Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Amin nakwambia, hiyo faida ya kuletwa na hizo ndege, kama itatokea, itaanza kupatikana kuanzia miaka 20 ijayo.Hakuna nchi iliyomaliza shida za wananchi wake wote kisha ndio ikawekeza kwenye vitega uchumi,ukisema usubiri matatizo yote yaishe ndio uwekeze kwenye Ndege basi sahau kununua hizo Ndege,
Ila hizo Ndege zikisimamiwa vizuri ndizo zitakazo leta faida ya kununua hayo madawati na mahitaji mengine,
Angalizo.Mimi sio shabiki wa vyama vya Siasa,usije ukaniita tu sijui buku 7 au bavicha au vyovyote vile.
Yaani ndege zilizonunuliwa kwa mabilioni ya cash money zirejeshe hiyo pesa halafu zitoe na ya madawati?
Kwa Tanzania hii (ya urefu wa kamba) isiyobadilika hiyo yaweza kuwa ndoto ya Alnacha.
Imagine, Ethiopian kama shirika la ndege linaloongoza kwa “faida” (profitability) Afrika, limesamehewa kodi kadhaa.
Ndege zake nyingi ni za kukodi (lease/purchase). Halina mchango wa maana kwenye hazina ya taifa bali indirectly kwenye uchumi na kule kuweza kujiendesha lenyewe tu.
Na linaendeshwa very professionally lakini zaidi ya kuwa nembo kubwa ya taifa, ziada ya kipato ni peanuts.