Serikali itenge fedha za kukarabati shule za Msingi nchi nzima, hali ya shule hizo ni mbaya

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Kwenye bajeti ya Serikali juu 2021/22 sijaona fedha zilizotengwa na Serikali kukarabati shule za Msingi Tanzania.

Shule nyingi za Msingi Tanzania sasa zimekuwa magofu. Hapa Kilosa Mkoa wa Morogoro kuna shule ya msingi inaanguka.
 
weka picha. Pia shule hazikarabatiwi na Wzara ya elimu. Shule zipo chini ya Tamisemini. So toa taarifa kwa mkurugenzi wa wilaya
 
Watoto wanakaa chini..inauma sana.. oondoeni ujinga wa wazazi kutochangishwa..ni ujinga..wachangie Elimu jaman.

Basi wasaidie kipengele walau kimoja cha dawati
 
Hiyo shule inayotaka kuanguka,wakuonyeshe kwenye fedha za uendeshaji kipengele cha ukarabati wana shilingi ngapi kwa mwaka,na wamekarabati wapi?
 
Mkuu, yeye anasimamia sera tu.

Shule za msingi na sekondari zipo chini ya TAMISEMI
 
weka picha. Pia shule hazikarabatiwi na Wzara ya elimu. Shule zipo chini ya Tamisemini. So toa taarifa kwa mkurugenzi wa wilaya
Mkurugenzi wa wilaya ameshindwa kuwalipa madiwani wa CCM mshahara 350,000@ Kwa mwezi,hataweza kukarabati shule zaidi ya 49 zilizopo kwenye Halmashauri yake?
 
Si tuliambiwa shule zimejengwa nchi nzima
 
Vipi ule mpango wa mmem haukukarabati shule zote? Au zilikarabatiwa lakini sasa zimechakaa? Pia zikarabatiwe nyumba za walimu ni aibu hasa za vijijini zingine ni za miaka ya 70 ni aibu mwalimu kuishi kwenye magofu huku anatoa elimu kwa wanafunzi kwenye madarasa mazuri
 
Tushapoteza dira kama Taifa, ngoja tuone kama PK atatuokoa.
 
Kwenye bajeti ya Serikali juu 2021/22 sijaona fedha zilizotengwa na Serikali kukarabati shule za Msingi Tanzania.

Shule nyingi za Msingi Tanzania sasa zimekuwa magofu. Hapa Kilosa Mkoa wa Morogoro kuna shule ya msingi inaanguka.
Habari nusunusu.
 
weka picha. Pia shule hazikarabatiwi na Wzara ya elimu. Shule zipo chini ya Tamisemini. So toa taarifa kwa mkurugenzi wa wilaya
Shule inakaribia kuanguka mkurugenzi na wasaidizi wake hawaioni mpaka mwananchi awapelekee taarifa ofisini?
Ni ipi kazi ya Mwalimu Mkuu, Mwenyekiti wa kamati ya Shule, Diwani, Mratibu Elimu Kata, Ofisa Elimu?
 
Watoto wanakaa chini..inauma sana.. oondoeni ujinga wa wazazi kutochangishwa..ni ujinga..wachangie Elimu jaman.

Basi wasaidie kipengele walau kimoja cha dawati
Kwani serikali imeshindwa kuzihudumia shale zake au haitaki?
Serikali kama imeondoa michango sisi ni nani tulazimishe ?
Jambo la msingi kwa wananchi waende wakalie na Mkurugenzi wao mpaka shule yao ijengwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…