Tatizo ni pale unapouliza Magufuli anakwama wapi kwa huyu Makonda, wakati Magufuli hajawahi kuwa na consistent and coherent agenda popote.
Hapa atakwambia anapiga vita rushwa, kule kauza nyumba za serikali nje ya utaratibu mpaka kwa hawara zake. Pia anasema trafiki kupewa rushwa ni "hela ya kupiga viatu brashi tu".
Hapa atakwambia yeye ni rais wa wanyonge, na maendeleo hayana vyama, pale atakwambia atapiga wapinzani mpaka shangazi zao.
Hapa atamfukuza kazi Kangi Lugola kwa kupiga dili ambalo halijapitia bungeni, kule atanunua ndege bila idhini ya bunge, tender ya wazi wala kuruhusu ukaguzi wa CAG ATCL.
Hapa atasema anawakilisha maslahi ya wakulima wanyonge, halafu hapo hapo ataingilia manunuzi ya korosho na kuharibu soko kwa namna ambayo inaangusha mapato ya mazao ya kilimo kwa asilimia 55 katika mwaka mmoja tu unaoishia Agosti 2019, kwa mujibu wa ripoti ya Bank of Tanzania ya Oktoba 2019.
Sasa mtu kama huyu utategemea vipi ajielewe zaidi ya wholesale politics?
Na watu waliokuwa sane serikalini waliotaka kummdhibiti Makonda na kufanya "damage control" kama kina Dr. Mahiga ndiyo wanaondokewa kwenye prominence. Go figure.
Wizara ya Mambo ya Nje sasa hivi tungehitaji sana watu wenye busara na uzoefu wa kimataifa. Lakini wameondolewa, wamewekwa die hard ideologues waimba sifa. Clear mesage kwamba hatutaki watu wa busara, tunataka watu wa kujikomba kwa mkuu.
For all I know yeye Magufuli na Makonda hawajapishana sana katika kufikiri, na sasa wanaandaa vita dhidi ya "mabeberu".
Sent using
Jamii Forums mobile app