Serikali isubiri utekelezaji wa Competency Based Education. Kenya wazazi, walimu na wanafunzi hawaitaki

Serikali isubiri utekelezaji wa Competency Based Education. Kenya wazazi, walimu na wanafunzi hawaitaki

Ujio wa CBC ni moja ya mafanikio katika nyanja ya elimu ambayo wote tunafaa kupokea kwa mikono miwili.
CBC ni carricilum inayozingatia Attitude, Skills na Knowledge kujenga imahiri kwa kuzingatia uwezo na mazingira ya kila mtoto tofauti na Carriculum iliyopita iliyojikita kwenye content/knowledge tu.

Tatizo la CBC , liko kwenye utekelezaji wa mtaala.System ya elimu ya competency based inategemea utekelezaji kutoka kwa wadau 3, mwalimu, mzazi na mwanafunzi + learning environment (infrastructure + facilities) .
MWALIMU
Changamoto ya mdau wa kwanza ni kuwa wengi wa walimu sio competent na hawako tayari kubadilisha teaching methodologies zao(wengi wao waliingia kwenye taaluma ya ualimu baada ya kufeli)-wadau hawa muhimu ndio watekelezaji wanaotegemewa kwa 50% ya utekelezaji kama watoa muongozo na kundi linalotafsiri mtaala wa CBC.

MZAZI
Mzazi-Mdau huyu anafaa kusaidia mwalimu kwa kumpa mtoto fursa ya kuwa na muda, mazingira na baadhi ya zana za kjifunzia (learing aids) pale zinapohitajika.Mzazi anahitajika kuwajibika katika ufatiliaji na utekelezaji wa kazi za nyumvani ambazo zaidi ya 80% zinafaa kuwa practicals/ projects (wamezoea homeworks za maswali ya kawaida na yasiyofikirisha).
Kwa kuzingatia hali ya kiuchumi na kupambana katika utafutaji wa rizki, wazazi wengi hawana muda wa kutekeleza jukumu la kusimamia watoto wao ili kuwajengea nidhamu na kuwaandaa kwa majukumu yanayojenga competency/umahiri.
Watoto wanapopewa kazi zinazofikirisha baadhi ya wazazi huchukuwa jukumu la kuwafanyia watoto wao assignments zao na baada ya muda flani wanaanza kuona kama hawatendewi haki kwasababu wamelipa ada! Na kuwa hili jukumu ni usumbufu.

MWANAFUNZI
Wanafunzi wengi wamesombwa na wimbi la utandawazi, burudani na uvivu.CBC inahitaji mwanafunzi, mwenye tabia ya kujisomea, mwenye nidhamu , anaezingatia matumizi sahihi ya muda, anaejituma na mwenye kiu ya kutaka kufahamu mambo tofauti tofauti.
Hili linategemea malezi, makuzi na aina /uongozi wa shule husika/waalimu.
Kwa kuzingatia wadau wa kwanza wawili na michango yao hafifu katika malezi na makuzi ukijumjisha na uwezo mdogo wa waalimu wanafunzi wanabaki kusoma mtaala wa CBC kwa kuzingatia content/knowledge. ...kitu ambacho kinasababisha attitude na skills kupotea.
Bila skills na attitufe sahihi, CBC inakuwa na contents nyepesi ila upimaji wake u akuwa mgumu.
Hivyo mwanafunzi anaekutana na Maswali ya application na analysis /evaluation anashindwa kuyamudu maana alipewa contents kidogo tu ambazo zingeongezeka kama angefundishwa skills na angezikumbuka/appreciate (sio kukariri) zaidi kama angekuwa na right attitide.
Maswali ya aina hii yanapokuja kwenye mtihani watoto hufanya vibaya na hivyo kuwavunja moyo na kusababisha hamu yao/motisha yao juu ya somo kupungua.
Na anapokumbana na swali fikirishi la homework au package anaisukumiza kwa mzazi.mzazi anaingia google anadownload majibu mtoto anacopy...

Mwisho wa siku;mzazi anaelimika (anaefanya assignments)mtoto anapewa mtihani, anafanya mitihani.akifeli mtoto anafokewa, mwalimu mkuu anashushwa cheo, waalimu wa private wanafukuzwa kazi.

