Serikali inunue umeme Ethiopia, tatizo ni kubwa mno. Pole Biteko

Ukinunua- utanunuaje na hauna dolla? Ethiopia hawataki dolla?

Halafu unaongelea Ethiopia - Tanzania, hiyo load ya umeme itakuwa remote? Wireless? High Tension Transmission kutoka Ethiopia hadi Dar nani atagharimia? Kwa nini hizo pesa zisimalizie miundo mbinu ya kwetu?
 
Kama tatizo la umeme ,lipo kwenyelevel za Kalemani, Makamba, au Dotto basi tunashida kubwa ( whichi is obvious) Kam Taifa!
 
Kwani huyo makamba alikopa hizo trilioni zifanye kazi ya umeme au ilikuwa kupitishia tu huko katika namna ya kuiba?
Wazo lako ni kununua umeme kutoka Ethiopia
 
Umeme ni biashara kubwa sana serikali mambo ya biashara sifuri kabisa suluhu makampuni ya biashara yaingie ubia na serikali.

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Hizo gharama za kununua umeme Ethiopia ni upuuz na sio sustainable na viable kiuchumi ,kuna gharama kubwa za kujenga power transmission lines na miundombinu ,wakati tungeweza kutumia pesa hizo na kuongezea kiasi ili kujenga kinu cha nuclear kufua umeme na kuanza kuvuna Uranium yetu pale Dodoma kwa ajili ya uzalishaji wa nishati ya umeme ,kitu ambacho ni sustainable in the future ,
Ukizingatia hata mabadiliko ya hali ya hewa yanaongezeka hivyo hata kufua umeme kwa kutumia maji sio sustainable in the future kwani maji yanapungua kwenye vyanzo vya maji .

Pia tungeweza kuwekeza kwa kujenga vinu vipya vya kufua umeme kwa kutumia makaa ya mawe ,tuna reserve kubwa ya makaa ya mawe nchi hii kule Songea ,Mbeya ,Njombe , Rukwa nk .na huu ndio mfumo wa bei rahisi kabisa wa kufua umeme ,cost za kujenga hivi vinu vya kufua umeme kwa joto (thermal power plant ) ni cheapest kabisa ukilinganisha na njia nyingine za kufua umeme ,
Why tumeshindwa hilo ? ,Kila siku tunaleta visingizio vya kipuuz ,
 
Tatizo la umeme katika nchi yenye mito, gesi, volcano, makaa ya mawe, upepo na jua ni ya kujitakia.
Tunaongozwa na watu wenye akili finyu ,that's all .Nchi yoyote yenye watu wenye akili ,public utilities hasa umeme na nishati kiujumla sio kitu cha kuleta masikhara kabisa .
Ni nchi wapumbavu kama hii ndio utakuta mambo kama haya
 
Halafu hawa wapumbavu TANESCO si ndio walisamehe deni la bilioni 60 walilokuwa wanaodai serikali ya Zanzibar ?
Pumbavu sana
 
Magu aliunganisha wsteja wengi kuliko awamu zote, hatukuona umeme ukikatika,
Ngoja niwaeleze
Umeme unakatika, maji yanakatika, mafuta yanakatia, bei zinapaaa usiku na mchana.
Tuacheni kuongea siasa hawa ccm nchi imewashinda
Huyo hajielewi tu
 
Suala la dollar limeumiza sana makampuni ya kigeni hasa ya mafuta, uendeshaji umekuwa mgumu sana kwenye shughuli zao za kila siku na serikali ipo kimya wala hawana mpango wa namna ya kutatua hili tatizo la kukosekana kwa dollar
 
Na huku bwawa la stigler gorge limeanza kutoa nyufa, wabongo sijui tunakwama wapi.
 
Kwani hamna nishati ya Geothermal(mvuke)hapo bongo ilhali mpo kwenye eneo la bonde la ufa?
Hapa Kenya tunaujuzi wa kuvua Geothermal miaka za kutosha tu na kupelekea hata Uhabeshi kukodisha kampuni yetu ya kiserikali (KenGen) kuwavunia nishati hiyo.
Nishati hutafutwa na njia zote,iwe upepo,maji,nyuklia,mvuke(geothermal),jua,mkaa na kadhalika.
Mpo wengi kutuzidi labda sijui tu kiasi Cha matumizi yenu lakini pia mkumbuke mna mradi wa treni za umeme.
Kwa hivyo msijisahaulishe kuwa majuto ni mjukuu,huja kinyumenyume.
Hata hivyo nafahamu mna gesi ya kumwaga labda mnahitaji tu subira.
Mtaarifuni mama.
 
Anasema
Wananchi wataka umeme na bodi aliyenayo ileile ,mkurugenzi yuleyule
 
Bei itapungua tutakapokuwa na uwezo wa kujenga miradi wenyewe kwa kutumia wataalamu wetu.
Kwa sasa miradi yote mikubwa ni kuendeleza mataifa yaliyotuletea contractors, kuanzia barabara, maji, reli tunaoendeleza China. Hata bwawa la Nyerere mchina amefanya kazi ya kujenga tuta kuu. Hivyo pesa yetu imepitia Misri kwenda China. SGR imeenda Uturuki.
Hizi hadithi za wanasiasa wetu kwamba ni maendeleo kujengewa barabara zote na miradi mikubwa ya maji baada ya miaka 60 ya uhuru ni za kupuuzwa, kizazi kipya kijenge uwezo wa ndani ili kupata maendeleo ya kweli na endelevu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…