Serikali isiyo na wajibu wa kutengeneza ajira ni ya nini?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Masuala ya ajira huwa ni ajenda kuu kwenye chaguzi kote ulimwenguni. Mgombea anatarajiwa kuweka mikakati yake na projections zake wazi kuwa atazalisha ajira ngapi katika kipindi gani.

Ajira si jambo la kufanyia mzaha.

Ajira za watu kupotea katika kipindi cha serikali moja, ni moja ya vigezo vikuu vya kuifurusha serikali hiyo kutoka madarakani kupitia sanduku la kura.

Kukua kwa ukosefu wa kazi kunatosha kuipumzisha serikali moja ili ikaje na mipango inayoeleweka kama ingependa tena kuja kushika hatamu za uongozi.

IMG_20230115_092933_511.jpg

Serikali inayokuja na mkakati wa wazi wa kujivua jukumu hili inalijua kweli inalolisema?

Serikali ya namna hii inatoa matumaini yapi kwa vijana mashuleni na vyuoni au wahitimu walioko mitaani bila ajira?

Ikumbukwe kama ilivyo kwa ajira kila vinavyoelea vimeundwa.

Kwani kama Hashim Rungwe au awaye yote ana suluhisho bora zaidi la tatizo hili, kulikoni kutompa yeye dhamana?

2025 haiko mbali kwamba mlioshiba hamtujui wenye njaa?

Tukutane kwenye sanduku la kura 2024/25.
 
serikali ina wajibu wa kutengeneza ajira hama kwa kuwajili au kuwezesha wajili binafsi na taasisi kuongeza ajira ikiwa kuna sera safi.
tanzania ndio nchi pekee maskini ni mtaji wa ccm
 
Ajira hazichipuki zenyewe kama uyoga. Sera za nchi, Kodi, tozo, Sheria, urasimu, rushwa, mapendeleo nk vimekaa je kuikuza au kuiua sekta binafsi.

Vipi raslimali za taifa zinatunufaisha je sote?

Biashara ngapi zinakufa na Kwa nini?

Kwanini ajira serikalini kuwa ni za kudumu? Vipi hii jamii ya walamba asali kuwa ni wao tu kunako ajira na keki ya taifa?
 
Masuala ya ajira huwa ni ajenda juu kwenye chaguzi kote ulimwenguni. Mgombea anatarajiwa kuweka mikakati yake na projections zake wazi kuwa atazalisha ajira ngapi katika kipindi gani.

Ajira si jambo la kufanyia mzaha.

Ajira za watu kupotea katika kipindi cha serikali moja, ni moja ya vigezo vikuu vya kuifurusha serikali hiyo kutoka madarakani kupitia sanduku la kura.

Kukua kwa ukosefu wa kazi kunatosha kuipumzisha serikali moja ili ikaje na mipango inayoeleweka kama ingependa tena kuja kushika hatamu za uongozi.

View attachment 2481663

Serikali inayokuja na mkakati wa wazi wa kujivua jukumu hili inalijua kweli inalolisema?

Serikali ya namna hii inatoa matumaini yapi kwa vijana mashuleni na vyuoni au wahitimu walioko mitaani bila ajira?

Ikumbukwe kama ilivyo kwa ajira kila vinavyoelea vimeundwa.

Kwani kama Hashim Rungwe au awaye yote ana suluhisho bora zaidi la tatizo hili, kulikoni kutompa yeye dhamana?

2025 haiko mbali kwamba mlioshiba hamtujui wenye njaa?

Tukutane kwenye sanduku la kura 2024/25.
Kwani ujui kazi pekee anayoweza huyo ni kula na [emoji90][emoji90]tu magogoni
 
img_20230115_092933_511-jpg.2481663

Hana exposure ya kutosha masikini ya Mungu, maskini Tanzania.

Ukienda nje huko kila siku ya Mungu maredioni na magazetini wanatoa takwimu za ajira, mfumuko wa bei, GDP, deni la Taifa, consumer confidence, vikapanda vikashuka, halafu wanalaumiana sababu ni nani, chama tawala, sera, ubishi wa waziri, bunge, au forces za uchumi duniani .... kiiiila siku ya Mungu.

