Serikali isiwalipe posho waliokuwa wakimsafirisha kwa gari mtoto mahututi toka Kigoma kwenda Dar es Salaam


Nadhani watu wengi hatuelewi hali halisi, sina uhakika kama katika utendaji wa wahudumu wa afya kuna kipande kinazungumzia ukiwa na special case furani unaweza kuomba ndege au helcopter as a policy (utaratibu ni huu). Tukiwa nje tunawaza vyema kweli kweli.

Mtu ambaye unataka afikirie ndege, anajua hata town trip zilivyo ngumu kutekelezeka/ataonewa tu. Ingawa ndo ulitakiwa kuwa uhalisia.

Huwezi kufikiria kisichokuwepo, ingawa katika hali halisi ndivyo ilitakiwa kuwa (kupata usafiri wa ndege/helcopter). Ndo maana huwa unasiki: Rais katoa ndege, familia imetoa ndege, jeshi limetoa ndege na au wizara ya afya inamshukuru X ametoa ndege. Sina uhakika kwa Wizara ya Afya kutoa ndege.

Kama hatujui kuwa wakati mwingine wagonjwa wenye rufaa huweza kusubirishwa ili wawe wengi na kupunguza idadi ya trip ndani ya mkoa, basi tuko mbali na ufahamu halisi. Kama unayafahamu, basi hata hao wamejitahidi kuweza kuji-ogarnize na safari kuanza. Ingawa hatujui hitaji la msingi la mgonjwa.

Kuna wagonjwa kupewa rufaa toka Kigoma kwenda Mwanza/Bugando na bado ndugu unaambiwa tunahitaji hela ya mafuta, sembuse hata aliyepewa gari?

Tunajua uimarishaji wa mifumo ya afya inaenda zonal wise na kwa kuiweka karibu na watu wengi, mtu kaamka kaenda kuweka hospitali kubwa kule pembeni tunashangilia tu.

NB: Kwa ground ni kugumu kwelikweli acheni mchezo au masihara.
 
Kwa hiyo unaona ilikuwa ni sahihi kabisa kumsafirisha hiyo mtoto kutoka Kigoma mpaka Muhimbili kwa ambulance!

Hospitali za rufaa na zile za Kanda kazi yake nini? Si wangeweza hata kupata suluhu ya muda kabla ya kufika huko Muhimbili? Angekuwa ni mtoto wa mkubwa angesafirishwa kwa usafiri huo?

Ngoja siku ufiwe na mtu wako wa karibu kwa uzembe wa kibinadamu wa hao madaktari, ndipo utakuja kuona umuhimu wa hao watu kuwa makini muda wote, na pia kujiepusha na makosa ya kizembe kama haya.
 
Bugando ni karibu kama uamuzi ulikuwa ni kutumia Abulance ya Gari.
Inategemea kama shida ya msingi ingeweza kupatiwa ufumbuzi pale Bugando. Wakati mwingine watu hupiga simu na kushauriana kuwa kwa hali ya mgonjwa ni vyema aende kituo X au Y.
 
Shida hujui kilicho wapata mpaka kuchukua maamuzi hayo mkuu
 
Hakuna mwenye uhakika kama walifanya consultation kwenye hospitali za kanda. Na unaweza kufanya ukaambiwa kwa hali ya huyo mgonjwa hatafaidika na huduma hapa. Mtaalamu yupo lakini vifaa hakuna au mtaalamu hayupo.

Hii ni issue ya kuwasikiliza wahusika kwenye level halisi ya tatizo ndo uwahukumu. Kesho unaweza kuwasikiliza ukawaita mashujaa walivyopambana na mazingira magumu.

Unaweza kumuita mtu mzembe kumbe hata hela ya mafuta watu wamechangishana au palepale kungeweza kutolewa huduma ila walikosa mtaalamu au vitendea kazi au vyote.

Kuna mtu unamuita mzembe sasa hivi anatokwa machozi kwa alivyojitoa mpaka lilipofikia. Tusihukumu mapema sana. Sisi wa pembeni tu wenye kujua mengi, lakini wao watendaji wanajua mengi zaidi.
 
Inategemea kama shida ya msingi ingeweza kupatiwa ufumbuzi pale Bugando. Wakati mwingine watu hupiga simu na kushauriana kuwa kwa hali ya mgonjwa ni vyema aende kituo X au Y.
Bugando kuna Wataalam wangemfanyia kazi halafu ndio wangeamua.
 