Wenu katika majukumu.

The consultant.
Quality Assurance and Standards Cosultant.
 
sio lazima tuige kila kitu, tunaweza kutumia hii hii elimu ya mkoloni na kuchanganya na vyetu tukatoboa...

Elimu ya form five na six ifutwe, watu wakimaliza form four waende college wakasome ujuzi moja kwa moja...

Specialization ianzie form one, kama ni wa science asome science tu, hakuna kuchanganya, anayetaka PCM anasoma masoma yake matatu tu, anayesoma PCB anasoma matatu tu, wengine HGL matatu tu..
Elimu ya sekondary inakuwa 3yrs, then college 3yrs then University...

Elimu ya msingi iwe miaka sita au mitano, tuangalie masomo ya kusoma muhimu mengine piga chini, baadhi ya topic zisizo na maana zipigwe chini..

Kingereza kiwe lugha ya kufundishia kuanzia msingi mpaka chuko kikuu, kiswahili kibaki Lugha ya nyumbani tu...
 
Narudia tena, Elimu ya form five na six ni janga katika nchi hii baadala yake kuwe na college education 3yrs mtu anatoka na skills tayari..

Form four isiwepo baadala yake kuwe na form one to form three huku mtu akisoma masomo matatu tu aliyochagua, labda mwisho yawe manne kwa maana ya moja ni option tu..

Kutoka form three kwenda college ni GPA zinaangaliwa kuanzia form one to three...

Watakaoshindwa kupata GPA nzuri kwenda college wanapata scholarship wote kwenda Veta na huko wakipata GPA nzuri wanakwenda college.....au wanarudia mwaka mmoja sekondari wanapiga paper masomo yao matatu na average marks ziwe min GPA ya 6 (BBB)
 
I am sure Mheshimiwa Jumanne Kishimba (Mbunge wa Kahama Mjini) ana common sense understanding ya CBE nzuri kuliko hiyo yake!
Sidhani Jumanne Kishimba hata hajui kuna mdau kaeleza vizuri sana kuwa mfumo unahitaji mzazi pia ushirikiano wake mkubwa ili ufanikiwe

Mfano Kishimba ana biashara nyingi tu kubwa lakini alilalamika bungeni kuwa mwanawe kamaliza digriii na serikali haijamwajiri!!!!!

Unamkuta mzazi ana malori zaidi ya mia ya usafirishaji ungetemea mtoto wa huyo tajiri ambaye hajasoma mwanae akasomee mambo ya usafirishaji chuo cha usafirishaji au ufundi magari au businesss administaration ,marketing na vitu related na hiyo biashara ili aweze kuwa part ya kuiendesha hiyo kampuni aipeleke mbali zaidi!!! Lakini utashangaa mtoto anaenda kusomea ualimu ambao baadaye analalamika serikali kushindwa kuajiri!! Competency ya Elimu ya mtoto inahitaji ushiriki wa mzazi pia
Wahindi,waarabu na wapemba wako vizuri mno kwenye hilo .Waswahili ngozi nyeusi kuna shida au laana .Mikampuni ya kiswahili mikubwa kabisa akifa mwenyewe mzazi nayo inakufa hakuna mtoto competent wa kuendesha halafu lawama zote serikali ndio inalaumiwa kuwa inatoa elimu hafifu wakati mitoto yenyewe haipewi direction na mzazi kuwa concentrate area hii mimi nazeeka au ushindani uko kasi teknolojia zinabadilika siwezi cope uje ku take over uendeshaji kampuni kisasa

Mzazi mfano ana biashara kubwa za ujenzi za real estates mtoto anaenda kusomea udaktari .Mzazi akifa obvious kampuni inakufa mtoto yuko zake hospitali anazalisha wajawazito !! Sijui kwa nini watoto hawawi directed area hizo za business za wazazi au huwa zinaanzishwa kishirikina na uendeshaji unahusisha zaidi ushirikina au?
 