Wakati anapewa Umakamu Rais kuna watu tuliuliza qualification zake, tukaambiwa ana international exposure, kipindi fulani alifanya kazi mradi wa FAO Zanzibar. Mi sikuona inatosha. Sasa yanatutokea puani.

Tuna tatizo kitaifa la kutotafuta the most qualified people among us to lead us. Anybody can be anything.
 
Hana exposure masikini ya Mungu, maskini Watanzania.

Ukienda nje huko kila siku ya Mungu maredioni na magazetini wanatoa takwimu za ajira, mfumuko wa bei, GDP, deni la Taifa, consumer confidence, vikapanda vikashuka, halafu wanalaumiana sababu ni nani, sera na chama tawala au ubishi wa mtalawa, au forces za uchumi duniani .... kiiiila siku ya Mungu.

Wakati anapewa Umakamu Rais kuna watu tuliuliza qualification zake, tukaambiwa ana international exposure, alifanya kazi mradi wa FAO Zanzibar kipindi fulani. Mi sikuona kama inatosha. Sasa yanatutokea puani.

Tuna tatizo kitaifa la kutotafuta the most qualified people among us to be leaders. Anybody can be anything.

Tunao wajibu wa kuhakikisha katiba ya nchi inabadilika kuzijibu changamoto kama hizi.

Utaratibu ulio wazi, huru na wa haki tokea ngazi za chini kabisa utatupa viongozi bora watakaotuvusha.

Kama ilivyo katika mechi ya mpira kwanini kuwaacha kina Messi au Mbappe nje kama nia yetu ni ushindi?
 
Wale tusio na ajira, vyuoni, mashuleni na wote wenye kuyaweka maslahi ya taifa hili mbele: "mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio na asikie."
 
Ajabu suala la ajira lipo kwenye ilani yao, lakini aliyepewa jukumu la kutekeleza hataki kulifanya, na chawa wa mama ndio wamesajili taasisi wapo kazini kumpigia makofi.

Hili taifa limejaa ujinga from the bottom to the top, tunajiendea kama kondoo tu.
 
Masuala ya ajira huwa ni ajenda juu kwenye chaguzi kote ulimwenguni. Mgombea anatarajiwa kuweka mikakati yake na projections zake wazi kuwa atazalisha ajira ngapi katika kipindi gani.

Ajira si jambo la kufanyia mzaha.

Ajira za watu kupotea katika kipindi cha serikali moja, ni moja ya vigezo vikuu vya kuifurusha serikali hiyo kutoka madarakani kupitia sanduku la kura.

Kukua kwa ukosefu wa kazi kunatosha kuipumzisha serikali moja ili ikaje na mipango inayoeleweka kama ingependa tena kuja kushika hatamu za uongozi.

View attachment 2481663

Serikali inayokuja na mkakati wa wazi wa kujivua jukumu hili inalijua kweli inalolisema?

Serikali ya namna hii inatoa matumaini yapi kwa vijana mashuleni na vyuoni au wahitimu walioko mitaani bila ajira?

Ikumbukwe kama ilivyo kwa ajira kila vinavyoelea vimeundwa.

Kwani kama Hashim Rungwe au awaye yote ana suluhisho bora zaidi la tatizo hili, kulikoni kutompa yeye dhamana?

2025 haiko mbali kwamba mlioshiba hamtujui wenye njaa?

Tukutane kwenye sanduku la kura 2024/25.
Wajibu wa serikali ni kujenga mazingira wezeshi for jobs creation and wealthy creation ili private sector ndio izalishe mali na ajira.
P
 
Ajabu suala la ajira lipo kwenye ilani yao, lakini aliyepewa jukumu la kutekeleza hataki kulifanya, na chawa wa mama wapo kazini kumpigia makofi.

Hili taifa limejaa ujinga from the bottom to the top, tunajiendea kama kondoo tu.

Inasikitisha sana. Labda itakuwa uchawa wa mama ni ajira kwao. Wameajiriwa kumsifia kwa lolote.

"Vijana wa namna hii ni wa hovyo kabisa wasiokuwa na mchango wowote kwa taifa hili." -- in jiwe's words.
 