Bugando kuna Wataalam wangemfanyia kazi halafu ndio wangeamua.
Inategemea tatizo la msingi, Bugando nao hupeleka wagonjwa Muhimbili kwa sababu mbalimbali.

Kulingana na hali ya mgonjwa unaweza kupiga simu ukaelezea mgonjwa alivyo na kupewa jibu.
Tunaweza vs hatuwezi au sehemu husika imejaa ambayo angeweza kulazwa.

Yote ni yote ni mpaka uwasikilize ndo utoe hukumu inayoendana na hali halisi kulingana na mazingira na hatua waliochukua.

NB: Kuna watoa huduma wanabeba trauma/magumu physically vs psychological kutokana na mazingira magumu ya kazi, tusiwatweze kirahisi hivyo tuwape nafasi pamoja na serikali kujenga mazingira rafiki ya kazi. Ingawa wazembe wapo kwa kiasi chao pia.
 
Hiyo ndege ya kukodi Nani angelipa mkuu? Au wewe umefika Jana hapa nchini ikitokea ugaibuni? Hiyo kitete hospital, inaizidi hadhi Maweni? Hujui zote Ni hospital za Rufaa za mikoa? Haya pale Benjamin mkapa, unadhani wanatibu bure? Ile hospital mkuu Kama hujui siyo ya makabwela. VIP tu vinaendda Hadi laki tatu na zaidi, unadhani Ni mchezo. Sis makabwela tukikosa matibabu huku tunakimbilia Muhimbili tu sio Benjamin's.
 
Angekuwa wa familia fulani,mtoto wa mtu maarufu...angepelekwa kwa ndege na kupata michango ya kutaka sifa watu
Ila kwa sababu mtoto hyo katokea familia ya kawaida/chini watu hawana habari

Ova
Acha tu aisee.

Kuna watu ambao ni muhimu,na ambao si chochote.

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Bugando kuna Wataalam wangemfanyia kazi halafu ndio wangeamua.
Kwa upande wangu sidhani kama madaktari wa maweni hawakuwasiliana na wenzao wa Bungando. Kuona kama huyo mtoto angebenefit kitu kupelekwa bugando.

Naamini hadi wanaamua kumpeleka National hospital waliona hakuna namna.
Pengine daktari bingwa wa mfumo wa fahamu aliebobea kwa watoto anapatikana Muhimbili pekee.

Ishu nyingine ni hiyo ya njia ya usafiri, pengine waliona process za kufuatilia ndege zingechelewa. Sote tunajua urasimu uliopo nnchini.

Sisi ni rahisi sana kulaumu kwasababu, hutukuhusika.
Tunaweza kuwalaumu wote, ila kuanzia mganga mkuu wa hospitali, madaktari , wauguzi, na madereva hawa watu si wa kuwalaumu.
 
Inasikitisha sana.
Mtoto alikuwa kwenye hali tete kiasi hicho angewezaje kumudu mikikimikii ua rough road hatimaye safari ndefu ya Kigoma to Dar?
Mimi sio daktari lakini hawa walilenga kulipana posho za safari vinginevyo wangetumia ndege kuokoa uhai.
 
Sawa hata majuzi tukiwa tunanyanduana na Wife kuna mama mjamzito alijifungulia katika geti la hospitali wauguzi wakiwa ndani na waligoma kufungua geti mpaka mtoto akafa... yaani waligoma kufungua hata alipokuja mwwnyekiti wa mtaa, ocd mpaka mkuu wa wilaya.. hilo unalizungumziaje mkuu?
 
Naamini hadi wanaamua kumpeleka National hospital waliona hakuna namna.
Pengine daktari bingwa wa mfumo wa fahamu aliebobea kwa watoto anapatikana Muhimbili pekee.
Sote nadhani tunayajua Majeraha ya Panga lililonolewa vizuri kwa lengo la kusababisha Maximum Demage kwenye mwili wa Mtoto 😥
 
Ni wakati sasa atcl kuwa na air ambulance
 
Angekuwa wa familia fulani,mtoto wa mtu maarufu...angepelekwa kwa ndege na kupata michango ya kutaka sifa watu
Ila kwa sababu mtoto hyo katokea familia ya kawaida/chini watu hawana habari

Ova
Kigwangala almgonga twiga wetu, akapelekewa chopper fasta,
Usipojulikana huna hudhaminiwi mkuu
 
Nisingeweza kiwalaumu wasiokuwa na maamuzi ya juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…