Serikali inanunua ndege kwa mbwembwe huku wanafunzi 65,000 wanakaa chini!

Amin nakwambia, hiyo faida ya kuletwa na hizo ndege, kama itatokea, itaanza kupatikana kuanzia miaka 20 ijayo.

Yaani ndege zilizonunuliwa kwa mabilioni ya cash money zirejeshe hiyo pesa halafu zitoe na ya madawati?

Kwa Tanzania hii (ya urefu wa kamba) isiyobadilika hiyo yaweza kuwa ndoto ya Alnacha.

Imagine, Ethiopian kama shirika la ndege linaloongoza kwa “faida” (profitability) Afrika, limesamehewa kodi kadhaa.

Ndege zake nyingi ni za kukodi (lease/purchase). Halina mchango wa maana kwenye hazina ya taifa bali indirectly kwenye uchumi na kule kuweza kujiendesha lenyewe tu.

Na linaendeshwa very professionally lakini zaidi ya kuwa nembo kubwa ya taifa, ziada ya kipato ni peanuts.
 
Uzuri wa SERIKALI ya CCM Haina kipau mbele
 
Akili za kimaskini ndio hizi

Hollywood kuna matajiri kama Will Smith, Denzel Washington na Tom Cruise wanaoishi kwenye majumba ya dola milioni 40 halafu kuna watu wanalala nyumba za maboksi, eneo hilo hilo moja.

Huwezi kusubiri kila mtu akawa vizuri kiuchumi eti ndio ununue ndege.
 
Hawa ndio wale Yerico nyerere kasema wanaihujumu Nchi.
 
Unachanganya mada.

Holywood ndio inatoa huduma za jamii kwa wamarekani?


Umekurupuka ndugu
 
Tunataka katiba mpya...ushuru wa local utumike ulipokusanywa na wananchi wawe na uwezo wa kuhoji na kuamua zitumike vipi,

Hayo matatizo ya madarasa na barabara za mtaani yangepungua, ila kusubiri Mwigulu akusanye then awaletee pesa itabidi msahau maendeleo
 
Ndio maana maeneo hayo wanayoishi hao billionaires yana shule nzuri na barabara nzuri , sababu ni hizo nyumba zinalipa property taxes na pesa yote inabaki hapo hapo kwa ajiri ya shule zao , park na barabara zao, na sehemu maskini US zina shule mbovu kwa sababu hiyo hiyo hawana loca tax base ya kutosha kufanya shule zao ziwe superb maana pesa wanayopata ni ya federal tuu ambayo ni limited,

Imagine Geita wangekuwa wanapata 10% ya tax inayolipwa hapo na makampuni yanayo operate hapo, ingesaidia kuleta ushindani na watu kufanya kazi kwa bidii popote walipo ili wapate maendeleo
 
Atcl wanashindwa kwenda nje kuna mizigo kibao inabidi iletwe na mashirika mengine kama ethiopian nk huku ndege ikimbeba hangaya tu
Hizi ni hasara kubwa kwa taifa letu.

Ndiyo maana watu tunahitaji katiba mpya ya kupunguza nguvu za viongozi wa juu.
 
Sisi ndiyo tuna ndoto za kulipita hilo shirika [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ebu twambie route za siku za ndege zote kumi na kitu mlizo nunua kwa kodi zetu.
 
Nakubaliana na mawazo yako mkuu.
 
Ni kama sisi kila siku tunaaminishwa kuwa mwenyekiti wetu ni tajiri, ila cha kushangaza makao makuu yetu hayana tofauti na banda la kuku.

Sasa tukipewa nchi sijui ni kipi cha maana tutachofanya kwa nchi hii.

View attachment 2168606
Kwa hiyo wakishajenga ofisi nzuri ndo ndo ufumbuzi wa kupata hayo madawati 65,000?
 
Kwenye ndege ndiyo wanakopigia rushwa kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…