Masuala ya ajira huwa ni ajenda kuu kwenye chaguzi kote ulimwenguni. Mgombea anatarajiwa kuweka mikakati yake na projections zake wazi kuwa atazalisha ajira ngapi katika kipindi gani.
Ajira si jambo la kufanyia mzaha.
Ajira za watu kupotea katika kipindi cha serikali moja, ni moja ya vigezo vikuu vya kuifurusha serikali hiyo kutoka madarakani kupitia sanduku la kura.
Kukua kwa ukosefu wa kazi kunatosha kuipumzisha serikali moja ili ikaje na mipango inayoeleweka kama ingependa tena kuja kushika hatamu za uongozi.
Serikali inayokuja na mkakati wa wazi wa kujivua jukumu hili inalijua kweli inalolisema?
Serikali ya namna hii inatoa matumaini yapi kwa vijana mashuleni na vyuoni au wahitimu walioko mitaani bila ajira?
Ikumbukwe kama ilivyo kwa ajira kila vinavyoelea vimeundwa.
Kwani kama Hashim Rungwe au awaye yote ana suluhisho bora zaidi la tatizo hili, kulikoni kutompa yeye dhamana?
2025 haiko mbali kwamba mlioshiba hamtujui wenye njaa?
Tukutane kwenye sanduku la kura 2024/25.