Serikali isubiri utekelezaji wa Competency Based Education kenya wazazi,walimu na wanafunzi hawautaki

Baadhi ya vyama vimeweka kama Agenda ya uchaguzi kuwa wakishika madaraka hup mfumo wa Competent based wataufuta sababu walimu hawautaki,wazazi hawautaki na wanafunzi hawautaki na wanashangiliwa sana

Serikali vizuri ikajifunza kupitia kenya kabla kukurupuka kuuanzisha.Wao walijiingiza kichwa kichwa
Ni competence based,siyo competent based.
Jipe muda usome vizuri aina za mitaala; competence based na content based curricula.
Tatizo kubwa wa huu mtaala ni utekelezaji,na si aina ya mtaala wenyewe.

NB:Msipotoshe kitu msichokijua.
 
Ingekuwa about telent ingeitwa TBE....😂😂
Mwalimu labda unieleweshe !
Mimi nilivoelewa huu ni mtaala unaofundisha kutokana na uelekeo wa mwanafunzi , ukisema tallent unakosea sana maana si kila mtu amekuwa gifted hivyo
MK254 ameeleza hapo juu kuwa ngedere na samaki wote wanafundishwa kuogelea na kupanda miti , utaona kuwa kila mmoja atafaulu na kufeli kwa wakati wake ,
Cbe inafanya ngedere afundishwe kupanda miti na samaki wafundishwe kuogelea , ili wote wawe experts kwenye nyanja husika .
 
Achana na articles za mtu mmoja mmoja hizi. Soma institutional publications ndipo utapata a more accurate understanding of a Competency-Based Education (CBE) model.

Kwa kifupi, CBE inaleta flexibility katika kujifunza. Student anajifunza kwa pace yake. CBE emphasizes mastery of skills rather than the time-based completion of required credits. Mtu sio lazima atumie miaka saba kumaliza elimu ya msingi au miaka minne kumaliza o’level, kwa mfano. Anaweza kutumia muda mfupi au mrefu, depending on individual learning pace or needs.

THE FIVE ELEMENTS OF CBE

[emoji3578]Students advance upon mastery.

[emoji3578]Competencies include explicit, measurable, transferable learning objectives that empower students.

[emoji3578]Assessment is meaningful and a positive learning experience for students.

[emoji3578]Students receive timely, differentiated support based on their individual learning needs.

[emoji3578]Learning outcomes emphasize competencies that include application and creation of knowledge, along with the development of important skills and dispositions.
Mbona kama unaeleza kitu kile kile ninachoelewa au kueleza

Mi nilivyoelewa kuwa badala ya mtoto kubeba vitqbu saba vaya masomo sita amabayo hatayatumia , Cbe inalenga kumshape mtoto kutokana na uelewa au response yake kwenye masomo au fani flani, ie kama mwanangu anaonyesha kupenda IT cbe inafanya emphasis kwenye masomo yanayoendana na fani hiyo, na ni obvious mtoto anaweza akawa master wa fani flan katika muda mfupi .
 
Kenya sio shule ya tz...hatujifunzi kwao!!! Dunia yasasa ujuzi ndiyo kilakitu na sio kukariri-kariri kulikotuletea maprofesa pumbafu!!
Mkuu unaakili sana.Tanzania Kuna baadhi ya Idara zinajifunza kutoka Kenya ,ni ushamba sana.Kuna kozi ya Afya ilianzishwa Kenya ,Wanafunzi wa Tanzania waliosoma hiyo kozi nakuja hapa Tanzania kwenye usajili Dr.Mzava ilibidi aende KENYA kujifunza ndipo wawasajiri.Chakushangaza Zaidi taratibu zinazotumika Kenya ndo hizo hizo walicopy na kupaste.
 
Sidhani Jumanne Kishimba hata hajui kuna mdau kaeleza vizuri sana kuwa mfumo unahitaji mzazi pia ushirikiano wake mkubwa ili ufanikiwe

Mfano Kishimba ana biashara nyingi tu kubwa lakini alilalamika bungeni kuwa mwanawe kamaliza digriii na serikali haijamwajiri!!!!!

