Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 1,012
- 2,317
Watanzania maskini wengi wao wamekuwa wakipitia wakati mgumu na manyanyaso wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wanaofanya kazi viwandani hali hii haikubaliki na inaminya haki za msingi za binadamu.
kuna ushahidi mkubwa kuwa kuna watanzania wengi wananyanyasika viwandani na kufanyishwa kazi kama mifugo kwa masaa 24 bila kupewa nafasi ya kupumzika huu ni ukoloni na unyama na wala sio sawa wala haki hao ni wanadamu sio mifugo.
lakini pia licha ya kufanyishwa kazi kwa masaa 24 bado malipo yao ni madogo na sio ya uhakika kuna siku nyengine hawalipwi chochote hatuwezi kwenda hivi sisi kama nchi kwani wanaoteswa ni watanzania wenzetu hivyo serikali inapaswa kuliangalia suala hili na kuona namna ya kukomesha vitendo vyovyote vya unyanyasaji kwenye maeneo hayo ikiwemo kuweka sheria na utaratibu mzuri ili kuwalinda watanzania wote na ukatili wanaofanya kazi huko.
Nashauri itungwe sheria na tuweke utaratibu mzuri ili kuwalinda watanzania wote wanaofanya kazi huko ikiwemo wanawake na watoto, hii ni pamoja na kuweka ukomo wa muda maalum wa watanzania kufanya kazi ili kuwalinda na kufanyishwa kazi kupita kiasi kama mifugo kwa muda mrefu, pia nashauri serikali kuangalia na kuweka kiasi maalum kama malipo sio watu wafanyishwe kazi masaa 24 alafu walipwe fedha kidogo mfano elfu 1000.
lakini pia nashauri serikali kuweka muda maalum wa kufanyika malipo hayo kwa wafanyakazi wote kwasababu kumekuwa hakuna utaratibu wa malipo hali inayoweza kupelekea watanzania wasilipwe malipo yao baada ya kazi, kwahiyo nashauri serikali kuweka muda maalum wa kufanyika malipo hayo kwa wakati ili kuhakikisha watanzania wanapata haki yao.
pia nashauri serikali kuweka sheria ili kuwalinda watoto wanaofanyishwa kazi viwandani ikiwemo kuweka ukomo wa umri wa watu wanaopaswa kufanya kazi huko, hii itasaidia kuwalinda watoto wetu kwani kwa sasa hakuna utaratibu mzuri wa kuwalinda watoto na ukatili hasa maeneo ya viwandani, nashauri serikali kuliangalia suala hili.