Serikali isipowapiga marufuku 'Mitume na Manabii' wa mchongo, miaka michache ijayo tutakuwa na Taifa la ovyo sana

Huu ni ukweli familia zinavurugika kwa Mambo haya,watu hawafanyi kazi kwa Mambo haha,watu wanaacha njia za tiba za kisayansi kwa Mambo haya,kuzaliana hivyo kunazidi ota mizizi kwa Mambo haya,umaskini unaongezeka kwa Mambo haya,elimu inaporomoka kwa Mambo haya,japo waaminio na wafanyao kuwa Ndio shambani kwao na ndipo wavunapo watapinga kwa herufi kubwa Ila watakuwa ni waongo na wenye kuhakikisha maslahi yao hayaingiliwi.
 
Kuna uyu namsikiaga kwenye redio sitoitaja usiku..[emoji23][emoji23]yeye huwa anasema tuma pesa (Sadaka) ikiingia tu anakuona paka Ulipo kwanzia ukivozaliwa[emoji23][emoji23]aseee aanaanza kutumia sayansi sasa tatizo nimekaaa siku nnne nasikiliza nakuja kugundua sjui wameweka record ya zile simu..[emoji23][emoji23][emoji23]dadeq kila siku kinajirudia. Ukipiga haumptaji..Alafu anasema mje kanisani watu wanamilestones bhn[emoji23] we kaa kizembe tu
 
Huwezi kusikia shekhe anajiita mtume/nabii wala kusikia kaanzisha msikiti


Lakini hawa wa upande wa 2 ni matatizo kweli kwel
 
Haitasaidia kitu.

Hayo mambo yatapungua mpaka pale watu wengi watakapokuwa vizuri kiuchumi. Tofauti na hapo wataendelea kwenda tu. Kumbuka wengi ni masikini na wanaahidiwa miujiza + pesa
Na hivyo ndivyo taifa linageuka kuwa taifa la miujiza kila kitu kinasubiri miujiza ili kitokee,ili kifanyike🥱
 
Aanze kupiga marufuku misikiti kwanza!
 
Walio na afya hawahitaji tabibu!
 
Jihadharini na watu wanaotumia jina la yesu kujipatia kipato.
 
Inasikitisha sana kuona mtu anatumia mwanya wa shida za mtu mwingine ili kujinufaisha. Dunia ya leo wenye matatizo tupo wengi, na utakuta mtu amezunguka mahala pengi, na ametumia gharama kubwa, lakini hakufanikiwa.

Ikifikia hapo, ndipo huamua kujaribu mahala popote ambapo atasikia/ataambiwa anaweza kupata suluhisho la tatizo lake. Huwezi kumlaumu mtu kama huyu, kwakuwa anatafuta suluhisho la tatizo lake. Na kuna msemo tunasema "mfa maji hakosi kutapatapa".

Wa kuwalaumu ni hawa ambao wanajuwa kabisa wanachokifanya ni utapeli. Mtu unamwona mwenzio ana matatizo, na ametumia gharama kubwa lakini hakufanikiwa, na wewe tena unachukua kile kidogo kilichobakia. Hivi hamna huruma?!

Kama una nia ya kumsaidia, si umsaidie bure. Mbona Yesu (na mitume wengine) aliwaponya watu bure? Kama karama ya uponyaji unayo, si ulipewa bure na Mungu? Ninyi manabii wa mchongo, Mungu anawaona!
 
Du! Hawa jamaa ni matapeli wakubwa sana. Kama huyu hapa mngefanya mpango akamatwe na TAKUKURU akaozee ndani; ni watu wabaya sana katika jamii.
 
Nina shemeji yangu mmoja alikuwa anasali kwa Mzee wa Upako. Baadaye alhamia kwa Apostle Mtalemwa. Sasa hivi amehamia kwa Bulldozer Mwamposa. Na Mwaposa akishuka umaarufu atahamia labda kwa Masanja Mkandamizaji.

Hawa akina mama tuwaombee tu kwa Mungu awape ufahamu. Wanateseka sana.
 
Wajinga hawaishi wanazaliwa kila siku. Sio kazi ya Rais kuingilia uhuru wa watu
 
Wajinga hawaishi wanazaliwa kila siku. Sio kazi ya Rais kuingilia uhuru wa watu
Mkuu sisemi kwamba Rais aingilie dini lakini nashauri aweke utaratibu mzuri ili kuwasaidia wapigakura wake wasipotoshwe. Kumbuka 2025 sio mbali. Ikiwa hawa wananchi wataangamizwa kiuchumi ni yeye ndiye atakayelaumiwa kuharibu uchumi wakati uchumi unaharibiwa na wachumiatumbo wachache kwa smalahi yao binafsi.
 

You're overthinking mkuu.

Kuzuia manabii na waganga wote hakuwezi kukuza uchumi. Nchi ina uchumi mbovu sababu haina mazingira rafiki ya uwekezaji, haina viwanda, haina vyanzo vipya vya kodi nk. Manabii are the last on the list if they make it at all.
 
Huwezi kusikia shekhe anajiita mtume/nabii wala kusikia kaanzisha msikiti


Lakini hawa wa upande wa 2 ni matatizo kweli kwel
Ulitaka wafanane..kila imani na utaratibu wake..huko ukijiita mtume kichwa chako halali yao vitukuu vya mtume.

Acha wakristo wafurahie uhuru wao mana hata kristo aliwaambia wakiwa na imani wanaweza fanya zaidi ya miujiza aliyoifanya.

Get a job.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mbona wanaombewa bure..na hakuna mtu anayeshikiriwa bunduki atoe sadaka.

Huko mahospitalini kwa waganga mbona mnatoa hela na hamlalalamiki.

Sikuhizi jf ina watu ambao wanaupeo mdogo wa kufikiri nakuhoji.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hujawahi pata na matatizo unadhani wanapenda kuzunguka makanisani kutwa kuchwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hakuna utaratibu mzuri zaidi ya serikali kuimalisha uchumi wa wanachi wake..kuwaelimisha zaidi na kuwa na huduma bora za ustawi wa jamik..haya mambo mbona ulaya yalikuwepo na yaliisha yenyewe baada ya serikali kuwekeza kwenye vitu nilivyokutajia.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…