Mkuu kwa barabara zetu za one way ajali nyingi ni head to head, gari kugongwa nyuma, gari kugonga nyuma, gari kuacha njia,kufeli brake.
Kwa ajali ya moto tunaweza zuia au kupunguza kwa kutumia technology. Bus nyingi za kichina saizi zinakuja na system ya kuzima moto kwenye engine bay ambapo wameweka mtungi unaozima moto wa ghafla.
Saizi kuna technology ya mpira wa Elide Ball fire extinguisher moto ukitokea yenyewe inazima bila amri ya mtu yeyote na ufanisi wake ni mkubwa sana. Kwenye basi la abiria iwekwe sheria angalau ziwekwe kwenye kila buti la mzigo,tank la mafuta, eneo la abiria.Minimum iwe 6 elide ball fire extinguisher na saizi Tanzania Kuna kampuni Ya Africable wanazalisha hizi fire extinguisher.
ELIDE FIRE EXTINGUISHER ni teknologia ya kisasa ya kuzima moto bila kuleta athari yoyote kwenye mazingira na watu.
HISTORIA YA ELIDE FIRE EXTINGUISHER
Hii teknologia iligunduliwa mwaka 1997 na raia Thailand aliyeitwa Phanawatnan Kaimart katika mji wa BANGKOK, Thailand.
Baada ya kunusurika kifo katika ajali ya moto iliyotokea katika Hotel ya Royal Jomtien Resort Hotel iliyopo mji wa Pattaya mwaka 1997 ambapo inakadiriwa watu wiapatao 100 walipoteza maisha.
Alivumbua huu mpira wa kuzima moto baada ya kuona maafa ya moto na idadio kubwa ya watu waliopoteza maisha baada ya mitungi na njia...
Kwa mabasi makubwa ya abiria mengi yananunuliwa mapya Latra waweke vigezo vya chini gari kupewa leseni ya masafa na kubeba abiria wengi.
Unapo ingiza gari ya abiria lazima iwe na technology ambazo zinasaidia usalama wa gari,abiria na Watumiaji wengine wa barabara.
Kila basi liwe na mfumo wa Advanced Driving Assistance System (ADAS) kwa yale yanayofanya safari ndefu. Hizi package za technology ukiweka kama minimum requirement kwa gari kuingia wachina wanaweka kama basic au standard features maana wao wanaenda na soko linataka nini. Na kwenye mabasi mnunuzi una option ya kipi uwekewe.
Hii system ya ADAS ina kuwa na camera pande za gari na sensor inamsaidia dereva kupata alarm ya tahadhari anapotaka kugonga au kugongwa akishindwa kusimama basi gari itasimama yenyewe.
YUWEI's Bus Collision Avoidance System enhances safety with ADAS, fatigue monitoring, and blind-spot alerts, helping reduce accidents for buses and coaches.
en.yuweitek.com