Serikali inaogopa nini kufanya lugha ya kufundishia iwe kingereza kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu?

Kizuri ni kwamba mnaopenda Kiswahili endeleeni kusomesha watoto wenu kwenye shule za Kiswahili hakuna anayewakataza ila muache kulialia Wakenya na Waganda wanavyozidi kupata kazi nchini mwenu, hakuna mjinga mwenye kampuni inayofanya kazi kimataifa au anayedili na watu wa kimataifa aajiri watu ambao ni 'vihiyo' kwenye Kiingereza.
 
Hakuna kitu kama hicho, mkuu. UN Kiswahili kinaheshimika, sasa je?

Nini kinachokosekana au kushindikana kufundishia kwa Kiswahili? Mbona hadi vyuoni maprofesa na wahadhiri wanakiswang'anya Kiingereza huku wakitumia Kiswahili kama kawaida?

Jambo la msingi, maandalizi muhimu yafanyike halafu utajionea mwenyewe. Tena Kiswahili kinaweza kuwa bora kabisa hata kuliko Inglishi.

Miaka zaidi ya 100 ya matumizi rasmi ya Kiswahili, halafu bado watu wanadai eti ni lugha changa?
Mtu unaongea hivi halafu watoto wako wote wako English medium. Acheni kupotosha watanzania. Interview zote za kazi nchi hii ni kiingereza, halafu wewe unaongea nini hapa.
 
Mbona kuna shule za primary za English medium? Kisichowezekana ni nini?
Utafiti ulifanyika majibu yakaonesha haiwezekani. Fanya nawewe itafiti utapata jibu haiwezekani. Watoto wanaosoma english medium sio sawa nawatoto wanaosoma shule za kawaida . Vile vile ufundishaji na maslah ya English medium sio sawa na shule za kawaida
 
Bado nashindwa kuelewa kwanini serikali bado inapata kigugumizi kuamua tuu kingereza kiwe lugha ya kufundishia kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu ili kuendana na teknolojia na ulimwengu. Je nini kinawakwamisha

1. Walimu hawana uwezo?

2. Wanalinda biashara ya shule za mabasi ya njano kukosa wateja?

3. Wanaogopa kiswahili kitapotea?

Au ni nini hasa?

Mwanafunzi anamaliza kidato cha nne hata kuomba maji kwa kingereza haj
Shule nyingi za Private ni mradi wa watu serikalini,
Haiingii akilini kwamba anayepitisha mitaala ya shule za serikali na ndy huyo huyo watoto wake anasomesha english school..

Kama ni sawa Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia mashuleni basi na wao watoto wao wawapeleke kayumba..
 
Wenye teknolojia woooote huko duniani, mashule yao hufundisha kwa lugha za kwao, lugha inayotakiwa kufundishia hapa Tz ni kiswahili .
Una teknolojia gani ya kujidai ufundishe kiswahili kitupu?

Wachina,warusi,wajerumani nk wana teknolojia mswahili hana hata teknolojia ya kutengeneza kijiti tu cha mti cha kuchokonolea meno hawezi chonga halafu unaleta miyowe humu oohh wasome kiswahili kitupu kiwapeleke wapi wakati teknolojia hawana? Una roho mbaya wewe
 
Ajira za lugha ya kiswahili zinahitajika sehemu mbalimbali duniani

Leo wazungu wanajifunza kiswahili wakiwa kwao, wanakuja huku wakiwa wanafahamu angalau kidogo na zaidi

Balozi zetu zinafanya vizuri mfano ubalozi wa Tanzania Korea kusini, taasisi binafsi na vyuo kadhaa vina toa elimu ya lugha ya kiswahili huko ulaya na marekani (ujerumani, uingereza, marekani nk)

Hivyo kiswahili kina songa mbele kwa mwenye kukithamini, wapo ambao kingereza cha nini na wapo ambao wanakithamini kama unavyofanya
Kufundisha vizuri kiswahili nje kunahitaji kujua lugha za nje vizuri huwezi kurupuka tu Tanzania ukaenda korea kufundisha kiswahili wakati huwezi mudu kingereza vizuri au lugha yao ya kikorea
 
Kizuri ni kwamba mnaopenda Kiswahili endeleeni kusomesha watoto wenu kwenye shule za Kiswahili hakuna anayewakataza ila muache kulialia Wakenya na Waganda wanavyozidi kupata kazi nchini mwenu, hakuna mjinga mwenye kampuni inayofanya kazi kimataifa au anayedili na watu wa kimataifa aajiri watu ambao ni 'vihiyo' kwenye Kiingereza.
Uko sahihi
 
Una teknolojia gani ya kujidai ufundishe kiswahili kitupu?

Wachina,warusi,wajerumani nk wana teknolojia mswahili hana hata teknolojia ya kutengeneza kijiti tu cha mti cha kuchokonolea meno hawezi chonga halafu unaleta miyowe humu oohh wasome kiswahili kitupu kiwapeleke wapi wakati teknolojia hawana? Una roho mbaya wewe
Hiyo teknolojia mnayofundisha kwa lugha za watu tokea enzi na enzi mpaka leo ina manufaa gani katika nchi??

Mkitaka kutengemeza barabaran mnaita wataalamu kutoka nje.
Yaani kila kitu mnaita wataalamu kutoka nje, sasa miaka yote hiyo mnasoma utumbo?
 
Ndio maana tunasoma kwa lugha za nje hadi hapo tutakapokuja kuwa na teknolojia zetu ndipo tutaacha
 
Waulize hao watunga sera kwanini watoto wao hawawapeleki shule za kiswahili ila wanalazimisha wengine wasome hicho kiswahili

Nb: Teknolojia ya sasa kingereza hakikwepeki
Taifa limefanyanini kuwafanya wenye kiswahili chao wazid kukichafua kupitia ukuahi wa technology, au waswahili ni followers tu hawawezi kuja na vitu vyao kupitia kiswahili chao
 
Sisi hatuna vyakwetu ndio maana tunakihitaji kingereza zaidi
 
Vyakwetu ni vingi, ubongo wa kuvitumia na kuviendeleza ndo hatuna

Tunajikomba kwa kujua lugha zao

Akili ingekua vema kwetu, wao ndo wangejifunza kiswahili sababu ya vya kwetu.
 
Vyakwetu vipi sasa wakati kila kitu tuna import mpaka vijiti vya kuchokolea meno
 
Back
Top Bottom