Serikali itafute njia mbadala kushughulika na wahalifu wa 'Tuma kwenye namba hii', kwenda kuripoti polisi ni kupoteza muda

Serikali itafute njia mbadala kushughulika na wahalifu wa 'Tuma kwenye namba hii', kwenda kuripoti polisi ni kupoteza muda

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Waziri Nape alitoa maelekezo watu kutoa taarifa polisi endapo watapokea jumbe za matapeli wanaokwambia tuma kwenye namba hii ama jumbe za waganga na kushinda jackpot ambapo kupata zawadi hiyo unaambiwa upige simu kwa maelekezo zaidi.

Badala ya watu kwenda kutoa taarifa polisi, kuwe na njia ya kidigitali ambapo mtu akipokea ujumbe huo ataweza kutoa taarifa hapohapo kwenda TCRA na ujumbe huo kupokelewa ukiwa taarifa zote na kuushughulikiwa moja kwa moja badala ya kuwa na mzunguko wa kwenda polisi, polisi nao wajivute mpaka kupeleka taarifa hizo TCRA watu wengi watakuwa wameshatapeliwa.
 
Nami sasahivi imetoka kuingia hii.
Screenshot_20230227-210857.jpg
 
Back
Top Bottom