Serikali ingilieni kati, huu mfumo wa elimu utasababisha watoto waanze kuichukia shule

Serikali ingilieni kati, huu mfumo wa elimu utasababisha watoto waanze kuichukia shule

Hakutakua na mfumo bora wa elimu bila raia kupigania.

Wana shida gani kwani!, Watoto wao wanasoma abroad.

Ubinafsi wa hao Mbweha umeshaua taifa.
 
Sema wazazi mnazingua sana, mtu anakaa Kibamba anampeleka mtoto nursery ya kimara mwisho wakati kuna nursery za karib ambazo mtoto angeamka saa 1 na nusu

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Shule siku hizi nyingi sana, mpeleke mwanao shule ambayo itasababisha akue vyema na sio presha ya kukariri

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Bado hapo hawajaanza bebeshwa macounterbook.
Mie yalinikuta haya ya makaunta book. Mtoto darasa la 3 anabebeshwa kaunta book 12. Sita ya classwork na 6 ya homework. Walau ingekuwa quire 1. Sasa ni quite 2.. mwisho wa siku mgongo unapinda. Sababu eti wanawaandaa kuingia la nne wasiteseke
 
Nimerudi nyumbani kutoka mahali ninapofanyia shughuli zangu, nimekutana na kitu kinanipa mawazo sana.

Mwanangu wa kwanza (4yrs old) alikuwa anapenda shule sana, mwaka jana alikuwa anasoma shule si mbali sana na hapa, walikuwa wanatoka saa 6 mchana, sasa mwaka huu nikaona nimtafutie nursery bora angalau hata mwakani aanze la kwanza.

Aisee sasa hivi ndio nimekaa nyumbani, yapata muda kidogo wife alinambia siku hizi dogo hapendi shule, nikamwambia labda hajapata marafiki hiyo shule mpya!

Sasa hawa watoto wa nursery wanaamka saa 11:30 saa 12 gari lipo getini, kutoka shule saa 12, homework kibao, mtoto muda wote namuona kachoka.

Leo kaamshwa kwenda shule mtoto analia tu, yaani hawa watoto wana ratiba ngumu kuliko hata watumishi, hivi kweli nursery mkiwaachia saa 7 kuna tatizo gani? Wanacheza na kurelax saa ngapi hawa watoto?

Leo naenda kukiwasha shuleni, mwanangu mwisho saa 8 atakua anakuja kuchukuliwa anapelekwa nyumbani, kama hawataki poa tu nitatafuta shule nyingine, uzuri private zipo kama utitiri.

Serikali wekeni miongozo ya elimu, hwa watoto wana ratiba ngumu hata physiological sidhani kama wanafurahia shule kama miaka yetu ile.

Elimu yenyewe hii ya kuja kukutana na mishahara ya laki 4 ukitoka chuo, upuuzi tu!

Wazazi wa siku hizi sijui mna nini!?
Yaani mko selfish kupitilizaaaa. Unamuamsha mtoto wa miaka 4 saa11 alfajiri ili akakuletee nini huko shuleni!?
Unampeleka mtoto arasa la kwanza akiwa na miaka5 ili iweje?
Mbona mnawaonea hawa watoto!??? Yaani Mungu anakupa pesa, pesa inakupeleka kuwa mtumwa wa kuitumia bila kufikiri!?

Kama unampenda mwanao miaka minne kushuka chini unatakiwa uamue kwenda kuishi jirani na shule unayompeleka ili hata akiamka saa moja aende; au mpe homeschooling, tumia hiyo pesa kuajiri walimu watakaomfuata nyumbani

Mimi kanuni yangu ya malezi siwezi ishi umbali wa zaidi ya km 5 kwenda shuleni kwa mtoto wa primary
 
Wazazi ndo mafala, mnaendekeza ujinga.
Omba ratiba ya masomo, mtoto aende na hayo madaftari pekee

Mi enzi nasoma vipindi vilikuwa masomo 3 tu kwa siku

Elimu ya siku hizi shule zote zafanana hakuna kipya, mpeleke mtoto shule ya karibu na unapoishi

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Shule nzuri kwa malezi ya watoto ni nadra sana za hizi... kila mtu yuko upande wake tu office politics pia za kutosha...
madogo wanapeeq homework sababu administratuin ya shule inataka walimu wafanye hivyo wasipofanya wanaonekana hawafanyi kazi...

