Serikali inayobadilisha maamuzi yake kwa kutegemea upepo ni Serikali dhaifu, haifai

Nimeshangazwa na hili hapa kama ni kweli: Mwigulu: Tumesikia malalamiko ya Watanzania kuhusu tozo za miamala na Rais ametoa maelekezo ya kuzitazama upya

Hivi inawezekanaje serikali (hapa serikali kwa maana ya watendaji wakuu wa serikali, mawaziri wakiwemo na vyombo vyao vinavyowasaidia katika maamuzi ya kisera) kuamua kitu na baadaye ikifikirie upya baada ya kusikilizia mwitikio wa watu?

Hebu imagine, hivi serikali ya aina hiyo itawezaje kweli kufikia malengo yake? Maana serikali ya aina hiyo itakuwa inaamua hili halafu sisi raia tukipiga kelele inaacha kulitekeleza.

Hii ni dalili kubwa kabisa kwamba tunaongozwa na watu dhaifu sijapata kuona. Hata JK hakuwa dhaifu hivi. Tulimpigia kelele kweli JK kuhusu safari zake but the man believed he was doing the right thing kwa masafari yake yasiyoisha. Na huyu mzee alisafiri hadi sekunde ya mwisho. Kiongozi wa aina yoyote ile anayestahili kuwa kiongozi lazima aamini katika maamuzi yake na kuyatetea ipasavyo.

Hivi mama ameshindwa kusimama na kujenga hoja ya kutushawishi watanzania kwa nini miamala ya simu ni muhimu kwa wakati huu?

Ameshindwa kusimama na kusema, kwa mfano, kwamba nchi yetu imehama kutoka kwenye uchumi wa kutegemea mataifa mengine, na ya kwambaa kuitwa nchi ya uchumi wa kati maana yake ni kwamba ni lazima kama wananchi tujitegemee kwa asilimia kubwa?

Ameshindwa kutetea ongezeko la kodi zake kwa kuutangazia umma wa watanzania kwamba miradi ya kimikakati iliyoachwa na JPM ni ya muhimu sana na ni lazima ikamilike kwa wakati, lakini zinahitaji pesa nyingi?

Ameshindwa kujenga hoja kwamba kwa mfumo wa zamani wa kukusanya kodi pesa ya kuendesha serikali na kutimiza miradi hiyo ya kimikakati ilitegemea kuwakamua watu wachache pesa nyingi, mfumo ambao haukuwa endeleve na ulileta malalamiko mengi na kukwamisha ukuaji wa sekta binafsi?

Ameshindwa kutushawishi watanzania kwamba ni kawaida kwa jambo jipya kama hilo la kukusanya kodi kwa njia ya miamala ni lazima lipokewe kwa mshtuko na watu na hilo linaeleweka, lakini uwaombe watu hao wawe na uvumilivu maana pesa yao inakwenda kufnaya mambo makubwa yatakoyogeuza sura ya nchi yao na kuwafanya wajivunie kuitwa watanzania?

Hakuna sababu ya kutikiswa iwapo unachokifanya unaamini ni sahihi. Sasa utafanya kitu gani ambacho hatutakupigia kelele -- baadhi yetu.

Aisee!
Tatizo kuna mengine pia yanayopigiwa kelele kama vile

1. Mishahara mikubwa ya wanasiasa

2. Kutolipa kodi kwa baadhi yao eg. Wabunge

3. Kutopandisha mishahara miaka 6

Hivyo vitu vitatu vimechangia sana kumrudisha nyuma. Kwa mfano wabunge wangekuwa mifano katika jambo zima la kulipa kodi ANGEPATA UJASIRI WA KUTETEA sasaa ujasiri unatoka wapi wakati wao kodi tu hawalipi.
 
Serikali lazima isikilize wananchi wengi wanatak nini. Hiyo ndio demokrasia.
 
Tulipompigia kelele JK kuhusu safari zake hadi tukamwita Vasco da Gama, serikali yake iliondolewa?

Mlipompigia kelele JPM kuhusu kile mlichokuwa mnakiita udkiteta serikali yake iliondolewa?

