Serikali isiwazuie Lissu na Hamad kufanya Maandamano

Sikwaziki ila nataka kuona hizi kelele mnapiga hapa zifanyike kwa matendo tuyaone kweli hayo maandamano ya Amani isije kuwa kama ya Mangekimambi.
Wengine wahamasishaji tu hawawezi kuwepo kwenye maandamano. Mimi binafsi sitakuwepo lakini sioni tatizo wakiandamana ,ni haki yao kikatiba sema kuna watu hawaitii tena katiba yetu, wanaifananisha na vijarida vya ABC vya chekechea.

Mtu anaandamana badala ya kwenda kusikiliza shida zake (hii hufanywa na viongozi wastaarabu wanaojua thamani ya kuwa kiongozi) wewe unatuma jeshi likawatawanye ( hii hufanywa na viongozi waoga wanaodhani mauaji ni suluhisho)
 
Hatukutaki humu leo nenda kaandamane huja ambiwa uwe ripota [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] saa mbil kasoro hii
 
Nilidhani utasema watu waachwe waandamane kutumia haki yao kikatiba kumbe wewe unasema itasaidia kutoa frustration za kushindwa na ndio hivi ccm inafurah wananchi kuwa wajinga na kutotambua haki zao kikatiba kujengewa hofu kila kitu wananchi wakipewa au kuruhusiwa kufanya kionekane ni hisani..
 
Mimi nadhani itakuwa ni busara kwa serikali kuwaachia Lissu na Hamad kufanya maandamano yao, tena iwape ulinzi mzuri na thabiti kusudi maandamano hayo yasiharibu mali za watu wengine...
Shida wanatumia vijana ambao hawajitambui, wavuta bag, wanachoma matairi, wangekuwa wanatumia ustarabu ingefaa zaidi,, lakn kwa sas WAPIGWE TU
 
Usinichanganyie Battery Na Gunzi Hiyo Torch Sitaiwasha
😁😊😅😄
 
Hoja yako ni ya msingi, Ila kama hao majizi wasingekuwa wamekwiba uchaguzi.

"The guilty are always afraid."
Hakuna ushahidi wowote kuonyesha kuwa kulikuwa na wizi wa kura. Kuna mazingaombwe yaliyofanywa na upinzani walipokuwa wanaona wanashindwa ili kutafuta sababu ya kutokea kwa kujifanya kuwa kukamata kura za bandia lakini wakawa wanazichoma badala ya kuzishika ili wazitoe ushahidi. Tena hiyo imeonekana katika majimbo mawili tu, ya Kawe na Kigoma mjini!
 
Usinichanganyie Battery Na Gunzi Hiyo Torch Sitaiwasha
😁😊😅😄
Hii picha ni zamanai kdiogo, ila huyo jamaa hapo kulia anaonekana an roho ya kinyama kweli
 
Unapotimiza haki yako ya kuandamana jua kuwa kuna mwingine anahitaji kutimiza haki yake ya kufanya kazi, kuwa na mali, kupata elimu, tiba n.k hivyo utaona umuhimu wa kuyazuia maandamano kwani haki nyingine zote hizo zinawekwa rehani.
 
ili badae muanze kulilia haki za binadamu?
 
Maandamano hayo pia yanaweza kuonyesha ukweli wa taarifa za waangalizi wa uchaguzi.
 
Ungeitaka serikali iwazuie polisi ambao wako mitaani wanaandamana na kuwatia hofu wananchi.
 
Wagawe uwatawale ... Tayari wamefanikiwa kutugawa wakoloni weusi.
 
Magufuli aruhusu maandamano????......labda ya kumpongeza.
Sawa wa kumpongeza nao wapange maandamano yao bila kuingilia ya wapinzani yanayokubalika kikatiba. Maandamano ya amani hugeuka kuwa vurugu Polisi wanapoingilia kati kujaribu kuyavunja kwa maagizo ya woga toka juu. Kama Rais ameshinda kihalali woga wa maandamano ya amani ya wananchi unatokana na nini? Mgombea wa Urais anaogopa hata kushiriki midahalo/mijadala ambayo wagombea wenzake walishiriki vizuri sana na yeye ndiyo akachaguliwa, ataongozaje nchi kama anaogopa kila linalokuja? Ingekuwa ni Mimi kwenye nafasi yake ningeomba kuyapokea maandamano hayo ya wapiga kura wangu nijibu hoja zao zote kuhusu ushindi wangu wa kishindo kufikia kikomo cha maandamano mpaka Uchaguzi mwingine. Tanzania inahitaji Rais jasiri wa kukutana na yote yanavyokuja!
 
Kama ameogopa uchaguzi huru na wa haki kwanini asiogope maandamano???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…