Serikali isiwalipe posho waliokuwa wakimsafirisha kwa gari mtoto mahututi toka Kigoma kwenda Dar es Salaam

Serikali isiwalipe posho waliokuwa wakimsafirisha kwa gari mtoto mahututi toka Kigoma kwenda Dar es Salaam

Sawa hata majuzi tukiwa tunanyanduana na Wife kuna mama mjamzito alijifungulia katika geti la hospitali wauguzi wakiwa ndani na waligoma kufungua geti mpaka mtoto akafa... yaani waligoma kufungua hata alipokuja mwwnyekiti wa mtaa, ocd mpaka mkuu wa wilaya.. hilo unalizungumziaje mkuu?
Kwahiyo wewe na mkeo mlikuwa mnanyanduana hospitali! JF kuna membazi wa hovyo sana.
 
Uongozi wa mkoa na hospitali ya Maweni ulishindwa kutumia akili kabla ya kuamua mtoto aliye mahututi asafirishwe kwa gari toka Kigoma mpaka Dar es Salaam kwa ajili ya tiba iliyowashinda, walishindwa kupata ndege ya Flying Doctor au kumpeleka Mwanza!

Walizipita hospitali za Kitete Tabora, Mkapa Morogoro na wakawa na nia ya kuipita ya Morogoro na mtoto akawafia njiani mkoani Morogoro! Hiki kitendo ni cha kijinga sana.

Watu hawa zero kabisa
 
Mwandishi unadhani hiyo Per Diem ni kiasi gani yenye thamani ya kuhatarisha maisha kwenye ambulance Kigoma to Dar?
 
Niliulize tu na wangemfikisha na akapata matibabu huu upuuzi ungeuzungumza?

Hawa watumishi mnao wazungusha mitaani na Diem zao mnaamua mzitoe au msizitoe huwa mnawaza wanayokumbana nayo?

Very sad... Hii nchi Dah ukakasi
 
Hivi kitengo cha Trauma cha Bugando kinaweza kukataa kweli?
Huwezi kukaa trauma section muda wote, rejea shida ya mgonjwa ni nini?
Na nafasi ipo kwa mgonjwa husika kulingana na hali yake?

Unakumbuka wagonjwa waliozidiwa wa COVID 19 walikuwa wanakataliwa kwenye hospitali? Unaambiwa kwa mgonjwa huyu atahitaji ventilator au mlete lakini akihitaji ventilator zimejaa.

Hivyo, mlete at your own risk na usaini kuwa tumekueleza. Mambo ya uwezo wa hospitali kukaa na wagonjwa wa hali fulani kwa idadi fulani/capacity inaweza kuwa juu pia. Anything can happen.
 
Ukisema wasilipwe Posho sana sana hapo unazungumzia Dokta na Escorting nurse ambao kwa kifupi hawana hatia wao wamefwata order, pia hatuwezi mlaumu sana Dr aliyetoa Rufaa nahisi aliona mgonjwa atabenefit zaidi Muhimbili kwani pale kuna madaktari Bingwa esp Neurologists sijajua kwa Bugando.

Changamoto imekuja kwenye means ya Transport sijajua logistics zilikaaje

Ila pia tunapata somo leo limetokea hili tumejua wengi je yanatokea mangapi hatuyajua wagonjwa wangapi wanafariki kwa dizaini hiyo, basi ni vema nchi ikaimarisha huduma za Afya nchini.

Hosp za Kanda ziboreshwe kwa kila kitu kwenda Muhimbili iwe ziada.

Tupeleke vijana wetu wakapige shule nje waje na exposure za kutosha
 
It's so sad, maisha ndani ya nchi yetu kama hujulikani your nothing, u just a number, huyu angekuwamtoto wa waziri au general fulani ingetumwa ndege kumsafirisha, wenzetu wamefanyeje sisi mbona ni shida, unaendesha kwenye freeways zao pembeni unakutana na ambulances zimepaki zinasubiria emergency, air ambulances nazo zinasubiria emergencies, looo kwa barabara kutoka kigoma hadi dar!
 