Ni kawaida ya raia kutoridhika, uongozi ni kujenga hoja na kuwashawishi watu kwamba maamuzi yako ni sahihi.

Urais ni mgumu, na usipokuwa na uthabiti wa maamuzi hiyo kazi haikufai.
Wananchi walio wengi lazima wasikilizwe wanataka nchi yao iende vipi.
 
Mkuu huna uzoefu na mambo ya serikali. Kuna serikali ziliondolewa katika uongozi kwa kukataa kushusha bei ya mkate tu, sembuse tozo!
Inategemea na nchi na nchi, kwa nchi hi ya MAPIMBI, hata kesho waseme bei ya mafuta ya petrol ni tsh.4000, hakuna la kufanya, zaidi ya kulalamika tu.
 
Acha utoto wewe ...... gang. Hii ni serikali sikivu.
Hakuna cha usikivu wala nini wameshatuona sisi ni MAPIMBI TU!!kabla ya bajeti kwenda bungeni baraza la mawaziri wameipitia, rais hadi amesaini na kuwa sheria, leo imeanza kuwaumiza wanyonge eti, rais ni msikivu ameomba liangaliwe upya?!!tatizo wanalitengeneza wao, kisha wanajifanya kulitatua halafu wanataka sifa tena?!!!
 
Haifai kabisa huu ni udhaifu uliopitiliza,watu tulilopa kodi ya kichwa kwa jasho na damu,tulipigania uhuru kwa jasho na damu afu eti Serikali inaacha kutoka nje kuwaeleza watu kwa nini tozo imeongezeka ,inataka ifanye nini inakuja kusalimu amri kwa ujinga?

Kodi yenyewe ni sio lazima ni unaamua mwenyewe.Rais kanikera Sana bila shaka hata Watendaji wake wamemshangaa.

Kuna mtu wa kutuletea maendeleo nchi hii? Na wapiga. Makelele ndio walikuwa wanashangilia watu kuporwa pesa na kutumbuliwa.

Mwendazake sijawahi mkubali ila kusimamia anachokiamini alikuwa vizuri,miradi mikubwa itaishaje? Changamoto lukuki zitapunguzwaje? Udhaifu Sana huu na kutojiamini.
Siku zote mwizi hawezijiamini, wanafikiria uchaguzi ukifika wataeleza nini
 
Ndugu, sasa aliyetuletea madeni tusiyopaswa kulipa sisi wengine, basi awe na mpango mzuri ukimhusisha yeye mwenyewe 'fairly', kuanzia viongozi wote hadi wananchi, na kuwa na mpango makini na wenye unafuu na tija wa jinsi ya kuyalipa madeni hayo au ktk jinsi ya kugharimia miradi hiyo mikubwa iliyoanzishwa, na sio kukimbilia kuumiza wananchi wengi, bila sababu za msingi......... kazi iendelee.
Nakuunga mkono mtoa mada hii nchi imejaa watu wavivu, walalamishi wasio na majibu afu hawataki kuwajibika.

Tangu lini mwananchi akaenda kununua au kuuza akatoa risiti kama sheria inavyotaka Ili serikali ipate mapato ya kugharamia maendeleo na kujiendesha?

Sasa tozo kama hizi zilikuwa zina offset hapo kwenye Ukwepaji kodi eti Serikali inaenda kusalimu amri,pengo la bajeti litakalojitokeza watatoa wapi pesa? Kukopa kwenye masharti ya kibiashara yanayoumiza zaidi? Hivi watu wanajua kwamba Serikali inatumia karibu Tilioni 10 kulipa madeni yaliyoiva
 
Nimeshangazwa na hili hapa kama ni kweli: Mwigulu: Tumesikia malalamiko ya Watanzania kuhusu tozo za miamala na Rais ametoa maelekezo ya kuzitazama upya

Hivi inawezekanaje serikali (hapa serikali kwa maana ya watendaji wakuu wa serikali, mawaziri wakiwemo na vyombo vyao vinavyowasaidia katika maamuzi ya kisera) kuamua kitu na baadaye ikifikirie upya baada ya kusikilizia mwitikio wa watu?

