Serikali isiwazuie Lissu na Hamad kufanya Maandamano

Serikali isiwazuie Lissu na Hamad kufanya Maandamano

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
18,069
Reaction score
25,172
Mimi nadhani itakuwa ni busara kwa Serikali kuwaachia Lissu na Hamad kufanya maandamano yao, tena iwape ulinzi mzuri na thabiti kusudi maandamano hayo yasiharibu mali za watu wengine.

Ikiwezekana maandamano yote yarekodiwe tangu mwanzo hadi mwisho; yakiisha bila kuingilia uhuru na haki za raia wengine basi vizuri, na yakitaka kuingilia uhuru na haki za raia wengine ndipo yadhibitiwe na kuwa na ushahidi wa video kuonyesha kuwa yalivunja Sheria.

Maandamano hayo yanaweza kusaidia kuwaondolea frustration za kushindwa uchaguzi na kuanza kujipanga upya kisiasa.
 
Kuna vijana wametangaza kubeba vidumu vya petrol kwenda navyo kwenye hayo maandamano.

Maandamano yanataka yasiwe na kikomo, yafanyike kila kata nchini.

Hakuna nchi duniani inayoweza kuruhusu maandamano ya hivyo. Hata kule Marekani walitumia Jeshi kudhibiti maandamano yasiyo na kikomo.

Vilevile, hawajafanya jitihada zozote za kuaddress matakwa yao. Kwa mfano, wagombea ubunge na udiwani wanaweza kufungua kesi. Wakapeleka ushahidi kama wanao. Mgombea Urais anaweza kutafuta dialogue na upande wa pili kupitia wasuluhishi mbalimbali.

Maandamano bila kikomo nchi nzima ni uhaini. Ni wajibu wa jeshi la wananchi pia kudhibiti uhaini.
 
Kuna vijana wametangaza kubeba vidumu vya petrol kwenda navyo kwenye hayo maandamano.

Maandamano yanataka yasiwe na kikomo, yafanyike kila kata nchini...
Waambiwe ukweli wazi kuwa wakifanya uharibufu wowote watakumbana na mkono wa dola. Halafu wapewe uhuru wa kuandamana huku wakithibitiwa kuzuia uharibifu.

Ninajua hata hapa JF kuna watu huchukia sana miradi hiyo na wangetaka ibomolewe ndipo wafurahi! Lakini bado ningependa waruhusiwe maandamano haya kwa uasimamizi mzuri wa polisi, kama ambavyo polisi walikuwa wakimsimamia Lissu wakati wa kampeini zake.
 
Tunaanzia wapi kuandamana na tunaishia wapi?!

Au tunazurura tu hovyo hovyo?!

Tupewe uelekeo na message ni ipi ili tuifikishe kwa muhusika.

Tunaenda Ikulu ya Magogoni au ofisi za tume Dodoma?!
 
Tunaanzia wapi kuandamana na tunaishia wapi?!

Au tunazurura tu hovyo hovyo?!

Tupewe uelekeo na message ni ipi ili tuifikishe kwa muhusika.

Tunaenda ikulu ya magogoni au ofisi za tume Dodoma?!
Ni kweli, maelekezo ya maandamano yako fuzzy kweli; inaonekama kama vile hayana lengo bali kuleta vurugu tu.
 
Swala sio kuzuiwa, wanatakiwa waombe kibali na wafuate sheria zilizopo.
 
...nachukulia kuwa wameomba kibali kwa mujibu wa sheria.
Hawakuomba mkuu, hapo ndio kwenye tatizo, kwa sababu wao wanataka maandamano yasiyo na ukomo. Vile vile hawataki hayo maandamano wafanyie kwenye majimbo yao walioshindwa bali bandari salama.
 
