Serikali ituambie sasa ni lini na wapi zabuni ya uwekezaji wa bandari ilifanyika?

Serikali ituambie sasa ni lini na wapi zabuni ya uwekezaji wa bandari ilifanyika?

Bandari ilikuwa imekodishwa na TICTS kwa miaka 22 na sasa biashara imekwisha, mbona kamuacha mke na sasa hivi anatafuta bwana mwingine?.
Serikali ilishidwa kuweka continuity plan TICTS wakiondoka waweze kuendesha wenyewe? Investments zilizofanyika io miaka haitoshi kuandaa wazawa kuendesha bandari na hazina maana yoyote? Kama TICTS walikaa miaka 22 hawa watakaa miaka mingapi? Ni makosa gani yalionekana kwenye mkataba wa TICTS na yamekua addressed vipi kwenye mkataba mpya?
 
Profesa Makame Mbarawa amekuwa akisema DP world ilipewa mkataba wa bandari kwa kuwa ilishinda kwenye kuomba zabuni ya uwekezaji wa Bandari (akidai ikizishinda kampuni zingine saba) na wakati huo huo document za mikataba ambazo zimetiwa saini na Professor Mbarawa huyo huyo zinaonyesha DP world walipewa mkataba moja kwa moja bila kupitia mchakato mwingine wowote wa kuomba zabuni baada ya Rais Samia kutembelea Dubai na kutia saini makubaliano ya DP world kuja kuwekeza kwenye bandari yetu.

Kwa kuwa suala la uwekezaji wa bandari ni suala la kisheria, na sheria ya utoaji Zabuni inataka kufanyika mambo kadhaa muhimu ikiwemo.
1. Kutoa tangazo la Zabuni kwenye gazeti la serikali.
2. Kufunguliwa (kuwekwa wazi) kampuni zilizoomba Zabuni.
3. Kushindanishwa (kujadiliwa) kwa Zabuni kwa haki ili kumpata mzabuni mmoja atakayepewa mkataba.
4. Kutangazwa rasmi kwa mshindi wa Zabuni.

Sasa ili kuondoa huu utata, bila kumumunya maneno, tunaitaka sasa serikali ifanye haya;
-Ituambie ni lini na wapi Zabuni za uwekezaji wa bandari yetu ilitangazwa

-Ni lini makampuni yaliyoomba hizo Zabuni yaliwekwa wazi (zabuni ziliwekwa wazi)

-Ni kampuni gani hizo Saba zilizotajwa na Profesa Mbarawa ziliomba kuwekeza kwenye Zabuni za Bandari.

-Ni lini na wapi Zabuni za uwekezaji wa bandari zilifanyika.

-Ni vipi ushindani wa Zabuni ya uwekezaji wa bandari ungekuwa wa haki ikiwa DP world tayari walikuwa wameanza ubia na serikali ya Tanzania kupitia urais wa Tanzania katika kutaka kuwekeza bandarini.
Mie hizo tarehe nitakutumia. Nipe namba yako ya simu na password yako.
 
🤣🤣wewe unataka kumuua mbarawa Sasa,si ana mji wake hapo daslam nenda mzungumze,tulia wenyewe amelikimbia gorofa lake,hapo jiran na saint jose,wamempa na mtaa kabisa hapo,ukigugo jina lake unafika hadi nyumbani kwake,saiv kaweka kambi mbeya,anaongea na machifu pale
 
Hali imekuwa siyo Hali,spin doctors Kila wakijaribu kuleta matukio ya kuwahamisha watz ndo kwanza moto unawaka
 
Na mbaya zaidi hata kujieleza anashindwa
Mbarawa amekuwa Kama mwigulu kuongea kwao tabu🤣🤣 mwigulu kile kiofisi Cha timu yake ya kizushi saivi kakipolish,pita singida,sabasaba barabaran unakiona,muda wote hakina hata secretary,Ila kinafanya kazi🤣🤣
 
Aaahaaaaaa
 
Kwamba zabuni za SGR, bwawa la nyerere hazijulikanai au ndo Mnajitoa ufahamu tu kama kawaida yenu
 
Serikali ilishidwa kuweka continuity plan TICTS wakiondoka waweze kuendesha wenyewe? Investments zilizofanyika io miaka haitoshi kuandaa wazawa kuendesha bandari na hazina maana yoyote? Kama TICTS walikaa miaka 22 hawa watakaa miaka mingapi? Ni makosa gani yalionekana kwenye mkataba wa TICTS na yamekua addressed vipi kwenye mkataba mpya?
Tunatafuta nafasi ya kufika uchumi wa kati wa juu. Kuna suala zima la teknolojia, linaingia katika uwekezaji wa bandarini.
Mwenzangu tambua kuwa mitambo ya bandarini kuimiliki ni kazi kubwa, wewe mwenyewe DummyI unaweza kuniambia tangu uzaliwe umevumbua aina gani ya mtambo wenye kuifaa bandari?.

Ni rahisi sana kusema baada ya TICTS kuwa wameondoka bandarini tulitakiwa sisi wenyewe tuwe wamiliki, uhalisia wa mambo haupo hivyo. Huu ni ulimwengu wa ushindani huwezi kuulinganisha na ule wa miaka ya 80, ni dunia ambayo afrika imeamka na kila bandari inaendelezwa kwa faida ya nchi ilipo.
 
Nenda mahakamani kamshtaki waziri kavunja sheria. Ila msituletee udini, ukabila mitaani, amani muhimu kuliko tamaa zenu za madaraka.
Wanahubiri utanganyika na siasa za udini na ubaguzi wakitumia majina ya bandia, wanadhani kuondokana na madhara ya dhambi hiyo ni kazi nyepesi tu.

Kenya kwa sasa watu wazima wanajuta, wanajua kuwa wanasiasa wenye madaraka watakimbia haraka sana nje ya nchi na kuwaachia maskini mzigo wa ugumu wa maisha.
 
Back
Top Bottom