Hii ndio serikali ya kuharibu ata ajira kidogo za sekta binafsi zilizopo.
 
Wajibu wa serikali ni kujenga mazingira wezeshi for jobs creation and wealthy creation ili private sector ndio izalishe mali na ajira.
P

Serikali haiwezi kujivua wajibu wa kuzalisha ajira directly (kupitia uwekezaji wa moja Kwa moja) au indirectly (kupitia private sector).

Mnufaika wa kwanza kutokana na job creation ni serikali yenyewe kwamba anacho cha kuonyesha kama mafanikio yake kiuongozi. Ili kama vipi tumpe tena dhamana.

Nchi zina raslimali ambazo kupitia hizo zinaweza kufanya uwekezaji. Kwani madege, viwanda, migodi, ma reli nk ni vya nini?

Zingatia:

"Ikumbukwe kama ilivyo kwa ajira kila vinavyoelea vimeundwa."

Hawa wazi wazi wamejivua jukumu la kuona ajira zinazalishwa. Wala si Kwa kumung'unya maneno. Wamesema hawahusiki.

Hawana haja ya kujua ajira ngapi zimezalishwa, ngapi zimekufa na wala kwa nini.

Siyo maajabu ya Mussa hayo?
 
Naona unacheza ngoma ya mwenyekiti.

Nendeni mkafute suala la kutengeneza ajira kwenye ilani yenu, ili muishi kwa amani.

Ngoma za namna hii zinalipa. Hatimaye Kafulila kaula. Au nasema uongo ndugu Pascal?
 
Masuala ya ajira huwa ni ajenda kuu kwenye chaguzi kote ulimwenguni. Mgombea anatarajiwa kuweka mikakati yake na projections zake wazi kuwa atazalisha ajira ngapi katika kipindi gani.

Ajira si jambo la kufanyia mzaha.

Ajira za watu kupotea katika kipindi cha serikali moja, ni moja ya vigezo vikuu vya kuifurusha serikali hiyo kutoka madarakani kupitia sanduku la kura.

Kukua kwa ukosefu wa kazi kunatosha kuipumzisha serikali moja ili ikaje na mipango inayoeleweka kama ingependa tena kuja kushika hatamu za uongozi.

View attachment 2481663

Serikali inayokuja na mkakati wa wazi wa kujivua jukumu hili inalijua kweli inalolisema?

Serikali ya namna hii inatoa matumaini yapi kwa vijana mashuleni na vyuoni au wahitimu walioko mitaani bila ajira?

Ikumbukwe kama ilivyo kwa ajira kila vinavyoelea vimeundwa.

Kwani kama Hashim Rungwe au awaye yote ana suluhisho bora zaidi la tatizo hili, kulikoni kutompa yeye dhamana?

2025 haiko mbali kwamba mlioshiba hamtujui wenye njaa?

Tukutane kwenye sanduku la kura 2024/25.
Sijui ni nani alimpotosha Rais kiasi hiki...Ni hatari sana hata kwa amani ya nchi na usalama...
 
Tatizo la Tanzania wenye akili hawataki kuingia kwenye siasa.

Ninakazia:

"Tunao wajibu wa kuhakikisha katiba ya nchi inabadilika kuzijibu changamoto kama hizi.

Utaratibu ulio wazi, huru na wa haki tokea ngazi za chini kabisa utatupa viongozi bora watakaotuvusha.

Kama ilivyo katika mechi ya mpira kwanini kuwaacha kina Messi au Mbappe nje kama nia yetu ni ushindi?"
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wajibu wa serikali ni kujenga mazingira wezeshi for jobs creation and wealthy creation ili private sector ndio izalishe mali na ajira.
P
Acheni kudanganya viongozi...Wajibu wa kwanza wa serikali ni kutengeneza ajira...Duniani kote...Kama hamwezi kutoa ushauri wa jinsi ya kutengeneza ajira msimpotoshe rais...Kama serikali haiwezi kutengeneza ajira inawezaje dai kodi, ili iweje? Wanalipwa mshahara na pesa za umma kwa ajili ya kazi gani?
 
Back
Top Bottom