Walimu nao wanapiga kazi mfukulizo kuwachosha watoto wetu ili waonekane wanafanya kazi na maboss wao hii ni private sector...

Huko serikalini bora liende tu dogo ajue asijue mtajua wenyewe...

Huko mbele tutakua na kizazi ccha kifala sana yani...

Tutaendelea kutawaliwa na wenye hela tu maana wao ndo wanaweza kuafford education system zenye maana...

Kuna mtaala sijui IB sijui cambridge wanawapunguzia watoto masomo mizigo isiyo na maana... washafutaga history na vitu vingine wanadil na science and math tu.... sa we dunia hii unakamririsha dogo mambo ya mwanemutapa sijui mansa mussa wapi na wapi...

Anywei education system is fucked trust me tuna walimu wachache sana wanaojua kulea watoto... wengi wanafanya tu kama kazi mshahara usome mwisho wa mwezi basi...

Hizi yellow buses za wanafunzi unakutana nazo mida ambayo watu wanafanya jogging asbh ss vitoto vishashwa mda huo yani vimevaa uniform vinaenda shule basi linakura route za kutosha dar nzima akifika shule kashajichokea unadhan atajifunza vp
 
Labda wanaamini wazazi wengi muda wa saa 7 wanakuwa wako kazini kwahiyo wanawachelewesha ili wakutane jioni.
Hiyo ni kwa sababu wapo wazazi huwapeleka watoto nursery kama kumtunza tu(huku alison's) wakati yeye akiwa kazini.
Wengi naona hata hawajui kwa nini wanawapeleka huko
 
Tutafute hela tuwasomeshe watoto mitaala tofauti na NECTA, wakati huo huo tukiwekeza ili waje waendeleze

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Wazazi ndo wanaendekeza huu upuuzi..why mtoto asiende nursery ya karibu alale Hadi Saa moja asubuhi...

Tena simu hizi kuna homework za mzazi na mtoto eti za weekend yoote au likizo yoote ...kutesa Tu watoto
 
Serikali kupitia wizara ya elimu hawawezi kuja na miongozo kwani? Wanakula Kodi zetu afu wanashindwa kusimamia vitu vidogo kama hivi, anyway kwa kutambua nchi yangu ni kichwa Cha mwendawazimu Leo saa 10 naenda kukiwasha, wakikataa nakubali hasara namuhamishia shule nyingine

Kipindi natafuta shule nilipewa recommendation tu na mtu wangu wa karibu wife ndo alienda tulifanya kosa kutojua ratiba zao

Ila kwa huu upuuzi mi mwanangu hapana aisee
Yaani hizi shule zina ujinga mwingi. Mwanangu darasa la kwanza wanatoka saa 11, anafika home saa 12, kachoka hawezi lolote, kapungua balaa. Namhamisha shule hii term ijayo, potelea mbali. Mimi nimesoma kayumba na sikuteseka hivyo na shule.
 
Wazazi ndo wanaendekeza huu upuuzi..why mtoto asiende nursery ya karibu alale Hadi Saa moja asubuhi...

Tena simu hizi kuna homework za mzazi na mtoto eti za weekend yoote au likizo yoote ...kutesa Tu watoto
Wee hata za karibu ni shida tupu. Wanashinda huko kutwa
 
Shule siku hizi nyingi sana, mpeleke mwanao shule ambayo itasababisha akue vyema na sio presha ya kukariri

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Shule ya karibu na nyumbani wanachapa sana wanafunzi, mtoto akipata chini ya 80 atakula fimbo za maana. Siku moja nilipita nikasikia watoto wanalia balaa, kuuliza naambiwa wanakula mboko sana
 
Back
Top Bottom