Unamkuta mzazi ana malori zaidi ya mia ya usafirishaji ungetemea mtoto wa huyo tajiri ambaye hajasoma mwanae akasomee mambo ya usafirishaji chuo cha usafirishaji au ufundi magari au businesss administaration ,marketing na vitu related na hiyo biashara ili aweze kuwa part ya kuiendesha hiyo kampuni aipeleke mbali zaidi!!! Lakini utashangaa mtoto anaenda kusomea ualimu ambao baadaye analalamika serikali kushindwa kuajiri!! Competency ya Elimu ya mtoto inahitaji ushiriki wa mzazi pia
Wahindi,waarabu na wapemba wako vizuri mno kwenye hilo .Waswahili ngozi nyeusi kuna shida au laana .Mikampuni ya kiswahili mikubwa kabisa akifa mwenyewe mzazi nayo inakufa hakuna mtoto competent wa kuendesha halafu lawama zote serikali ndio inalaumiwa kuwa inatoa elimu hafifu wakati mitoto yenyewe haipewi direction na mzazi kuwa concentrate area hii mimi nazeeka au ushindani uko kasi teknolojia zinabadilika siwezi cope uje ku take over uendeshaji kampuni kisasa

Mzazi mfano ana biashara kubwa za ujenzi za real estates mtoto anaenda kusomea udaktari .Mzazi akifa obvious kampuni inakufa mtoto yuko zake hospitali anazalisha wajawazito !! Sijui kwa nini watoto hawawi directed area hizo za business za wazazi au huwa zinaanzishwa kishirikina na uendeshaji unahusisha zaidi ushirikina au?

Hivi unaamini kwa dhati ya moyo wako kuwa kila mtoto wa mfanyabiashara ana interest ya kuwa mfanyabiahara?

That aside, a successful businessperson isn’t minted in a classroom!
 
Ni competence based,siyo competent based.
Jipe muda usome vizuri aina za mitaala; competence based na content based curricula.
Tatizo kubwa wa huu mtaala ni utekelezaji,na si aina ya mtaala wenyewe.

NB:Msipotoshe kitu msichokijua.
Ukweli 100%. Kunywa soda nakuja kulipa....
 
Mwalimu labda unieleweshe !
Mimi nilivoelewa huu ni mtaala unaofundisha kutokana na uelekeo wa mwanafunzi , ukisema tallent unakosea sana maana si kila mtu amekuwa gifted hivyo
MK254 ameeleza hapo juu kuwa ngedere na samaki wote wanafundishwa kuogelea na kupanda miti , utaona kuwa kila mmoja atafaulu na kufeli kwa wakati wake ,
Cbe inafanya ngedere afundishwe kupanda miti na samaki wafundishwe kuogelea , ili wote wawe experts kwenye nyanja husika .
Nikitulia nitashusha nondo tueleweshane kidogo.
 
Hivi unaamini kwa dhati ya moyo wako kuwa kila mtoto wa mfanyabiashara ana interest ya kuwa mfanyabiahara?

That aside, a successful businessperson isn’t minted in a classroom!
Idea sio kuwa mtoto wa mfanyabiashara awe mfanyabiashara
Idea ni kuwa mtoto a pick up fani yake akiwa mdogo na aweze kuni master fully kwa msaada wa mtaala husika , mathalani labda mtoto awe IT expert, si anaweza kumsaidia baba yake mfanyabiashara kwenye fani hiyo? ,Badala ya kuwa na degree ambayo inamlazima aajiriwe tu
 
Mbona kama unaeleza kitu kile kile ninachoelewa au kueleza

Mi nilivyoelewa kuwa badala ya mtoto kubeba vitqbu saba vaya masomo sita amabayo hatayatumia , Cbe inalenga kumshape mtoto kutokana na uelewa au response yake kwenye masomo au fani flani, ie kama mwanangu anaonyesha kupenda IT cbe inafanya emphasis kwenye masomo yanayoendana na fani hiyo, na ni obvious mtoto anaweza akawa master wa fani flan katika muda mfupi .

Bado unachanganya mambo! Focus ya CBE sio specialization.
 
Hivi unaamini kwa dhati ya moyo wako kuwa kila mtoto wa mfanyabiashara ana interest ya kuwa mfanyabiahara?

That aside, a successful businessperson isn’t minted in a classroom!
Hiyo sentensi yako ya mwisho ndio lengo kuu la mtaala wa CBC.
 
Back
Top Bottom