Serikali inawapa sana hype na kick zisizo za lazima viongozi wa CHADEMA

Serikali inawapa sana hype na kick zisizo za lazima viongozi wa CHADEMA

Aliyemzuia Heche kaharibu sana. Kampa airtime ya bure kabisa. Chama cha siasa kuongelewa ndo kinakuwa hai. Leo na kesho ataongelewa Heche na CHADEMA bila gharama zozote wakati inatakiwa iongelewe CCM kwenye wakati huu wa kampeni. Hili kosa la kiufundi lisirudiwe tena.
umeona Impact ilikua ni ndogo kama hasingezuiliwa kama hata Suala la Lissu lilikua kosa kubwa walifanya
 
Vina wa Abduli wana mikwala mno.
Kuna huyu na mwenzake Lucha wana mikwala
mimi namshangaa! Huyu kimada akipelekewaga moto, anakuja humu kumsifia mama mkwe wake alafu anataka na sisi tumshabikie! Yeye na LUCHA wanapigwa kolabo so huwaambii!!
 
Ewee msukule sugu, usichokijua ni kwamba wao wanajua impact ya CDM ila nyie misukule ambao mnatembea na propaganda hamuwez elewa impact ya CDM!!
 
Tulitegemea tuone nini kutoka kwa kiongozi mtupu kichwani?

Na hapa bado , Mama atahaibika zaidi ya hapa ,tuombe tu Mungu atujaalie uhai ,tutalishuhudia anguko lake kweupe hadi tutapatwa na simanzi .

Kuongoza Taifa lililokukataa huwa kunachangamoto zake .
 
Ni UKICHAA ZAIDI KUAMINI CCM KIPO KWA AJILI YA MASLAHI YA WANANCHI,TENA UNATAKIWA UWE MIREMBE
uzuri tunategemea chama kipya cha upinzan, ni sku chache zmebaki tupate chama kingine huenda kitakua kinajielewa zaidi kwa kuelezea shida za wananchi
 
Jioni hii heche kazuiliwa kwenda msibani habari imeenda viral kila mtu amejua mfano asingezuiliwa kwenda msibani ni watu wachache wangejua heche ameenda msibani wengi wasingejua ila kwa tukio la jana watanzania wengi sana wamejua

Kuna mambo serikali inabidi iyapuuzie sababu yanawapa kick wapinzani ambazo hazina ulazima na inaharibu taswira ya serikali kwamba inaowaonea wapinzani

Hata wakati wa utawala wa magufuli mambo yaliyomwaribia taswira ni mfano wa haya ya kudeal na wapinzani mpaka kwenye vitu ambavyo ni vya kawaida sana
  • Wakati lema yupo gerezani aliwazuia wabunge wa ccm kwenda kumuona waliojaribu kwenda kama vick kamata alichukiwa jumla
  • Wakati tundu lissu yupo hospitalini kenya akawazuia wabunge wa ccm kwenda kumuona
Hayo ni baadhi ya matukio ambayo yalimwaribia sana taswira ya serikali yake

Serikali inawapa watu ushujaa watu kwa mambo ya kawaida sana sina chuki na heche mfano wamemnyanganya passport yake na ameenda kenya bila utaratibu
  • Nashauri heche akirudi wasimkamate sababu wakimkamata tena itazua taharuki kwa wananchi na inapeleka picha mbaya kwa wananchi kwamba wana/anaonewa
Mtu pekee ambaye angewasaidia sana sana ccm alikuwa ni polepole yule jamaa alikuwa very strategic kuongelea ccm tu hakuna chama kingine sema ndio hivyo tena wao wamemuona kama adui vile.
 
Aliyemzuia Heche kaharibu sana. Kampa airtime ya bure kabisa. Chama cha siasa kuongelewa ndo kinakuwa hai. Leo na kesho ataongelewa Heche na CHADEMA bila gharama zozote wakati inatakiwa iongelewe CCM kwenye wakati huu wa kampeni. Hili kosa la kiufundi lisirudiwe tena.
Ndio ujue kwamba hii ccm ya samia inaongozwa na vilaza tupu, yaan kwenye jopo lake hakuna smart strategist hata mmoja, kwanzia yeye mwenyewe ni kilaza mtupu...

