Serikali itunge sheria kuhusu uzazi wa mpango angalau watoto wawili kila familia maana kasi ya uzazi Tanzania inatisha

@Mathanzua na @safuher mnakubaliana
Nikushukuru sana kwa kunitag hapa,naomba na mimi nitoe maoni yangu kwa kuhoji kama ifuatavyo
Fikiria Kijiji kina shule mbili za msingi lakini bado shule zimezidiwa na wanafunzi. Hizi shule unakuta shule Ina hadi watoto mia Saba hadi mia tisa.
Mkuu mimi nadhani tatizo sio kwq.ba 2atoto ni wengi hapana,ila tatizo ni kwamba shule chache.

Kwa hiyo tukisema tusolve tatizo maana yake tuongeze shule,na sio tuache kuzaa kwa sababu kuzaa sio tatizo halisi.
Kama hali hii isipodhibitiwa na wizara ya afya basi huko mbeleni kazi ya serikali itakua kujenga madarasa na hospitals
Sasa unatakiwa ujue kwamba ni jukumu la serikali kuweka miundombinu sasa hivi ya madarasa na vituo vya afya kabla ya wakati wa mahitajio ya vitu kufika.

Tunatakiwa tutengeneze miundombinu kabla watumiaji hawajafika,na sio wameshafika ndio unaanza miundombinu.

Hao watoto unaowaona wengi mashuleni ni kwa sababu hawakuandaliwa miundombinu kabla hawajaja,tatizo sio watoto.
Australia nchi yenye maendeleo makubwa Ina watu ambao wahazidi million Saba
China nchi yenye maendeleo makubwa ina watu zaidi ya Bilioni moja pia.

Urusi nchi yenye maendeleo ina watu zaidi ya milioni 145(zaidi ya mara mbili ya idadi ya watz)

Uwingi wa watu sio kikwqzo cha maendeleo,bali usimamiaji na usambazaji wa rasilimali ndio tatizo kubwa,

so tutatue tatizo,tusitatue jambo ambalo sio tatizo,matatizo hayaishi kwa sababu tunatatua mambo ambayo sio tatizo kama umavyotaka kufanya mtoa mada.
 
Unataka tupunguze wapiga kura?
 
Mtz ukimwambia uzazi wa mpango ana sala kama mbogo huzani kwamba unamzuia asipige mashine😁
 
Wale watu hawazaliani kama uyoga na wako vizuri kiuchumi kuanzia family level.

Ktk kusoma kwangu enzi zangu sijawahi kukutana na rafiki anayetoma kanda hizo akaniambia kuwa kwao ni watoto saba au 10. Sana sana utasikia siai kwetu ni watoto 3 wakiwa wengi ni wa nne. Na kila mtoto amesoma vizuri au kaka au Dada ana nyazifa nzuri kielimu na kiuchumi.

Sisi akina kajamba nani ambao wazazi walikuqa kwenye ligi ya kuzaa hata boom tu la chuo ndilo lilikuwa linatumika kusomesha wadogo zetu na kutibia wengine wakiumwa huko vijijini.

Ukishindwa kupangilia Idadi ya familia kuoingana na uwezo wako basi umepanga kuwa maskini maiaha yako yoote.
 
Watoto wa Adamu walikuwa wangapi? Nuhu? Ibrahimu, Yakobo? vipi watoto wa Isaka? wewe ndio unaelewa sana bibilia kuliko Adamu aliyeambiwa uso kwa uso na Mungu?
 
Rasilimali lukuki na umaskink huu?? Unadhani kisa cha kulalamikia lita ta mafuta 3000 kinatokana na nini?
 
Mkuu serikali inalisha watoto wako?
 
Umesema kweli mkuu,shule nyingi za msingi maeneo ya machame hazina wanafunzi kabisa. Kuna moja darasa la saba walikuwa sita tu.
Unadhani ni kwa sababu wamezalina sana?? Fikiria Machame darasa moja wanafunzi 40. Ukerewe darasa moja wanafunzi 200.

