Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 9,548
- 28,817
Kwanza niipe hongera serikali kwa kwa upanuzi wa barabara ya Kimara-Kibaha siku hizi ukitoka Kimara Stop Over mpaka Kibaha unateleza kusimama ni kwenye mataa tu.
Ila janga ni ile barabara ya katikati ambayo ilikusudiwa iwe ya mwendokasi lakini mpaka sasa haitumiki ipo kama pambo. Huwa nikipita naumia sana kuona ikiwa haina matumizi na ni kama imetelekezwa.
Sijajua mkandarasi alifikiria nini? Au alikuwa amepiga hesabu gani, kwa sababu kwa jinsi imejengwa kwa sasa hata haiwezekani kujenga vituo vya mwendokasi kwa sababu ya ufinyu wa eneo la katikati kutosha kujenga vituo
Mwisho wa siku mabasi ya mwendokasi kutoka Kimara kwenda Kibaha yanapita barabara ya kawaida na kutumia vituo vya daladala. Huu sio utaratibu wa BRT kokote ukienda duniani.
Tatizo lilianzia wapi kwa mkandarasi au mamlaka iliyompa kazi mkandarasi?
Ni uzembe wa hali ya juu ukizingatia kodi za Watanzania zimetumika na nyumba za makazi na maeneo ya biashara yalivunjwa ili kupisha upanuzi wa barabara ya Kimara-Kibaha ikiwemo na mradi wa barabara ya mwendokasi.
Wenye mamlaka watupe majibu kuhusu barabara ya mwendokasi ya Kimara-Kibaha