hiyo level huwezi kumwelewa ameongelea uholela ambao umeachiwa kwenye huduma ya bodaboda ndio chanzo Cha matatizo mengi zikiwemo hizi ajali. Mbona kwenye magari hatujaachwa holela hivyo?
 
We jamaa hauko serious rais anapoapa anakabidhiwa mamlaka ya nchi juu ya vyombo vyote vya nguvu ili kuhakikisha ikiwa ni Kwa hiyari au kwa lazima sheria za nchi zinafuatwa na Kila mtu aliyepo Tanzania.

Ikitokea mtu yeyote anavunja sheria anatakiwa kushughulikiwa Kwa mujibu wa sheria.
Ndio maana kukiwa na uvunjifu wowote wa sheria lazima serikali ibebe huo wajibu Kwa sababu ipo hapo Kwa kazi hiyo
Sipingani na ulichosema serikali kuhakikisha sheria zinaheshimiwa. Mimi nachopinga ni kuwa vyote vinafanyika isipokuwa hawa wenzetu wa bodaboda wapo radhi kufa kuliko zifuata. Nenda Moroko, Mwenge,Magomeni,Tazara, UONE WASIVYOTII sheria wanakatiza hovyo barabarani kwa kuona kuwa ni ngumu kuwakamata sababu ni rahisi kuwakimbia polisi usalama barabarani. Labda ungesaidi nini kifanyike mfano wazuiwe kabisa ila kumbuka ni biashara kama biashara ingine. Pili ni kwa nini wa Dar tu mbona wengine mikoani hawako hivi? Mbona vyombo vingine wao hawana shida ? kwani trafiki si ni hawa hawa? Akili tu ya boda boda ni shida na wanajazana ujinga sana.
 
Yes hapo kwenye nini kifanyike ndio mtoa mada amesema kama serikali imeishiwa mawazo ya namna ya kudhibiti hili kundi basi watoe kandarasi hata Kwa kampuni za kizungu ili zitusaidie kufikiri nini kifanyike kunusuru mali na maisha ya watanzania, maana inaonyesha PhD na doctorate zetu zimeshindwa kupata suluhisho!!
 
Serikali na CCM wamebaki kuwa washangaaji wa ajali za bodaboda.
 
Ajali za Bodaboda zimekuwa nyingi saana, mfano barabara ya Kilwa Road (barabara ya Mbagala) madereva wanne wameleta ajali wawili kwa hali waliyotolewa nayo kwenye ajali ni mbaya mno. Hivyo wanahofiwa
hawajafika hata hospitali ni ndani ya leo tu na abiria waliokuwa wamewabeba ni majerui.

Swali la kujiuliza watu sita ndani ya siku vipi ndani ya mwezi? Vipi ndani ya mwaka?.

Nashauri Serikali imefika wakati sasa na wao waingilie kati...
bodaboda zipungue...ila kwasababu hizo ni ajira za vijana wengi kwa sasa nchini Tanzania napendekeza:-
1. Bodaboda wapatiwe elimu na kuwapo na ufuatiliaji mkubwa wa matumizi yao ya barabara...

2. Kuwepo na usajili maalumu wa bodaboda zote ambapo mwananchi yeyote ambaye ataona kuna bodaboda anavunja sheria anaweza aka-report hata usajili wa hiyo bodaboda kisha muhusika akakutana na adhabu yake badae huko, kwa maana ya kutafutwa kupitia usajili huo

3. Mwisho kuna nchi ilikataza Bodaboda isiwe Public transport, ni kweli ni fast transport ukizingatia foleni za Dar but not safe
 
Back
Top Bottom