Serikali imwangalie Prof. Assad isimwache ateseke hivi. Huyu jamaa hayupo sawa

Wanyonge ni watu gani katika nchi hii? Nani aliwafanya wawe wanyonge? Magufuli alifanya nini kuondoa unyonge wao? Hizo ni kauli za ALIYE JUU MNGOJE CHINI badala ya kumfuata huko huko juu.
Kauli tu za kubeza matajiri na kuwaita MASHETANI ndiyo zilikuwa zinawafurahisha unaoita wanyonge. Maisha ya unaouta wanyonge yamebaki vile vile wanacheza bao vibarazani wanamsubiri Magufuli mwingine wamshagilie.
 
Kwa hiyo kila mmoja wetu akileta shida zake ili Serikali imsaidie si itakuwa balaa. Huyo Prof. atulie afanye mishe zingine mbona zipo tu, si ndo hao hao wanawaambia vijana wajiajiri ajira hakuna na yeye ajiaji maisha yasonge asituletee upuuzi wake hapa kila kukicha kulalamika.
 
Mkaruka...
"Upuuzi," "kulalamika," nk.
Lugha ya mtu aliyeghadhibika.

Unapoghadhibika akili inatoweka.

Suala la Prof. Assad linataka akili iliyotulia.

Prof. Assad hajalalamika.

Sikiliza mahojiano kwa utulivu na zingatia hukumu iliyopitishwa na mahkama.

Assad kaulizwa ana walinzi wangapi?
Tafakari jibu lake.

Ulinzi wa maisha yake yalihusika vipi na utekelezaji wa haki ya ukaguzi wa hazina ya nchi?

Haya hukuyasikia katika mahojiano?
Umeyasikia lakini hukuyapenda.

Huna akili ya kutambua vitisho huja baada ya kushindwa njia kubwa ya kushawishi?

Ushahiangaisha akili yako kupita katikati ya mistari kusikiliza kile ambacho Prof. Assad kwa uungwana hakukisema?

Usifanye haraka ya kutaka kunijibu.

Sikiliza mahojiano upya.

Ikiwa umejaaliwa fahamu utaelewa.

Ikiwa uko hivi kwa kuwa wewe ni "slow learner," pia utaelewa.

Kujificha nyuma ya pazia huna akujuae isiwe njia nyepesi ya kutukana na leseni ya kukejeli.

Kasema msemaji ati Prof. Assad anahitaji msaada wa kisaikolojia.

Mwonyeshe mwanasaikolojia kwanza yale yaliyosababisha Prof. Assad kukaidi kisha pili muulize huyu mtaalamu wa akili anaehitaji msaada wa kuwekwa akili yake sawa ni nani?

Elewa pia kutukana halikadhalika kujaribu kutisha watu ni dalili ya tatizo la akili.
 
Inawezekana pia sababu yeye waandishi wanamfuata kumuhoji....ndo maana anafunguka.Si kuna wengine walijifia kabisa inasemekana..bora yeye bado anapumua.
Pia wengine hamfikiwi kuhojiwa hamna pa kushushia jazba labda.
Ni kweli. Ila kwa huu mtazamo wa watu hivi, labda tu afunge hiyo chapter ya hayo maongezi. Inatosha. Anaweza kuwaambia waandishi kuwa hataki tena kuongelea hayo pindi wanapomfata.
 
kaa kimya, hayajawahi kukukuta
 
Huyu mpuuzi mwache amalizie siku zake duniani!
Mnafiki sana huyu na alikuwa anatumika na Kikwete kuhujumu serkali ni sawa na yule Daktari wa Moyo ameshakuwa kama taahira mwili kama ngozi ya joka eti anaelimisha jinsi ya kula!
 
Ni kweli. Ila kwa huu mtazamo wa watu hivi, labda tu afunge hiyo chapter ya hayo maongezi. Inatosha. Anaweza kuwaambia waandishi kuwa hataki tena kuongelea hayo pindi wanapomfata.
Jima...
Mahakama imetoa maamuzi ya kesi hii.

Prof. Assad ndiye mshindi.
 
Sasa analia lia nini kama hana njaa, yeye alimfukuza dereva aliyekataa kupanga mafaili bila sababu za msingi,wacha apate ukichaa kwa kulialia kila kuchwao, maisha si lazima uajiriwe, kuna lundo la watu wameachishwa kazi zao na hatuwasikii kulialia mitandaoni.
 