Chagua mwenyewe kuishi kama kilaza au kama mwenye akili.
 
Unadhani ni kwa sababu wamezalina sana?? Fikiria Machame darasa moja wanafunzi 40. Ukerewe darasa moja wanafunzi 200.

Chagua mwenyewe kuishi kama kilaza au kama mwenye akili.
Sasa hivi vilaza wako vijijini na familia zao wanakula vyakula vya asili, wanamiliki rasilimali wakati "wenye" akili wako mtaani wanalialia na ukosefu wa ajira na upungufu wa nguvu za kiume.
 
Hakuna mtu anayasema watu wasizae, hapa jambo linalozungumziwa ni kupunguza idadi ya watoto watu wanaozaa.

Serikali haiwezi tu kuwa ina kazi ya kujenga shule kila siku, sasa hivi kuna shule zaidi ya moja karibia kila kata lakini bado halizitoshi, au unataka kuwepo na shule kila baada ya nyumba kumi? Bado maabara, vituo vya afya, hospitali, barabara, maji, umeme n.k Hospitali zetu kubwa ukifika zina msongamano wa hatari na zinakatisha tamaa kwa wagonjwa.

Tujizuie tuzae watoto wasiozidi wawili ili Tutengeneze kwanza miondombinu na huduma za msingi za kijamii ziwe nzuri kisha tutarudi kufyatua hata 10,Sera ya Uzazi wa mpango wa mtoto 1 ya China miaka ya 1980 hadi 2015 ilikuwa ni ya lazima na ilitekelezwa kikatili sana, sisi serikali sio lazima itumie nguvu na ukatili kuna sera nyingi mbadala inaweza kutumia kufanikisha hilo.

Russia ni nchi mojawapo yenye population ndogo sana, hao watu milioni 150 wanaishi kwenye eneo la km za mraba million 17.
 
Sasa hivi vilaza wako vijijini na familia zao wanakula vyakula vya asili, wanamiliki rasilimali wakati "wenye" akili wako mtaani wanalialia na ukosefu wa ajira na upungufu wa nguvu za kiume.
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜πŸ˜πŸ˜„πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜€
 
Unafahamu watoto wengi wa vijijini ndio wanaongoza kwa udumavu na kwashakoo??
Hizo stories zenu za maisha kijijini ni kama peponi huwa mnazitoa wapi? Nchi hii maisha ni magumu zaidi vijijini kuliko mijini na umaskini mkubwa uko vijijini zaidi.
Sasa hivi vilaza wako vijijini na familia zao wanakula vyakula vya asili, wanamiliki rasilimali wakati "wenye" akili wako mtaani wanalialia na ukosefu wa ajira na upungufu wa nguvu za kiume.
 
Na kulingana na hayo maandiko wakati huo dunia ilikuwa ni hiyo familia moja tu.
Watoto wa Adamu walikuwa wangapi? Nuhu? Ibrahimu, Yakobo? vipi watoto wa Isaka? wewe ndio unaelewa sana bibilia kuliko Adamu aliyeambiwa uso kwa uso na Mungu?
 
[emoji23]
Serikali na asasi za kiraia zinatakiwa zitoe elimu ya uzazi mpango na Serikali iwaondoe hofu watu wa aina hiyo, iwahakikishie wataendelea kupiga mashine vizuri tu.
Mtz ukimwambia uzazi wa mpango ana sala kama mbogo huzani kwamba unamzuia asipige mashine[emoji16]
 
[emoji23]
Serikali na asasi za kiraia zinatakiwa zitoe elimu ya uzazi mpango na Serikali iwaondoe hofu watu wa aina hiyo, iwahakikishie wataendelea kupiga mashine vizuri tu.
😁😁😁mtu maskini ni maskini hadi kwenye ubongo
 
Ninao wanne na bado natamani miaka irudi nyuma ili niongeze watoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…