Serikali isikubali kutangaza “total lockdown” au Karantini. Wanaoishawishi ama hawajui wanachokishauri au ni wabinafsi

Soma bandiko lako kisha usome bandiko nililoandika kufuatia lako, utaelewa tu bila shaka.
Sijaelewa hizo aya zako za chini zina uhusiano gani na post yangu... Ila ngoja nikujibu zile zinazohusiana; lockdown inategemea idadi ya maambukizi ya nchi husika pamoja na kasi ya maambukizi ya hiyo nchi...Totally lockdown sio mkumbo,inaenda na uhalisia.. Wewe unapiga kelele sababu upo bongo,hujui yanayoendelea huko nje... Tembelea forum za hizo nchi zilizo ktk total lockdown ulinganishe na hali hiyo ikiwa tz ndo upate uhalisia.., sio kuleta mambo ya trump,sijui hata kaingiaje hapa.
 

Mkuu si nia yangu kupigishana kelele na wewe.

Kaza uzi hapo hapo jiaminishe uko vizuri. Kwani taabu iko wapi?
 
Nakuunga mkono mkuu. Serikali haijazuia 'personal or family lock down', anayeweza kujifungia ajifungie sisi wengine tuendele na mambo yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawana lolote!! Ukiwasikiliza utadhania wana huruma sana na maskini, kumbe wana yao, ili kuja kufaidika na tabu watakazo kuwa wanapata masikini, wakati wa total lock down!!
 
Nimegundua kuwa wimbi la wasiojua kuandika kwa ufasaha JF limeongezeka sana,yaani wamekuja upesi kama dhoruba!Sijui tatizo ni nini?Hasahasa tatizo hili lipo hasa kwa wale wafa na tai shingoni!
Huyu unayesema hajui kuandika alikuwa Mwandishi wa Hotuba wa Rais Kikwete, akiachiwa kazi hiyo na January Makamba...


So fikiri kabla ya kusema, yawezekana aliyoyaandika yanazidi upeo wa akili zako, Pole sana!

Finally, Linganisha muda MM Togolani aliojiunga JF(2010) na muda wako Wewe, Then uweke hoja zako chini tujadili
 
Mkuu si nia yangu kupigishana kelele na wewe.

Kaza uzi hapo hapo jiaminishe uko vizuri. Kwani taabu iko wapi?
Endelea kupingana na uhalisia...Namba zikipanda unafikir haitakuja? Itakuja tu...Na ndo utaona hicho unachokililia kije kana kwamba ni burudani hivi... Siku njema.
 
Sitetei uwepo wa lockdown... Umenisoma vibaya nadhani.
 

Uko sawa kabisa.

Ila jiulize maswali. Lengo la Lockdown ni kitu gani? Bila shaka utaniambia ni kuzuia maambukizi watu wengi wasiugue na baadhi yao wakafa (maana tunajua sehemu kubwa ya wanaougua wanapona). Sasa ni asilimia ngapi ya watanzania wanaweza kubaki ndani wakiwa hawana chakula wala maji kwa hata wiki moja wakaishi? Itasidia nini kukimbia maambukizi ya Covid-19 halafu watu wakafa na njaa, utapiamlo, na magonjwa mengine kama kipindupindu, malaria na kuhara? Utakua umeokoa nini na kupunguza nini?

Mimi siesemei serikali wala sijasema viongozi wasichukue tahadhari nyingine za kitaalamu wanazopewa. Nimezungumzia jambo moja tu kwamb Lockdown haifai kwa nchi yetu kwa sasa. Inaweza kuwa worse case scenario tutakapoona tumezidiwa na hakuna namna. Wakati huo athari ya kukaa ndani itakua ya muda mfupi na tumejiadhaa nayo. Hata hivyo sio lazima kila nchi ifikie walipo Italy na Spain.

La uandishi nakuachia maana kama ungeona hakuna cha maana usingesoma
 

Uko sawa kwenda dhana ya nature ya ugonjwa. Ila nasita kukubaliana nawe kwamba uwezo wetu wa kufikiri na kufanya maamuzi yanayotufaa unategemea nchi nyingine kama ulizozitaja zimefanya nini.

Ila jiulize maswali. Lengo la Lockdown ni kitu gani? Bila shaka utaniambia ni kuzuia maambukizi watu wengi wasiugue na baadhi yao wakafa (maana tunajua sehemu kubwa ya wanaougua wanapona). Sasa ni asilimia ngapi ya watanzania wanaweza kubaki ndani wakiwa hawana chakula wala maji kwa hata wiki moja wakaishi? Itasidia nini kukimbia maambukizi ya Covid-19 halafu watu wakafa na njaa, utapiamlo, na magonjwa mengine kama kipindupindu, malaria na kuhara? Utakua umeokoa nini na kupunguza nini?