Hebu imagine, hivi serikali ya aina hiyo itawezaje kweli kufikia malengo yake? Maana serikali ya aina hiyo itakuwa inaamua hili halafu sisi raia tukipiga kelele inaacha kulitekeleza.

Hii ni dalili kubwa kabisa kwamba tunaongozwa na watu dhaifu sijapata kuona. Hata JK hakuwa dhaifu hivi. Tulimpigia kelele kweli JK kuhusu safari zake but the man believed he was doing the right thing kwa masafari yake yasiyoisha. Na huyu mzee alisafiri hadi sekunde ya mwisho. Kiongozi wa aina yoyote ile anayestahili kuwa kiongozi lazima aamini katika maamuzi yake na kuyatetea ipasavyo.

Hivi mama ameshindwa kusimama na kujenga hoja ya kutushawishi watanzania kwa nini miamala ya simu ni muhimu kwa wakati huu?

Ameshindwa kusimama na kusema, kwa mfano, kwamba nchi yetu imehama kutoka kwenye uchumi wa kutegemea mataifa mengine, na ya kwambaa kuitwa nchi ya uchumi wa kati maana yake ni kwamba ni lazima kama wananchi tujitegemee kwa asilimia kubwa?

Ameshindwa kutetea ongezeko la kodi zake kwa kuutangazia umma wa watanzania kwamba miradi ya kimikakati iliyoachwa na JPM ni ya muhimu sana na ni lazima ikamilike kwa wakati, lakini zinahitaji pesa nyingi?

Ameshindwa kujenga hoja kwamba kwa mfumo wa zamani wa kukusanya kodi pesa ya kuendesha serikali na kutimiza miradi hiyo ya kimikakati ilitegemea kuwakamua watu wachache pesa nyingi, mfumo ambao haukuwa endeleve na ulileta malalamiko mengi na kukwamisha ukuaji wa sekta binafsi?

Ameshindwa kutushawishi watanzania kwamba ni kawaida kwa jambo jipya kama hilo la kukusanya kodi kwa njia ya miamala ni lazima lipokewe kwa mshtuko na watu na hilo linaeleweka, lakini uwaombe watu hao wawe na uvumilivu maana pesa yao inakwenda kufnaya mambo makubwa yatakoyogeuza sura ya nchi yao na kuwafanya wajivunie kuitwa watanzania?

Hakuna sababu ya kutikiswa iwapo unachokifanya unaamini ni sahihi. Sasa utafanya kitu gani ambacho hatutakupigia kelele -- baadhi yetu.

Aisee!
Wewe ni mwigulu nchemba.
 
Ndugu, sasa aliyetuletea madeni tusiyopaswa kulipa sisi wengine, basi awe na mpango mzuri ukimhusisha yeye mwenyewe 'fairly', kuanzia viongozi wote hadi wananchi, na kuwa na mpango makini na wenye unafuu na tija wa jinsi ya kuyalipa madeni hayo au ktk jinsi ya kugharimia miradi hiyo mikubwa iliyoanzishwa, na sio kukimbilia kuumiza wananchi wengi, bila sababu za msingi......... kazi iendelee.
Kwa hiyo wewe kwa uelewa wako mfupi kuumiza wananchi ni kwenye Kodi tuu?

Unapokuwa huna umeme, barabara,shule, hospital,maji nk huumii?

Utatoka vipi kwenye umaskini? Hakuna ku move bila kuumia haipo hiyo na ukiwa maskini ndio unaumia kwenye kila kitu
 
Hapo ndipo ninapowakubali wanasiasa wasiofikiri in terms ya kupata au kukosa kura. Na ukweli wa mambo serikali hukubalika kwa sababu ya uimara wake katika kutekeleza yaliyomo kwenye ilani yake ya uchaguzi.

