herikipaji
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 1,198
- 1,369
Mie yalinikuta haya ya makaunta book. Mtoto darasa la 3 anabebeshwa kaunta book 12. Sita ya classwork na 6 ya homework. Walau ingekuwa quire 1. Sasa ni quite 2.. mwisho wa siku mgongo unapinda. Sababu eti wanawaandaa kuingia la nne wasitesekeBado hapo hawajaanza bebeshwa macounterbook.
Wanapewa sana homeworkMtoto wa miaka minne homework ya nini? Hao walimu kweli ni wa nursery?
Amandla...
Nimerudi nyumbani kutoka mahali ninapofanyia shughuli zangu, nimekutana na kitu kinanipa mawazo sana.
Mwanangu wa kwanza (4yrs old) alikuwa anapenda shule sana, mwaka jana alikuwa anasoma shule si mbali sana na hapa, walikuwa wanatoka saa 6 mchana, sasa mwaka huu nikaona nimtafutie nursery bora angalau hata mwakani aanze la kwanza.
Aisee sasa hivi ndio nimekaa nyumbani, yapata muda kidogo wife alinambia siku hizi dogo hapendi shule, nikamwambia labda hajapata marafiki hiyo shule mpya!
Sasa hawa watoto wa nursery wanaamka saa 11:30 saa 12 gari lipo getini, kutoka shule saa 12, homework kibao, mtoto muda wote namuona kachoka.
Leo kaamshwa kwenda shule mtoto analia tu, yaani hawa watoto wana ratiba ngumu kuliko hata watumishi, hivi kweli nursery mkiwaachia saa 7 kuna tatizo gani? Wanacheza na kurelax saa ngapi hawa watoto?
Leo naenda kukiwasha shuleni, mwanangu mwisho saa 8 atakua anakuja kuchukuliwa anapelekwa nyumbani, kama hawataki poa tu nitatafuta shule nyingine, uzuri private zipo kama utitiri.
Serikali wekeni miongozo ya elimu, hwa watoto wana ratiba ngumu hata physiological sidhani kama wanafurahia shule kama miaka yetu ile.
Elimu yenyewe hii ya kuja kukutana na mishahara ya laki 4 ukitoka chuo, upuuzi tu!
Hao ndo wengine wanachokea kwenye vituo vya daladala.Mlete asome dumu fagio shule za serikali
Wengi naona hata hawajui kwa nini wanawapeleka hukoLabda wanaamini wazazi wengi muda wa saa 7 wanakuwa wako kazini kwahiyo wanawachelewesha ili wakutane jioni.
Hiyo ni kwa sababu wapo wazazi huwapeleka watoto nursery kama kumtunza tu(huku alison's) wakati yeye akiwa kazini.
Yaani hizi shule zina ujinga mwingi. Mwanangu darasa la kwanza wanatoka saa 11, anafika home saa 12, kachoka hawezi lolote, kapungua balaa. Namhamisha shule hii term ijayo, potelea mbali. Mimi nimesoma kayumba na sikuteseka hivyo na shule.Serikali kupitia wizara ya elimu hawawezi kuja na miongozo kwani? Wanakula Kodi zetu afu wanashindwa kusimamia vitu vidogo kama hivi, anyway kwa kutambua nchi yangu ni kichwa Cha mwendawazimu Leo saa 10 naenda kukiwasha, wakikataa nakubali hasara namuhamishia shule nyingine
Kipindi natafuta shule nilipewa recommendation tu na mtu wangu wa karibu wife ndo alienda tulifanya kosa kutojua ratiba zao
Ila kwa huu upuuzi mi mwanangu hapana aisee
Wee hata za karibu ni shida tupu. Wanashinda huko kutwaWazazi ndo wanaendekeza huu upuuzi..why mtoto asiende nursery ya karibu alale Hadi Saa moja asubuhi...
Tena simu hizi kuna homework za mzazi na mtoto eti za weekend yoote au likizo yoote ...kutesa Tu watoto
Angalau hataamka Saa kumi na moja....Wee hata za karibu ni shida tupu. Wanashinda huko kutwa
Shule ya karibu na nyumbani wanachapa sana wanafunzi, mtoto akipata chini ya 80 atakula fimbo za maana. Siku moja nilipita nikasikia watoto wanalia balaa, kuuliza naambiwa wanakula mboko sanaShule siku hizi nyingi sana, mpeleke mwanao shule ambayo itasababisha akue vyema na sio presha ya kukariri
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Nawaona saa 12 wanaenda shule kwa mguu, najiuliza ,saa hii wanaenda kufanya niniAngalau hataamka Saa kumi na moja....