Serikali isikubali kutangaza “total lockdown” au Karantini. Wanaoishawishi ama hawajui wanachokishauri au ni wabinafsi

Togolani, you are missing the point, dhumuni la msingi la Total lockdown sio kuzuia Covid 19, ni kupunguza rate ya maambukizi. Point hiyo tu imenifanya nikuone hujui unachokitetea.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndugu Chesty nashukuru kwa elimu. Ila bahati mbaya umeitoa mahali pasipo sahihi. Kwa unaajiaminisha kabisa kwamba mimi naweza kukurupuka kuandika dhana/concept/idea nisiyojua ina maana gani? Umesoma bandiko langu au umekimbilia majibizano na Rebeca 83 ambayo hujui yalipoanzia?
 
Hivi dada unaamini kuwa Togolani atakuelewa, mtu ambaye hajui hata dhana ya Lock-down, anasema nia ni kuzuia COVID 19, mtu kama huyu siwezi kupoteza muda kuongea nae.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ooh, dear Chesty!! You must be a very angry person and I am very sorry about that. Calming down and respecting others is a healthy practice in so many ways. Give it a try.
 
Nimeshawaelezea kwamba mimi sio Togolani munayemdhania. Tafadhali usimchafue kwenye makosa ya mjadala wangu. Pia unajichanganya sana kuhusisha siasa na mjadala huu.
 
Pangueni (elezeeni) hoja yake ya kukaa kwenye hiyo karantini sijui lokidauni tutaimudu vipi hali hiyo sisi wabangaizaji... siyo mnatuletea ujinga tu hapa eti "oo, mimi na familia yangu tumeshachukua hatua hatuna haja ya kumsubiri huyo Magufuli" sasa hiyo si wewe mwenye vijisenti na ubinafsi wako je sisi wengine!? pambaf kabisa
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Its true unapinga lockdown sababu haizuii vifo na hakuna theory inayosupport this,wakati nimekuambia lockdown inapunguza rate ya maambukizi,na hio inaweza kuwa proved kisayansi kwa kuangalia statistics...unasema unaleta concepts usiyoijua ..je na wale walio implement lockdown kwenye nchi zao..hawajui cha kufanya pia??
 
Mimi niwaulize tu waungwana;

Eti kipi bora (chagua moja) kati ya

A.kujifungia ndani UKAFA au UKAATHIRIKA kwa kukosa mahitaji ya msingi kama mlo wakati uwezo wa kwenda kutafuta chakula ulikwepo ila kwa tahadhari tu (hukutoka kwakuwa) umehofia kupatwa (au pengine kusambaza) virusi vya maradhi

AU

B.kwenda kujitafutia mahitaji msingi (mfano chakula) na kisha UKAATHIRIKA au UKAFA kutokana na virusi vya maradhi vilivyosambaa na kuenea katika mji


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikushauri tena mdogo wangu. Jitahidi kujadili mada objectively by focusing on the subject matter. Hoja zako zinarukaruka sana kiasi kwamba inakua ngumu mtu kukujibu maana kila unapoibuka kuna jipya. Hii mada haikulenga kuhoji lockdown inafanya kazi au haifanyi. Imelenga kujadili utekelezaji wake kwa nchi kama yetu.

Nimekuuliza maswali mengi hujajibu. Nilikutegemea hadi sasa kwa wingi wa comments ambazo umetoa, ungekua umedraft mapendekezo ya jinsi ya kuitekeleza Tanzania kwa data. Kwa kufanya hivyo ungekua umeonesha ukweli tofauti na niliouchambua mimi. Otherwise, naona kama unatumia makusudi unapoanza kujadili iwapo mimi sijui maana ya lockdown na nini malengo yake. Seriously? Walisema akutukane hakuchagulii tusi.

Cheers

MM Togolani
 


Asante mkuu..kwa kunipongeza kwa 'kukomaa nae'..lol..

Ni kweli kuna cases mpya za coronavirus Italy..kila siku, but I believe hii ni matokeo ya kuwa na watu wengi kuwa infected initially, kwa kuwa wameweka lockdown sasa hivi,hawa walio na virusi watapunguza maambukizi...narudia kupunguza maambukizi na sio kuzuia 100% maambukizi...