You’re trash!! Zao la KAYAFA wa chato
 
nchi yetu ipo kwenye mfumo wa utawala ambapo mtu akishateuliwa kuwa kiongozi anajitwalia uhalali wa kuwaza kwa ajili ya walio chini yake. kwa maneno mengine viongozi wetu wanadhani wanatushikia akili.

kwamba anadhani kwa kuwa kwake kiongozi basi wale anaowaongoza wanajitoa akili zao na kumkabidhi huyo kiongozi na wao wanabaki vichwa nazi.

matokeo yake ni hawa viongozi kujifungia vyumbani na kutunga sera na miongozo bila kupata public ipinion.

inakera sana.
 
Kwa hiyo wewe kwa uelewa wako mfupi kuumiza wananchi ni kwenye Kodi tuu?

Unapokuwa huna umeme, barabara,shule, hospital,maji nk huumii?

Utatoka vipi kwenye umaskini? Hakuna ku move bila kuumia haipo hiyo na ukiwa maskini ndio unaumia kwenye kila kitu
Nchi za Scandnavia ndizo zinazoongoza kwa kulipa kodi. Kule mtu anapigwa kodi hadi utabaki unashangaa.

Cha kushangaza zaidi wananchi wanafurahia utaratibu wao huo wa kodi kubwa. Kwa nini?

Kwa sababu kila raia anapata huduma ya afya first class bila kujali kipato chao.

Kwa sababu barabara zao ni za kiwango cha lami cha kwanza kuanzia mjini hadi vijijini.

Kwa sababu kila raia ana fursa ya kupata elimu hadi chuo kikuu kwa ruzuku ya serikali.

Labda hawa jamaa wanaoitwa viongozi wetu waliweka hayo makodi bila kuwa na nia ya ndani kabisa ya kuhakikisha kila senti ya kodi ya mtanzania inatumika kuleta tofauti katika sura ya nchi yetu na maisha ya watu wetu. After all JPM alikuwa mtu mmoja tu wa aina yake tofauti kati ya lundo la wanasiasa ambao kwao hawana nia ya dhati ya maono na usimamizi katika kufikia ndoto za nchi yetu.

Ndio maana hawa wakiyumbishwa tu na kelele wanakimbilia shimoni kama panya aliyesikia kelele za nyau.

Kuna mtu mmoja hapo juu amehoji, Hivi kwa uongozi wa aina hii hivi hata SGR, Nyerere Dam vingethubutu hata kuanza?

Uongozi wa aina hii ungeweza kuja na msimamo thabiti na wa aina yake kwamba no lock down?

Demokrasia siyo kuyumba katika maamuzi, huo ni udhaifu. Demokrasia ni kuja na maono na mawazo shirikishi, lakini ikifika wakati wa kutekeleza uthabiti wa maamuzi utahitajika.
 
Sasa unadhani huduma ilianza kabla ya kodi? Kodi zilianza ndio huduma zikafuatia,ilitakiwa Serikali iseme tumewwka tozo x kwa ajili ya kufanya y z ndio yasipofanyika inakuwa haki kulalamika sio kukataa kulipa kodi na Serikali inasikiliza hili jambo afu mwisho wa siku huduma zitakuaje kama Hali ndio hii? Kwamba imekuwa nchi ya kila mtu atajijua au?
 
Nimeshangazwa na hili hapa kama ni kweli: Mwigulu: Tumesikia malalamiko ya Watanzania kuhusu tozo za miamala na Rais ametoa maelekezo ya kuzitazama upya

Hivi inawezekanaje serikali (hapa serikali kwa maana ya watendaji wakuu wa serikali, mawaziri wakiwemo na vyombo vyao vinavyowasaidia katika maamuzi ya kisera) kuamua kitu na baadaye ikifikirie upya baada ya kusikilizia mwitikio wa watu?

Hebu imagine, hivi serikali ya aina hiyo itawezaje kweli kufikia malengo yake? Maana serikali ya aina hiyo itakuwa inaamua hili halafu sisi raia tukipiga kelele inaacha kulitekeleza.