....Nina amini kabisa akilini mwa viongozi wa ccm waliamini Heche alikuwa anatumia huu mwanya kwenda kwenye msiba kukimbia nchi hasa kipindi hichi ambacho kuna political crisis inanukia...

....Na hapo nyuma Samia mwenyewe alisema watawazuia viongozi wote wanaohamasisha maandamano wasiondoke nchini hili wote tuungulie hapa hapa.

Kwa hiyo hawa maafisa uhamiaji walipewa maelekezo kabisa wafanye hicho walichokifanya hiyo jana..

Matokeo yake sasa hivi serikali ya samia inazidi kuchafuka tu huko nje, inaonekana ni serikali ya kihuni inayoongozwa na wajinga wajinga wasiojielewa ambao wanatumia vibaya madaraka waliyopewa.
 
Maana yake wafanya maamuzi wengi siyo smart na taharuki nyingi zinasababishwa na mfumo zaidi
 
si bora useme CHAUMA wanajali nchi kwa sababu wao wamejiandaa kwa HOJA kwann wachaguliwe sio nyie mnapenda kiki 😂 😂
Hao chauma/cha wali wana hoja gani na wakati muda mwingi kwenye mikutano yao wanaongelea watu ambao hata uchaguzi hawashiriki?
 
Sasa serikali imejaza wazanzibari vichwa bapa kichwani watupu kabisa unadhani wanajua hilo, hata mimi nilikiwa sijui kama heche anaenda kumzika huyo bwana odinga, ila nimejua baada ya hicho kisa cha heche na uhamiaji , wameicheza vizuri ngoma ya lissu
Aisee nilijua ni mimi tu ndio ambaye ninawaona wazanzibar kichwani hamnazo, hao watu hawana kabisa uwezo wa kureason kwa mapana... wana maamuzi ya ovyo sana halafu wakiharibu hawajui kma wanaharibu.

Tena naskia ndio wamejaa kwenye nafasi zote za juu huko TISS.
 
Tatizo wao wanaamini wanapambana na chadema na wanajitoa ufahamu kwamba chadema ni watu kama ilivyo ccm ni watu , sasa wao hawataki kuamini kwamba CHADEMA ni chama kama ilivyo ccm na chadema nacho kimebeba maamuzi ya watanzania na wanachama wake ni watanzania kama ilivyo ccm, wao wana treat chadema kama kikundi cha watu tu na sio chama chenye imani kubwa kwa wananchi na hawataki kuamini hilo hapo ndipo wanapo kosea kuelewa.

Ni sawa na kuamini kwamba mashabiki wa yanga ni halali lakini wa simba ni kikundi cha watu tu.serikali yetu kwa sasa haina watu wenye uwezo mkubwa wa kutambua mambo wamejaa vilaza watupu
Binafsi mimi huwa nashangaa na kujiuliza sana mzee kikwete huwa anamshauri nini Samia? Maana kwa uzoefu mkubwa aliano yule mzee wa siasa za kitaifa na kimataifa anajua nyakati kama hizi ni nini cha kufanya hili kuzuia political damage inayoweza kuitia doa serikali..

....hata siasa za fitina mzee JK anazijua vizuri sana, angeweza kumshauri samia apambane vipi na hao chadema kwa ustadi bila kuleta athari zozote ambazo zitakuwa ni advantage kwao.

Nashaanga sana sijui huwa anamshauri nini samia.. na hakuna kipindi ambacho samia anahitaji ushauri mzuri na makini kama kipindi hiki..

...ila ninavyoona samia amechagua kufanya siasa za kimafia wakati huu na si ajabu mshauri wake mkuu kwenye siasa hizo za kimafia ni bashite.
 
Back
Top Bottom