Serikali ituambie sasa ni lini na wapi zabuni ya uwekezaji wa bandari ilifanyika?

Nenda mahakamani kamshtaki waziri kavunja sheria. Ila msituletee udini, ukabila mitaani, amani muhimu kuliko tamaa zenu za madaraka.
 
Una maana kwamba siku ile bendera ya Tanganyika inawakawaka kwenye lile jengo ndio Watanganyika tuliuzwa rasimi?
 
Kwani hujui kuwa kuna kesi mahakamani?
 
Ni kawaida sana kujifunza kutokana na makosa.
Yalishatokea hapo kabla hivyo km tuna utimamu wa akili ni lazima kusahihisha makosa yetu.
 
Uchaguzi wa nchi gani mkuu?
Maana hapa kwetu huwa kuna maigizo.
 

Hasira zote hizo, kumbe una Ukereketwa??!!!!
 
KUNGEKUWA NA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA WAZIRI ANGEZIONYESHA BINAFSI NAAMINI DP WORLD WAMETEULIWA TU na MAFISADI
 
huyo mbarawa lazima atanyea debe. Ni kusubiri tu hawa madhalimu watoke madarakani
 
Wakati wa JPM hakuna wanaharakati waliokosoa, viongozi wa dini waliokosoa? Wanasiasa waliokosoa?

Ngoja nikuulize, fatma karume na Maria sarungi walikua wanamkosoa nani?

Wanasiasa Kuna haja wa kuwataja kweli? Hawa kina zitto na chadema wote walikua wanamkosoa ni? Lema Lissu sugu mbowe heche n.k hawa wote walikua wakiitwa polisi kufanya nini?

Viongozi wa dini wengi waliibuka wakosoaji wakati wa Magufuli,ngoja nikutajie askofu shoo, bagonza, mwamakula, niwemungizi hadi akapaata kesi ya uraia, kakobe alipewa hadi kesi, kitime na TEC waitoa hadi waraka kupinga anachofanya Magufuli

Au hukua Tanzania?
 
Karume and Sarungi hawa watoe humu wana maumivi yao kuhisi wazazi wao wametupiliwa mbali. Hao viongozi wa dini walikuwa wanakosea lakini hawakuwahi kutumia maneno ya kumuita hadharani huyu Msukuma, walikuwa wanamkosoa na ujumbe unafika., ila wachache. Leo wamechiwa imekuwa unamuita Rais matusi. waliokuwa wanamtukana matusi JPM walikuwa wanajificha wengine wanakosoe kwa heshima. JPM alikuwa hana ustahimilivu ukivuka mipaka yake.
 
Kwa mawazo yako kila anaekosoa mkataba huu ana interest za kisiasa na mawazo ya uchaguzi..huu ulevi wa kichama hata kwenye rasilimali za taifa mnautoaga wapi?
 
Ni kwa sababu alikuwa hafanyi mambo ya hovyo ambayo hata mtoto mdogo anaweza kubaini, alijua kuzitetea rasilimali za taifa kwa sauti na vitendo
 
Ni kwa sababu alikuwa hafanyi mambo ya hovyo ambayo hata mtoto mdogo anaweza kubaini, alijua kuzitetea rasilimali za taifa kwa sauti na vitendo
Sasa rasilimali kazi yake ni nini? kuzikalia au? elimu zero hii mijitu ya CDM. Nyinyi si mlikuwa kila siku mnamtukana JPM leo mnamkumbuka, na bado siku Rais Samia ataondoka kitakuja chuma mtamkumbuka Mama Samia
 
Wataalam toka CCM akina... GUSSIE Lord denning Faizafoxy covax choiceVariable wanakuja na ufafanuzi!!
 
serikali ifanye haya;
-Ituambie ni lini na wapi Zabuni za uwekezaji wa bandari yetu ilitangazwa

-Ni lini makampuni yaliyoomba hizo Zabuni yaliwekwa wazi (zabuni ziliwekwa wazi)

-Ni kampuni gani hizo Saba zilizotajwa na Profesa Mbarawa ziliomba kuwekeza kwenye Zabuni za Bandari.

-Ni lini na wapi Zabuni za uwekezaji wa bandari zilifanyika.
 
Kwa hiyo shida yako wewe zabuni tu? wewe ulikuwa unajuwa zabuni ya SGR, unajuwa zabuni ya bwawa na Nyerere, unajuwa zabuni ya Airport. Shida yako ni nini DP au zabuni au mkataba maana hamjulikani mnataka nini
 
Kuna njia nyingi za kumpata mzabuni sio lazima hiyo unayoieleza wewe.

Wapi na lini nenda wizarani na ppra
 
Nani ana operate airport, watu mnafahamishwa mara mia lakini kwakuwa hamtaki na tunaendeshwa ni mihemuko ya kisiasa ndio tunabaki kuongea vitu havina mantiki mara mmeuza mara hakuna kikomo mare hakuna tender hujui watu wanataka nini.
Zungumzia vipengele vya mkataba. Tafsiri ya jumla ya mkataba huu ni kwamba Tanzania imeiuzia Dubai bandari zake zote za bahari na maziwa yote, pamoja na miundombinu na fursa zozote zilizopo na zitakazojitokeza, na hatuwezi kumualika muwekezaji mwingine bila ruhusa ya Dubai. Shida sio uwekezaji, sio udini wala sio uzanzibari na utanganyika. Shida ni vipengele vya mkataba.
 
Imetangazwa mpaka JF tuliileta. Jifunze kutumia google.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…