Hii ni dalili kubwa kabisa kwamba tunaongozwa na watu dhaifu sijapata kuona. Hata JK hakuwa dhaifu hivi. Tulimpigia kelele kweli JK kuhusu safari zake but the man believed he was doing the right thing kwa masafari yake yasiyoisha. Na huyu mzee alisafiri hadi sekunde ya mwisho. Kiongozi wa aina yoyote ile anayestahili kuwa kiongozi lazima aamini katika maamuzi yake na kuyatetea ipasavyo.

Hivi mama ameshindwa kusimama na kujenga hoja ya kutushawishi watanzania kwa nini miamala ya simu ni muhimu kwa wakati huu?

Ameshindwa kusimama na kusema, kwa mfano, kwamba nchi yetu imehama kutoka kwenye uchumi wa kutegemea mataifa mengine, na ya kwambaa kuitwa nchi ya uchumi wa kati maana yake ni kwamba ni lazima kama wananchi tujitegemee kwa asilimia kubwa?

Ameshindwa kutetea ongezeko la kodi zake kwa kuutangazia umma wa watanzania kwamba miradi ya kimikakati iliyoachwa na JPM ni ya muhimu sana na ni lazima ikamilike kwa wakati, lakini zinahitaji pesa nyingi?

Ameshindwa kujenga hoja kwamba kwa mfumo wa zamani wa kukusanya kodi pesa ya kuendesha serikali na kutimiza miradi hiyo ya kimikakati ilitegemea kuwakamua watu wachache pesa nyingi, mfumo ambao haukuwa endeleve na ulileta malalamiko mengi na kukwamisha ukuaji wa sekta binafsi?

Ameshindwa kutushawishi watanzania kwamba ni kawaida kwa jambo jipya kama hilo la kukusanya kodi kwa njia ya miamala ni lazima lipokewe kwa mshtuko na watu na hilo linaeleweka, lakini uwaombe watu hao wawe na uvumilivu maana pesa yao inakwenda kufnaya mambo makubwa yatakoyogeuza sura ya nchi yao na kuwafanya wajivunie kuitwa watanzania?

Hakuna sababu ya kutikiswa iwapo unachokifanya unaamini ni sahihi. Sasa utafanya kitu gani ambacho hatutakupigia kelele -- baadhi yetu.

Aisee!
Hizo tozo ni mzigo kulingana na hali ya uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Pili sio kupenda kwao. Miamala imeshaanza kudorola imebidi washtuke maana kinachoenda kutokea ni wao kukosa hata kile kidogo walichokua wanakipata kupitia VAT ya ada za miamala

Hivi unadhani kama mzunguko wa miamala ungekua kama zamani wangejari kelele? Si unakumbuka juzi tu mwigulu alisema tutazoea tu? Unafikiri alikurupuka? Alisema kutoka moyoni kuonyesha they don't care hata tukilalamika.....

Ngoma imenoga watu wamegoma kuweka hela ambayo inakatwa mpaka kichwa kinauma. Hela yenyewe unaipata kwa mbinde
 
Tulipompigia kelele JK kuhusu safari zake hadi tukamwita Vasco da Gama, serikali yake iliondolewa?

Mlipompigia kelele JPM kuhusu kile mlichokuwa mnakiita udkiteta serikali yake iliondolewa?

Ni kawaida ya raia kutoridhika, uongozi ni kujenga hoja na kuwashawishi watu kwamba maamuzi yako ni sahihi.

Urais ni mgumu, na usipokuwa na uthabiti wa maamuzi hiyo kazi haikufai.
Ni mgumu zaidi ukitaka kiendesha nchi kwa hisia zako na sio uhalisia.

Tunataka mambo makubwa wakati hatujajenga miundo mbinu ya kuyafikia hayo makubwa. Maendeleo ni hatua. Ni sawa na ukuaji kwa viumbe hai....

Hivi ni nani atakuelewa akatwe hela kubwa wakati mlo mmoja tu ni shida kwake?
Hivi bora ufe na njaa wewe na familia yako ili hela ikajenge nyumba za wastaafu?

Ni tahira peke yake atakubali upumbavu huo.

