Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Kuna hii tabia ya watumishi walioajiriwa na serikali kukaa kwenye ajira kwa miaka kadhaa halafu wanaandika barua kwenda masomoni kujiendeleza au wengine wanabadili fani kabisa ,kama alikuwa mwalimu anabadili fani kwenda fani nyingine ambayo kwake ataona inamfaa.
Sasa ubaya wa hili jambo ni pale serikali inapoendelea kumlipa mshahara huyu mtumishi hali ya kuwa kipindi hicho hakuna kitu anachokifanya kuliingizia taifa faida bali ni kwa manufaa yake binafsi.
Mbaya zaidi kipindi anakwenda masomoni nafasi yake bado inahesabika na hivyo kuwazibia nafasi waombaji wengine.
Sasa hili jambo kiukweli liondolewe , kama mtumishi atataka kwenda kusoma tena basi asilipwe chochote na ikiwezekana baada ya kuhitimu aombe upya kazi kulingana na elimu atakayokuwa nayo kipindi hicho.
Maana anaweza akaenda kweli kusoma na kumaliza lakini asiwe competent vilevile kulinganisha na wenzake aliomaliza nao ila kwa kuwa yeye tayari nafasi yake ipo basi kwake inakuwa mtelezo.
Tubadirike , serikali iache kuingia hasara kuwalipa hawa watu na kuwahalikishia ajira , kama wameamua kurudi tena kusoma basi iwe for their own risk ,wajilipie wenyewe na waombe upya kazi.
Mbaya zaidi huyu mtumishi mliyemsomesha huko mbeleni anaweza akaacha kazi kwenda sehemu nyingine au nchi nyingine atakayoona kwake ina manufaa ,hivyo hasara inabaki kwa serikali maana hizo pesa walizompa sio mkopo kusema watamdai.