Wasomba
JF-Expert Member
- Dec 19, 2016
- 559
- 818
Hali ilivyo katika maeneo mengi ya bonde la Kilombero ni ya kusikitisha sana. Maeneo karibia yote yaliyokuwa yakitumika kwa shughuli za kilimo yamechukuliwa na serikali kwa kigezo cha kuhifadhi ardhi oevu na pia kuhakikisha mradi wa umeme wa bwawa la mwalimiu Nyerere una sustainability.
Matokeo yake uchumi katika maeneo karibia yote ya tarafa ya Lupiro, Mtimbira na Malinyi uko na hali mbaya sana na inayosikitisha. Njaa imekuwa tishio kubwa katika maeneo hayo. Biashara nyingi za watu zinekufa na watu wengi wamekosa ajira. Mfano katika Kijiji cha Lupiro pekee Kuna magodauni makubwa zaidi ya 90 ya kuhifadhi mpunga ambayo yote yamefungwa kwa kukosa malighafi. Idadi ya biashara za maduka zikizofungwa ni ya kusikitisha sana achilia mbali nyumba za kulala wageni na biashara nyingine lukuki.
Wananchi wa eneo hilo wangekuwa wanyonge wasiyo na mtu wa kuwapigania. Wabunge wangekuwa kimya pasipo kulipigia kelele jambo hilo. Kupitia ujumbe huu naiomba kwa unyeyekevu mkubwa serikali sikivu ya Rais Samia irudishe baadhi maeno ya ardhi hiyo ya kilimo kwa wananchi ili kupunguza athari hizo ambazo zinazidi kujua. Ni matumaini yangu kuwe serikali italifanyia kazi jambo hilo.