Sisi wakristo tunafundishwa kusamehe na kua usipomsamehe mtu hata wewe hutasamehewa na Mungu, angekua ni mkristo anayeisoma bible na kuielewa angeshasamehe
Mbona naona kama unaweka Udini? kwani Bible ipo kwa ajili ya wakristo tu ?
 
Siwezi kusemea kuruhani ya waislamu maana sijui vilivyoandikwa mle
Nafikiri kwenye biblia kuna msitari unasema 'jino kwa jino,hicho kea jicho' na kwenye Quran kuna aya inasema '..kusamehe ni bora'
 
Yamenikuta but i acted like a man. Siwezi kutembea nalia lia.
Ni upuuzi tuu...uanaume ni kukubali matokeo...
Profess wa hovyo kabisa....udini mwingi kucha kulalama....Wakina prof Abddallah Safari waliwahi kupitia madhaibu, mbona hatuwaskii wakilalama???
 
Mumbai...
"Hovyo" au "Ovyo?"

Lugha kali zinazodhihirisha chuki na hasa.

Katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam nakuhakikishia hakuna kuanzia VC hadi ngazi ya mwisho anaeweza kumwita Prof. Assad mtu wa ovyo.

Wewe una ujasiri huo.

Nimeandika fikra zangu katika post yangu # 133.

Naona inakwepwa wachangiaji wanaendelea kuandika kejeli na kashfa dhidi ya Prof. Mussa Assad.

Toka mwanzo imechukuliwa "wrong premise" kuwa Prof. Assad analia kuililia kazi aliyokuwanayo.

Kutokana na hilo ndilo haya yote yanafuatia.

Lakini hata pale inapokumbushwa kuwa hilo silo inaelekea hamtaki kusikiliza.

Mjadala wa aina hii hauna maana.

Tieni maanani kuwa ipo hukumu ya mahkama.

Prof. kashinda kesi.

Au tuchukulie mahkama imekosea?
 
Nadhani angepewa hata nafasi katika Bodi yo yote ili atulie! Mtu alikuwa CAG harafu akatupwa jalalani kwa kweli lazima aathirike kisaikolojia.
 
Hapana acha uongo!

Prof Mussa Assad alipofanyiwa interview na Kikeke alitoa machozi baada yakuulizwa swali ni kitu gani kinamuumiza sana kwenye maisha yake,akasema ni kifo cha mke wake, na wala siyo kutolewa kwenye post ya CAG! Tuache uongo!

Pili katiba yetu,inasema hivi, CAG akishatoka kwenye nafasi yake,hawezi teuliwa au chagulia kwenye post yoyote ile, so Rais hawezi mteuwa tena hata kwenye post ya Balozi!
 
Asote tu na yeye, kwani wengine tunaosota siyo watu?
Professor mzima unakuwa unajilizaliza ukisubiria usaidiwe na serikali au uteuzi ni dalili ya ulafa. Elimu uliyonayo haijakusaidia kujikomboa kutoka kwenye mawazo mgando. Kuna minafasi kibao internationally, kwa nini asitafute kazi huko? Amekalia kulialia tu!
 
Mbona clip niliyosngalia mimi Prof Assad hakulia kwa sababu ya kuondolewa ofisini, isipokuwa alilia alipoulizwa kuhusu mke wake aliyefariki? Alisema kulia kwake si sababu yuko weak, bali yuko strong ila amempoteza mtu muhimu sana katika maisha yake. Sasa inawezekana wewe uliangalia clip nyingine na mimi nyingine na si hiyo ya kuhojiwa Kikeke.
 
Professor wa Ovyo kweli huyo, Anadhalilisha Wasomi Aiseee, Yaani Yeye Kila Siku ni kulialia tu, Wenziwe kina Beno ndulu Wako Ughaibuni Wanapiga Pesa Uko,
Hapa kwenye bold nimekudharau kabisa!

Prof Beno Ndulu alishafariki toka mwaka 2021!

Pia Assad kilichomtoa machozi ni kifo cha mke wake na wala siyo post ya CAG aliyotolewa! Nenda kasome Katiba Ibara ya 144 (1) hadi 144 (6)
 
Huyu mwalimu wangu wa accounts ananisononesha sana.
Mwenzie Ludovick Utoh anakula mema ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…