Serikali isipowapiga marufuku 'Mitume na Manabii' wa mchongo, miaka michache ijayo tutakuwa na Taifa la ovyo sana

Hili tatizo mimi binafsi sioni utofauti wake na tatizo la Betting ndani ya nchi.
Matatizo makubwa yanayolinyemelea nchi ni betting na mitume na manabii wa uongo. Pia harusi na sherehe zimekuwa nyingi na zinatia watu unasikini mkubwa. Tuombe sana kwa Mola wetu atupatie maarifa kutoka juu.
 
Ni kweli. Mama awaache tu. Sema wangekuwa wanalipa kodi walau.
 
Ushuhuda mzuri mkuu. Ubarikiwe sana. Sisi wote tunaowajibu kusaidia jamii kujitambua na kuondokana na haya majanga. Watanzania tunakabiliwa na unasikini kwa kujitakia wenyewe. Kuibiwa kila kona, betting, waganga wa kienyeji, manabii wa uongo na sasa kuna janga kubwa linashamiri, harusi na sherehe. Hili nalo ni janga. Kwa hapa hata mimi ni mjinga na najaribu kujiokoa. Kwa mwezi utakuta unachangia zaidi ya laki tano na zaidi. Kwanza ni kujitoa kwenye kamati. Kupunguza madau. Kuna siku nilipiga michango niliyotoa ya arusi kwa mwaka ilikuwa zaidi ya milioni. Sasa kwa kipato gani? Huku unasomesha, misiba, kipa imara na mibarikio. Kenya wao wamejikomboa na haya majanga. Unatakiwa kuchangia kwa kiwango sawa na uwezo wako. Japo kwa kuweka mambo sawa ujiandae kuitwa bahili, roho mbaya, ngoja na yeye ataozesha nk. Hata Yesu wetu hakuleta amani bali upanga. Kutekeleza mambo hayo yote ya kijamii unajikuta kwenye mgogoro mkubwa wa madeni na kuchanganyikiwa. Wakenya wakichangiana ni misiba na harambee ya kupeleka vijana wao kusoma ng'ambo. Hata hivyo kwa shida ambazo tutapitia tutajifunza. Muda ni mwalimu mzuri sana.
 
Mbona wanaombewa bure..na hakuna mtu anayeshikiriwa bunduki atoe sadaka.

Huko mahospitalini kwa waganga mbona mnatoa hela na hamlalalamiki.

Sikuhizi jf ina watu ambao wanaupeo mdogo wa kufikiri nakuhoji.

#MaendeleoHayanaChama
Du mtumishi naona umeguswa. Unatetea sana hoja.
 
Yaani ni burudani hasa
 
Mkuu umeongea ukweli sana. Kenya hakunaga ujinga kama huu. Kipindi nasoma Homa Bay High School wananchi walikuwa tukichangiana karo za wanafunzi kupitia harambee. Tangu nihamie Tanzania sijawahi kuona watu wakichangiana kwenye masuala muhimu kama elimu na matukio mengine ya maana zaidi ya misiba na harusi.
 
Ule ni utapeli. Sala inasomwa Mara moja, ukiisoma Mara Saba inakuwa kitu kingine au fasion ya kujitambulisha. Ni Kama uimbe wimbo wa taifa Mara Saba for what purpose.
Hata mimi huwa nawashangaa sana waumini wake kwa jinsi wanavyopelekwa kama makondoo bila kujitambua. Na wakimaliza kusoma mara saba wanaongezea na maneno mengine tena. Huyu jamaa mm namuona kama mpigaji tu hana jipya wala la zamani. Wakati wote utamsikia anawaombea watu wapate pesa, watoto, magari na mali nyingine za kidunia. Sijawahi kumsikia akihubiri kuhusu uzima wa milele.
 
Mkuu umeongea jambo zuri sana. Natamani wana JF wote wangepitia hili andiko lako hata ikibidi kuandika nyuzi watu wengi zaidi wasome CC Mshana Jr
 
Okay, but kuiga siyo dhambi maana Serikali zipo zinazofanya hivyo haswa huko UTUME na UNABII ulipoanzia hapa Afrika..

View attachment 2545822
Serikali zinazojitambua haziachi wananchi wake waangamizwe na manabii wa mchongo bali wanachukua hatua kuwalinda wananchi bila kusita. Hapa Tanzania wanaangalia kura zaidi. Hata wananchi wakiangamia hawajali.
 
Wanabii kama hawa sio wa kuchekea hata kidogo. Serikali isipowashughulikia itabidi wananchi tujichukulie sheria mkononi.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…