Taifa letu linawasomi wavyeti, Kwa akilibya kawaida ata mwendawazimu hawezi fanya huu ujinga
 
Nilikuwa nasoma comment nione kama kunaatakae jali hata mmoja. Mods naombeni radhi kwa comment hii
1. Kuhusu kwenda Mwanza Bugando au Mkapa Dodoma nadhani Dokta alipima kulingana na hali ya mtoto na alijua alicho kifanya, usimuone zuzu kabisa.
2. Wakati wewe unamnyandua mke wako huko madaktari na manesi wamepambana kufa kupona kumsafirisha mtoto huyu aliyekatwa na mapanga vibaya. I know haikuwa safari rahisi kama ulivyokaa kwenye keyboard unatype... safari ya uchungu mwendo wa kasi kufa na kupona kuokoa maisha ya mtoto akafariki saa 1 kabla ya kufika muhimbili.
3. Watumishi hawa chini wanafanya kazi kama punda... mateso makali... wewe sijui ndio nyie wa wizarani huko mnao toaga maagizo kama MCD...
4. Binafsi nimewaza ipo umuhimu kuimalisha hospitali za kanda na mikoa. Kuliko kushikilia huo mzero iq harafu unaandika comment za kuwatukana punda wenzetu hao.
5. Chukueni posho... posho ya damu na uchungu japo najua hata hamtaweza kununulia kilo ya nyama kwa kumbukumbu ngumu ya usiku wa Giza la mauti
Kwan nini Kazi ya kodi zetu mbona wao yakiwapata ufuatwa na chopa
 
Emergency kilometa zaidi ya elf 1 are we crazy.
Kwann tusiboreshe hospital za mikoa. RIP mtoto ukuzaliwa kwenye familia ya walamba asali usingefia njiani.
 
Hili tukio ni mfano tosha kuwa awamu hii maskini hawana chao.

Sijui mnataka muambiwe nini ili muelewe??
 
Ndio utajua tulivyo wabinafsi.
Hao waliomsafirisha yawezakawa walitoa ushauri mkubwa tu juu ya jambo husika ila bila kujali watu wakajipangia cha kufanya.

Wewe ingia kwa Cruiser..huyo atafika tu kwa mipango ya Mungu Muhimbili.

Siwezi kuwalaumu hao waliokuwa kwa Ambulance kumsafirisha.

Nani alihusika kutoa maamuzi ya kubahatisha kiasi hicho?
Kwa muda waliotumia hao ,je nini kilishindikana kwenda Bugando na kama lengo lilikuwa uhai.Hao Madaktari Bingwa walishindwa kusafirishwa kwa dhararua kuokoa uhai wa Mtoto?

Ubinafsi na mawazo mgando kwa baadhi ya watu wenye nyazifa huko kwenye maamuzi.

Waliohusika kufanya maamuzi wana la kujibu mioyoni mwao.
Msishangae huyo sio wa kwanza na kwa hali hilivyo hatokuwa wa mwisho, nchi ya ajabh sana hii.
 
Kitete inatofauti gani na Maweni?

Hali ikiwa tete pale Kitete, mgonjwa hupelekwa Nkinga Hospital ipo wilaya ya Igunga.
 
Wabongo kwa kulalamika mpo vizuri mno. Ukute na wao walilazimishwa kuchukua maamuzi hayo ili kumuweka mtoto karibu na wanasiasa akipata nafuu waanze kupongezana pale muhimbili
 
Wakulaumu ni dakitari alio towa kibali cha rufaa, baada ya kujua hali ya mgonjwa kumrifa dar es salaam muhimbili hopeless
Madakatari wenu wa miaka hii ni wapumbavu,harafu wakiswekwa Ndani utasikia mpuuzi mmja anasema siasa inaingilia taaluma..

Watu WA hivyo kama Hawa wanalipwa salary kwa Kazi gani hasa?

Mwisho , serikali imalisheni huduma za kibingwa bobezi kwenye hospital za Kanda ,hii biashara ya kila kitu Dar ikomeshwe.
 
Back
Top Bottom