Ok, tuchukulie lockdown ni lazima kwa sasa. Tusaidie kutuambia itachukua muda gani kukaa ndani (maana hatujui kilele cha maambukizi kitafika lini). Tuambie mamilioni ya watanzania wasio na kazi au akiba ya chakula wataishije kwa kukaa ndani. Tuambie wanaotegemea kutembea kms kadhaa wakachote maji, kuni, mkaan nk watayapata wapi.
 
Mkuu naona na wewe umeandika eti? Sawa tusubirie wakati mnalazwa pale kwa mkapa tena chini au kwa magodoro mliyotoka nayo nyumbani ndo akili zitakurudi na kuanzia hapo utaelewa kwamba lockdown ingekuwa na faida zaidi kwako kuliko huu upupu ulio uweka hapa.For your information Mimi na familia yangu tumeshajiweka lockdown wenyewe,hatuna sababu ya kumsubiria Magufuli,but wewe endelea kupiga kazi nikisha maliza kucoronwa utanikopesha hela kwa riba ya asilimia 200
 
Mkuu Kama hujawahi onja sumu au kupita mikumi kwa baskeli basi wewe mwoga tu
 
Wengi wenu humu hata hilo neno "lockdown" mmelisikia hivi majuzi tu!

Sasa hivi kila mtu kawa mjuaji.....
oooh "tunataka lockdown"....

Wagonjwa wenyewe ishirini ambao ni sawa sawa na asilimia sifuri nukta sifuri ya wagonjwa wote wa corona dunia!

Jamani, muwaache wabangaizaji watafute maisha. Msiwaongezee mzigo mwingine wa hiyo corona!

Kila mtu achukue tahadhari binafsi. Ukiona haujatosheka unaweza kujifungia kwenye contena ili corona asikupate!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ndugu Sijijui Tahadhari binafsi ni jambo la msingi sana. Hongera kwa hatua hii nzuri uliyochukua. Ila mimi nilichoongelea ni zaidi ya mimi binafsi au familia yangu. Nimeongelea Tanzania kama nchi na hali za wananchi wake ambazo zinanihusu sana.
 
Ndugu Sijijui Tahadhari binafsi ni jambo la msingi sana. Hongera kwa hatua hii nzuri uliyochukua. Ila mimi nilichoongelea ni zaidi ya mimi binafsi au familia yangu. Nimeongelea Tanzania kama nchi na hali za wananchi wake ambazo zinanihusu sana.
Ungekuwa serious ungeishauri serikali wafanye kitu kuliko kuwambia watu wakafe au wakaambukizane kwa wingi eti kisa wanajitafutia riziki while ukijua mfumo wetu wa afya hauwezi ukawahandle Wala kuwatibu pale hali itakapokuwa imekuwa mbaya.Siku zote kwa watu wenye akili kinga ni bora kuliko tiba.sasa ninyi kwa ujinga wenu singizieni umasikini wa mtanzania,sasa wakishaambukizana kwa maelfu ndo umasikini wao utakuwa umeisha mkuu
 
Utakapokuwa kuwa umelazwa pale taifa bila nesi Wala daktari wa kukuhudumia ndiyo utaelewa lockdown ilikuwa kwa faida yako but for now wanyoshee vidole wengine na aendelea kupiga mzigo kaka? Wewe si mpangaizaji?
 
Si kwamba bongo hatuna maambukizi sema mfumo wetu wa afya ni hoe hae,Jana Kuna familia moja imebebwa huko mbezi msakuzi baada ya baba kuugua corona aliyoambukizwa huko Kongo,je safari nzima na roli lake toka tunduma mpaka amewashushia wangapi hilo zigo.Kama Tanzania haina Mungu wa pekee yake just wait you will see
 
Ukiacha supermarket umejiuliza hapo kahama mna hospital ngapi na manesi wangapi na zinaweza kuhudumia watu wangapi kwa mpigo? Kama US wanachemsha na wanamlaumu Trump kwa kufanya uzembe sisi tutaisha na hii lugha ya umasikini sijui itatoweka na kila mtu atajiweka mwenyewe kwenye lockdown same way mipaka yetu ilivyojifunga
 
Wewe Togolani una uhuni usio na kipimo na uliopitiliza. Ebu peleka use...ge wako huku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…