Serikali inavuna ilichopanda: Fundi Maiko Syndrome - Goba Collapse

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594

Kwa muda mrefu sasa Serikali imepigia debe ujenzi wa majengo kwa kutumia Force Account na kutumia Local Fundi , ambaye mitaani anajulikana kama fundi Maiko.

Wananchi wameupokea mtindo huo kwa kuushangilia katika ujenzi wa majengo kwa nia ya kupunguza gharama.

Jengo lililoanguka huko Goba lilititia na kuanguka kama mbuyu uliojaa maji.

Wanasiasa watajipiga jaramba huku wakiwalaumu wengine.

Waziri wa Ujenzi Prof Mbarawa ni mmoja wa watu wamepigia sana upatu kujenga kwa Force Account na fundi Maiko.

Serikali inavuna ilichopandikiza kwa wananchi wake.
 
Ile video jana ilionesha nguzo ina nondo 2 cjui zile ama nne?
 
Nadhani unapotosha dhana ya force account

Force account haimaanishi kupunguza gharama kwa kupunguza material /ubora, bali kupunguza gharama kwa kutumia uwezo uliopo ndani ya Mifumo ya serikali na kwa wananchi pia.

Kwa mfano ujenzi wa madarasa unaofanyika sasa kwa Mtindo huo, Engineer wa halmashauri ndio msimamizi badala ya kumpa kandarasi mtu binafsi.

Wananchi nao wanachangia nguvu kazi hivyo gharama inapungua na urasimu pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…