Lukonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 1,469
- 2,086
Uongozi wa mkoa na hospitali ya Maweni ulishindwa kutumia akili kabla ya kuamua mtoto aliye mahututi asafirishwe kwa gari toka Kigoma mpaka Dar es Salaam kwa ajili ya tiba iliyowashinda, walishindwa kupata ndege ya Flying Doctor au kumpeleka Mwanza!
Walizipita hospitali za Kitete Tabora, Mkapa Morogoro na wakawa na nia ya kuipita ya Morogoro na mtoto akawafia njiani mkoani Morogoro! Hiki kitendo ni cha kijinga sana.
Nadhani watu wengi hatuelewi hali halisi, sina uhakika kama katika utendaji wa wahudumu wa afya kuna kipande kinazungumzia ukiwa na special case furani unaweza kuomba ndege au helcopter as a policy (utaratibu ni huu). Tukiwa nje tunawaza vyema kweli kweli.
Mtu ambaye unataka afikirie ndege, anajua hata town trip zilivyo ngumu kutekelezeka/ataonewa tu. Ingawa ndo ulitakiwa kuwa uhalisia.
Huwezi kufikiria kisichokuwepo, ingawa katika hali halisi ndivyo ilitakiwa kuwa (kupata usafiri wa ndege/helcopter). Ndo maana huwa unasiki: Rais katoa ndege, familia imetoa ndege, jeshi limetoa ndege na au wizara ya afya inamshukuru X ametoa ndege. Sina uhakika kwa Wizara ya Afya kutoa ndege.
Kama hatujui kuwa wakati mwingine wagonjwa wenye rufaa huweza kusubirishwa ili wawe wengi na kupunguza idadi ya trip ndani ya mkoa, basi tuko mbali na ufahamu halisi. Kama unayafahamu, basi hata hao wamejitahidi kuweza kuji-ogarnize na safari kuanza. Ingawa hatujui hitaji la msingi la mgonjwa.
Kuna wagonjwa kupewa rufaa toka Kigoma kwenda Mwanza/Bugando na bado ndugu unaambiwa tunahitaji hela ya mafuta, sembuse hata aliyepewa gari?
Tunajua uimarishaji wa mifumo ya afya inaenda zonal wise na kwa kuiweka karibu na watu wengi, mtu kaamka kaenda kuweka hospitali kubwa kule pembeni tunashangilia tu.
NB: Kwa ground ni kugumu kwelikweli acheni mchezo au masihara.