Mtu mmoja kutoka nje unaona ni maafa?? je tukiruhusu wote watoke nje freely huoni impact ni kubwa zaidi??

Ni vizuri,kama mnafata njia nyingine za kupunguza kasi ya ueneaji,but this doesnt mean mui underate lockdown,kama ukisafisha mikono,umezuia watu 5,kama umefanya social distance umezuia watu 5 wasipate infection,hao ni watu kumi,huoni ukifanya lockdown utaongeza idadi ya wengine 5 wasipate infection..je huoni kufata njia ZOTE za kujikinga na huu ugonjwa utakuwa ume save more lives???
 

Lipi unaona sijalijibu twende sawa???....mada yako haijalenga lockdown inafanya kazi au haifanyi???? are you serious???..kujadili utekelezaji wake Tanzania bila kuangalia lockdown inafanyaje kazi..?? mnhhh ...

Tanzania sio kisiwa ndugu kilichojitenga na dunia....naona umeamua makusudi kuignore yanayoendelea duniani na kung'ang'ania 'nchi yetu' ...nchi yetu ingekua special mpaka sasa kusingekua na maambukizi ya coronavirus...

Nitapingana na wewe mpaka kufa,sitaki kuona watanzania wenzangu wakifa kama kuku, and yes hujaleta data kwa hiki unacho jaribu kukihubiri hapa zaidi ya speculations zinazobase on 'what if' and yet unataka watu waje na data??!!!??
 
Mkuu huna haja ya kunitukana maana si Mimi niliyekufanya uwe mbangaizaji.siajabu wakati wengine wanaenda shule wewe ulikuwa unatoroka kwenda kufanya biashara uchwara,sasa umeshasahau ujinga ulioufanya unaanza kunyooshea wengine vidole eti ni wabinafsi.corona ikikufyekelea mbali sisi tutakufukia tu ukabangaize huko mbele Kama unadhani kukaa nyumbani ni kwa faida yangu
 
Lol. Data zipi unahitaji dada? Huoni kama huo ni udhaifu mkubwa sana wa hoja iwapo huijui hali ya Tanzania na maisha ya watu kiasi kwamba unahitaji nikupe data?

Pili, kwenye huu uzi mzima hakuna mahali nimtumia "what if". Kinyume chake nimesema hii ndio hali yetu na hali ya lockdown ni hii. Hivyo haitekelezeki. Kama unajadili kwa lengo la kuaddress mkwamo nilioainisha, ulitakiwa uje na data za kuonesha utekelezaji wa lockdown na sio kujadili maana ya lockdown.

Tatu, sasa kwa vile wewe unajua lockdown inafanyaje kazi na mimi sijui, tueleze basi utakavyoitekeleza with the necessary mitigation strategies za madhara ya wazi yatakayojitokeza. Hadi sasa sioni unapojadili hilo.

Wasaidie wasomaji jinsi lockdown inatekelezwa practically Tanzania na utakua umeisidia nchi. Ukifa kwa kupambana nami hutafaidika lolote.

Hizi hoja nyingine za kupambana nami hadi kufa and all that, I'm worried, they are misplaced arguments and I will not go down that line of thinking.

MM Togolani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni kurushiana maneno ya aina hii. Jadilini lockdown na utekelezaji wake. Mutakua mumetoa mchango wa mawazo kwa jamii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna chaguo bora ndugu yangu kati ya haya. Ila maamuzi yanabidi yatazame hatua inayotekelezeka bila madhara makubwa kwenye maisha ya watu unaolusudia kuwalinda.

Pili, hoja ya kwamba kupata maambukizi ya Corona maana yake ni kifo, ni hoja dhaifu sana kuitumika kuhalalisha lockdown. Tafuteni hoja zingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa Kama wenye mifumo bora ya afya wanakufa Kama kuku sisi wenye hospital zisizo na hata panador unategemea nini? Mkuu mwenzako akinyolewa wewe unapaswa kutia maji, hivi huko kujiamini kwenu kunatokana na uwezo mlio nao,kiburi cha uzima na mauti au ujinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…