Naona mnaingilia uhuru wa watu, hivi watu wanaoshinda Gym kuongeza vifua, mikono, miguu na kukata tumbo hamuwaoni?.
Iweje aliyeamua kwa hiyari yake kuongeza kalio iwe nongwa?
Mbona nasikia kuna hospitali hapa bongo zinaongeza makalio na hatusikii kelele?.
Hii dunia ni yetu sote, na kila mmoja ana angle yake ambayo anamkosea mwenzake ila tunaishi kwa kuvumiliana.
Nimeona clips nyingi za huyo mtumishi akiburudisha na kufundisha watu mazoezi hayo lakini siwezi sema mazoezi yake yana shida ya kuchangia ushoga na usagaji au laa.
Tuache hulka ya kila kitu kukihusisha na ushoga.