Waambiwe ukweli wazi kuwa wakifanya uharibufu wowote watakumbana na mkono wa dola. Halafu wapewe uhuru wa kuandamana huku wakithibitiwa kuzuia uharibifu. Ninajua hata hapa JF kuna watu huchukia sana miradi hiyo na wangetaka ibomolewe ndipo wafurahi! Lakini bado ningependa waruhusiwe maandamano haya kwa uasimamizi mzuri wa polisi, kama ambavyo polisi walikuwa wakimsimamia Lissu wakati wa kampeini zake.
Nakubaliana na wewe. Katika kufanikisha hili, ilibidi wanaotaka kuandamana kuonyesha ishara ya amani. Changamoto ni lugha wanazotumia. Halafu wamekuwa wakitumia lugha hizohizo kabla hata uchaguzi haujafanyika. Kwahiyo inaonyesha ishara kuwa walijiandaa na shari.
Maandamano ya amani sio kitu kigeni Tanzania.
 
Hakuna nchi duniani inayoweza kuruhu chaos kwa kisingizio cha maandamano.

Prevention is better than cure...
 

Attachments

  • Screenshot_20201101-231759_Facebook.jpg
    Screenshot_20201101-231759_Facebook.jpg
    129.4 KB · Views: 14
Ni kweli, maelekezo ya maandamano yako fuzzy kweli; inaonekama kama vile hayana lengo bali kuleta vurugu tu.
Hahaha mnaogopa bure, Tanzania hii maandamano yanatofauti gani na siku zingine.

Watembea kwa miguu nchi hii ni wengi ukilinganisha na idadi ya wenye magari.

Binafsi hayo ni matembezi ya amani tu, kama inavyokuwa siku zote.

Msije mkawapiga watembea kwa mguu mkadhani ni waandamanaji.

Maana polisi huko leo wanavutishwa bangi, wakitoka huko watapiga hadi vivuli vyao wakidhani ni waandamanaji.

Nchi za wenzetu maandamano yanaonekana kweli ni maandamano kwasababu binadamu siku zote humanity barabarani kwa mguu, ni magari tupu.
 
Kuna vijana wametangaza kubeba vidumu vya petrol kwenda navyo kwenye hayo maandamano.

Maandamano yanataka yasiwe na kikomo, yafanyike kila kata nchini.

Hakuna nchi duniani inayoweza kuruhusu maandamano ya hivyo. Hata kule Marekani walitumia Jeshi kudhibiti maandamano yasiyo na kikomo.

Vilevile, hawajafanya jitihada zozote za kuaddress matakwa yao. Kwa mfano, wagombea ubunge na udiwani wanaweza kufungua kesi. Wakapeleka ushahidi kama wanao. Mgombea Urais anaweza kutafuta dialogue na upande wa pili kupitia wasuluhishi mbalimbali.

Maandamano bila kikomo nchi nzima ni uhaini. Ni wajibu wa jeshi la wananchi pia kudhibiti uhaini.
Mpore uchaguzi then mtake watu watii sheria. Mmezoe uharamia. Sasa basi.
 
Kuna vijana wametangaza kubeba vidumu vya petrol kwenda navyo kwenye hayo maandamano.

Maandamano yanataka yasiwe na kikomo, yafanyike kila kata nchini...
Nenda wewe kafungue kesi ya kuzuia maandamano, Mahakama ziliwekwa MFUKONI na Magufuli muda mrefu hatuwezi kwenda KUJISUMBUA TU HUKO. Sisi tunaingia barabarani mapema sana
 
Mimi nadhani itakuwa ni busara kwa serikali kuwaachia Lissu na Hamad kufanya maandamano yao, tena iwape ulinzi mzuri na thabiti kusudi maandamano hayo yasiharibu mali za watu wengine...
Magufuli aruhusu maandamano? labda ya kumpongeza.
 
Mimi nadhani itakuwa ni busara kwa serikali kuwaachia Lissu na Hamad kufanya maandamano yao, tena iwape ulinzi mzuri na thabiti kusudi maandamano hayo yasiharibu mali za watu wengine...
Frustration anayo Magufuli, aliyeiba kura kweupee!

Ndio maana anazuia maandamano!

Lissu na Hamad wasingeandamana wangeshindwa kihalali, shinz!
 
Back
Top Bottom