Tetesi: Serikali itoe ufafanizi kuhusu tetesi za mfumo wa uhamiaji KuCollapse maana kuna baadhi ya viashiria vipo

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
17,595
Reaction score
39,893
Moja kwa moja.

Juzi niliona Uzi wa member wa Jf ambaye amelelemika kuwa wiki nzima anarudishwa uhamiaji wakati wa kufuatilia passport anaambiwa kuwa Kuna Virus kwenye mfumo na data hazipo , kaambiwa atulie .

Na Mimi mwenyewe ndugu zangu zaidi ya wawili wanasubiri Visa ya kwenda nchi Fulani mpaka sasa bado wanasubiri na imekuwa kipindi kirefu sio kawaida .

Leo Kuna posti hii ya kutoka kwa Maria Sarungi kuhusu mfumo wa uhamiaji inayozua taharuki .
===============
MFUMO WA UHAMIAJI UME COLLAPSE !!

Jamani hali bado haijatengamaa ila tatizo ni KUBWA Kwa mujibu wa mtoa taarida mfumo unaonekana kuharibiwa kwa makusudi kwani umefuta kumbukumbu zote za paspoti, visa, na hata mipakani kuingia. Ni kwamba taarifa zote kuanzia mwaka 2025 zimefutika!
Mnaelewa uzito wake!!??

Hii ina maana kama kuna wauwaji au magaidi au wahalifu wowote waliingia kipindi hicho basi taarifa zao hazipo kabisa kwenye mipaka na airport zetu. Hata watanzania waliopata pasipoti kipindi hicho taarifa zao zimefutika, so kama zilitolewa pasipoti kwa watu ambao sio watanzania maana yake hatuwezi kujua tena.
Kibaya zaidi mifumo ime-collapse hadi kwenye balozi zetu zote za nje ya nchi. Maana yake ni kuwa hata nje ya nchi walifunga mfumo wa e-Passport na e-ETD kwa hiyo watanzania wakipata changamoto huko hawawezi kurudi nyumbani.

Sasa tutafakari: kwa mwezi uhamiaji inakusanya Bilioni 25, na kwa madudu haya serikali imekubali kupoteza mapato hayo kwa faida wanayoijua wao. Kamishna wa uhamiaji Makakala yupo tu, hajaguswa!
Akili kichwani! Nchi inaendeshwa KIHUNI kabisa na genge la wahalifu!
Tukisema nchi imewashinda mnatuona wakorofi

Uhamiajina mifumo saba na yote ime
collepse
Dorder
-Pesaport
-Visa
e-Parma
e-Pussee
-ETD e-Ajka

Taarifa nite za kwenye mifumo hiye tang 2025 hadi bo zimafriks
Mikoo vote hakuna kazi inayofanyika, wenalazimisha tu kwa Kamini-Do ambayo nayo hait in kombukumbu Maafisa Uhamail wote hichi nzima wamsambiwa watabedilshiwa usemime na pessword matengenero vakkamilika.

 
Utasikia mtu anasema wanaharakati wanatumika , imagine katika nchi ambayo media ziko mateka na kugeuzwa vuvuzela za CCM jambo kama hili zito wamelikalia kimya walioliibua ni wanaharakati na ushahidi upo watu wamekosa huduma ila hao immigration wako kimya.

Wanaharakati wana nafasi yao na wataendelea kuwepo na wataibuka wengi tu katika zama za giza kuziba ombwe la habari kuchujwa kupitiliza.
 
inawezakana kuna wafanyakazi wachache wasiowadilifu wanao ifanya ofisi ya uhamiaji kutenda haki na kufanya kazi chini ya kiwango
 
Naomba kuuliza pengine niko nyuma.

HAo wauaji, wahalifu kutoka nje kwani lazima wapite mpkani waache taarifa zao.
Si wanaingia kama wahamiaji haramu wanavyoingia sema wao wanakuwa wanalindwa na mfumo.
Hata mimi nashangaa , ndio maana napata wasiwasi na taarifa wakati serikali inaweza kuingia mtu kimafia kama wakitaka lao bila kuleta mambo mengi
 
Daah kazi ipo aisee ngoja nisubiri wathibitishe taarifa hao wahusika naona wamekaa kimya mno..
 
Inakuwaje taasisi kama Uhamiaji inayokusanya mabilioni ya fedha ikose mfumo madhubuti wa Disaster Recovery au Off-site Backup?

Kuna kitu hakipo sawa mahali.
 
K
MAGUFULI lazma akumbukwe, serikali hii imejaa wapuuzi na Wala rushwa wakubwa

Ingekuwa ni mwamba MAGUFULI mpaka Sasa Kuna vilaza wangekuwa tayari wako nyumbani wanachunga ng'ombe wengine wangekuwa wananyea debe jela, kuanzia mkuu wa uhamiaji na wenzake wote mpaka waziri muhusika na kingeeleweka tuu
 
Af
Afu wawalipe watu gharama walizotumia za kujaza mafomu na kugharamikia passport wasifanye nchii hii kama shamba la bibi Yao mamaye zao
 
Mkuu hii ni hasara wamewatia wananchi hasara ya kurudia kujaza fomu za 20,000 upya na Bado na rushwa wanataka, serikali hii ya kipumbavu sana imeoza mpaka inanuka uvundo
 
Tulieni mwendelee kuangalia channel ya vichekesho!
Tanzanite inazalishwa Tz pekee, ila Tz ni exporter namba tatu baada ya india na kenya🤣🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…