Leo hii mnakuja na ngonjera za kisengerema. Juzi kati tu hapa mnataka mtumie zaidi ya mil 400 kujenga sanamu. Hivi tupo serious kweli na maisha ya watanzania?
 
Tulipompigia kelele JK kuhusu safari zake hadi tukamwita Vasco da Gama, serikali yake iliondolewa?

Mlipompigia kelele JPM kuhusu kile mlichokuwa mnakiita udkiteta serikali yake iliondolewa?

Ni kawaida ya raia kutoridhika, uongozi ni kujenga hoja na kuwashawishi watu kwamba maamuzi yako ni sahihi.

Urais ni mgumu, na usipokuwa na uthabiti wa maamuzi hiyo kazi haikufai.
Huyo ni upinzani hawezi kukuelewa. Uongozi ni lawama cheap popularity ni hatari katika uongozi
 
Sasa unadhani huduma ilianza kabla ya kodi? Kodi zilianza ndio huduma zikafuatia,ilitakiwa Serikali iseme tumewwka tozo x kwa ajili ya kufanya y z ndio yasipofanyika inakuwa haki kulalamika sio kukataa kulipa kodi na Serikali inasikiliza hili jambo afu mwisho wa siku huduma zitakuaje kama Hali ndio hii? Kwamba imekuwa nchi ya kila mtu atajijua au?
Kwamba itakuwa nchi ya kila kitu kitajijua? Bonge la swali.

Nchi ina watu milioni 60, walipa kodi rasmi idadi yao haifiki hata milioni 10 (na walio wengi kati ya hao ni wafanyakazi wanaokatwa over 30% ya mshahara wao kila mwezi kwa kodi tu PAYE).

Then kodi ya miamala ingewagusa walau hao wengine ambao kiukweli ndio walio wengi, but hawajulikani katika vitabu vya kodi vya serikali lakini wanawajibika pia katika kuijenga nchi yao.

Tusitake kuitana majina yasiyo na sababu za msingi, eti watanzania wa chini. Hakuna cha mtanzania wa chini au wa juu wote ni watanzania na hii nchi tuliambiwa ni nchi ya kijamaa.

Hapa kinachokosekana ni kiongozi wa kujenga hoja za ushawishi na kusisimua ili hii kodi ionekane ya kawaida, ya lazima na ya kuleta mabadiliko.
 
Ni mgumu zaidi ukitaka kiendesha nchi kwa hisia zako na sio uhalisia.

Tunataka mambo makubwa wakati hatujakenga miundo mbinu ya kuyafikia hayo makubwa. Maendeleo ni hatua. Ni sawa na ukuaji kwa viumbe hai....

Hivi ni nani atakuelewa akatwe hela kubwa wakati mlo mmoja tu ni shida kwake?
Hivi bora ufe na njaa wewe na familia yako ili hela ikajenge nyumba za wastaafu?

Ni tahira peke yake atakubali upumbavu huo.

Leo hii mnakuja na ngonjera za kisengerema. Juzi kati tu hapa mnataka mtumie zaidi ya mil 400 kujenga sanamu. Hivi tupo serious kweli na maisha ya watanzania?
"Tunataka mambo makubwa wakati hatujakenga miundo mbinu ya kuyafikia hayo makubwa."

JPM alipokuwa akitumia muda mwingi akitetea miradi yake ya miundombinu mlikuwa mnasemaje?

Si mlikuwa mkipiga kelele oh maendeleo ni watu sio vitu?

Sasa nakushangaa leo unasema tena kwamba miundombinu ni muhimu kuyafikia hayo maendeleo. Duh!

Ni hivi hakuna kitu ambacho kiongozi yeyote atafanya/atatekeleza asipigiwe makelele. Mimi namtaka kiongozi anayeamini kwamba kile anachokifanya ni sahihi na awe tayari kukitetea kwa kauli na kwa matendo. Walipokuwa wanaweka hizo kodi walikuwa hawana maono ya nini wanataka kufanya kwa kupitia kodi?
 
Back
Top Bottom