Mr mutuu
JF-Expert Member
- Jan 27, 2023
- 2,869
- 14,501
Nimerudi nyumbani kutoka mahali ninapofanyia shughuli zangu, nimekutana na kitu kinanipa mawazo sana.
Mwanangu wa kwanza (4yrs old) alikuwa anapenda shule sana, mwaka jana alikuwa anasoma shule si mbali sana na hapa, walikuwa wanatoka saa 6 mchana, sasa mwaka huu nikaona nimtafutie nursery bora angalau hata mwakani aanze la kwanza.
Aisee sasa hivi ndio nimekaa nyumbani, yapata muda kidogo wife alinambia siku hizi dogo hapendi shule, nikamwambia labda hajapata marafiki hiyo shule mpya!
Sasa hawa watoto wa nursery wanaamka saa 11:30 saa 12 gari lipo getini, kutoka shule saa 12, homework kibao, mtoto muda wote namuona kachoka.
Leo kaamshwa kwenda shule mtoto analia tu, yaani hawa watoto wana ratiba ngumu kuliko hata watumishi, hivi kweli nursery mkiwaachia saa 7 kuna tatizo gani? Wanacheza na kurelax saa ngapi hawa watoto?
Leo naenda kukiwasha shuleni, mwanangu mwisho saa 8 atakua anakuja kuchukuliwa anapelekwa nyumbani, kama hawataki poa tu nitatafuta shule nyingine, uzuri private zipo kama utitiri.
Serikali wekeni miongozo ya elimu, hwa watoto wana ratiba ngumu hata physiological sidhani kama wanafurahia shule kama miaka yetu ile.
Elimu yenyewe hii ya kuja kukutana na mishahara ya laki 4 ukitoka chuo, upuuzi tu!