Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
RAIS SAMIA AMETOA BILIONI 150 KUJENGA BARABARA YA LUSAHUNGA - RUSUMO
Mbunge wa Jimbo La Ngara Mhe. Ndaisaba Ruholo Amemupongeza Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa Kutoa Bilioni Mia Moja na Hamsin (150)Katika Mradi Wa Barabara ya Lusahunga Mpaka Rusumo Yenye Kilometa Tisini na Mbili (92)
Akiongea na Baadhi ya Wananchi Katika Mkutano Wa Hadhara Uliondaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera Mhe. Oliver Semuguruka Amesema Kuwa Ilikuwepo Changamoto ya Barabara hiyo Ambayo Ilikuwa Imeanza Kuchakaa na Kusema Kuwa anampongeza Mhe. Rais Kwa Kutoa Pesa Hiyo.
Amesema Kuwa Jimbo La Ngara Ni Miongoni wa Majimbo Ambayo Yamepokea Pesa Nyingi za Maendeleo na Kusema Kuwa Chama Cha Mapinduzi Kipo Tayari Kutekeleza Miradi Ya Maendeleo Kwa Wananchi.