Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,884
- 21,175
Moja ya sekta kubwa inayochangia GDP na kutoa ajira nyingi ni ujenzi. Nchi yetu, miji na majiji mengi yana barabara mbaya za mitaa.
Tunaweza kuboresha barabara hizo kwa kutumia mafundi wa ndani, materials zote za ndani, bila kugusa forex yetu kwa kulipa wakandarasi wa nje na kununua vitu kama lami. Hapo hapo tutapendezesha miji yetu na kuzalisha maelfu ya ajira kwa vijana. Mawe tunayo, mchanga tunao, cement tunayo, nadhani na nondo za zege tunazo.
Tuanzishe kampeni ya kupave kila barabara ya mtaa. Serikali kuu itoe(ichapishe) pesa kila mwaka na kuwapa miji na majiji wajenge barabara za mitaa. Huko machimbo ya mawe na mchanga na kokoto yatachangamka.
Wasafirisha materials watapata ajira, wachimba mawe watapata ajira, waponda kokoto watapata ajira, wajenzi na saidia fundi watapata ajira. Kila mji na jiji kutakuwa na ajira za ujenzi, mwaka mzima na kwa miaka mingi. Zaidi ni kuwa miji itaboreka.