Serikali itupie jicho mkata hotelini yanaposimama magari ya abiria kwa ajili ya chakula na" kuchimba dawa"

Serikali itupie jicho mkata hotelini yanaposimama magari ya abiria kwa ajili ya chakula na" kuchimba dawa"

Broxine

Member
Joined
Dec 23, 2016
Posts
29
Reaction score
20
Serikali ijikite kuangalia na kuchukua hatua kwa kituo cha mkata kwenye suala la Afya .Juzi wakati nasafiri kutokea Tanga tulisimama hapo kupata Chakula nilichukua takeaway wakati nipo kwenye gari nimeanza kula nikahisi nimekula Chakula kilicholala na kimechacha ilibidi nikitupe kwenye dustbin.Kwa mustakabali wa afya za watu hotel hii Inapaswa kukaguliwa mara kwa mara maana inapokea abiria wengi kwa siku.
 
Pole sana mgosi,afadhali hukula,ila niliwahi kula mishkaki pale ilikuwa mitamu balaa...
 
Vyakula vingi katika hizi hotelin sio salama kabisa,,

Kunywa maji kwa usalama wa afya yako
 
unatoka wilaya moja kwenda nyingine ndani ya mkoa mmoja hiyo njaa ya kula njiani unaipata wapi? Natoka mwanza hadi dar npiga maji na matunda tu nafika fresh
Mkuu kwani hiyo huduma ya chakula Ina tolewa bure?

huyu ni mteja kaona atoe kero ili kulinda afya za wengine, wewe una Anza masuala ya kuji zuia kula, wapi na wapi🤣😂
 
Serikali ijikite kuangalia na kuchukua hatua kwa kituo cha mkata kwenye suala la Afya .Juzi wakati nasafiri kutokea Tanga tulisimama hapo kupata Chakula nilichukua takeaway wakati nipo kwenye gari nimeanza kula nikahisi nimekula Chakula kilicholala na kimechacha ilibidi nikitupe kwenye dustbin.Kwa mustakabali wa afya za watu hotel hii Inapaswa kukaguliwa mara kwa mara maana inapokea abiria wengi kwa siku.
Ungemsikiliza Mshauri wa Rais mambo ya AFYA Prof. Janabi Hilo lisingekutokea.
 
Mwezi wa funga..hiyo itakuwa daku ilibaki.. acheni kula kula ovyo.. hii ni Ramadan/quadragesmal
 
unatoka wilaya moja kwenda nyingine ndani ya mkoa mmoja hiyo njaa ya kula njiani unaipata wapi? Natoka mwanza hadi dar npiga maji na matunda tu nafika fresh
Kwa nini unadhani kila mtu anapoanza safari anatokea nyumbani kama wewe? Kuna watu wanaunganisha safari, wengine walikuwa na shughuli mpaka muda wa safari, wengine ni wagonjwa, wengine wana watoto, wengine wametokea msibani, wengine wameondoka kwa ghafla... yaani kuna sababu nyingi mno zinazofanya watu watake kula wakiwa safarini. Njia sahihi ni serikali kuwajibika na kurudisha ule utaratibu wa mabasi kusimama kwenye stendi zenye hotel nyingi ili kuwe na ushindani na siyo sehemu moja ambayo wanafanya watakavyo.
 
Binafsi hizo Motel Huwa sijaribu kabisa Kula Misosi yake kwasababu huwa Ni Viporo tu and they dont care,
Motel Pekee ambayo huwa sivuki bila Kula ni Liverpool Mombo hapa Ni nyama pamoja na Mswolwa Morogoro road basi the rest ni bora niingie kwenye hotel ya Kawaida nile fresh food kuliko ivo viporo vya Motel
 
Mkuu kwani hiyo huduma ya chakula Ina tolewa bure?

huyu ni mteja kaona atoe kero ili kulinda afya za wengine, wewe una Anza masuala ya kuji zuia kula, wapi na wapi🤣😂
Ndiyo watanzania tulivyo. Tumezoea ''kuzunguka'' matatizo badala ya kuyaondoa. Ndiyo maana nchi imefika hapa ilipo. Hawa wanadhani kila mtu anayesafiri anakuwa kwenye situation kama zao. Kuna wengine wamelala msibani na hawajala siku kadhaa, kuna wengine wameunganisha magari, yaani dhararu ziko nyingi sana
 
Mwezi wa funga..hiyo itakuwa daku ilibaki.. acheni kula kula ovyo.. hii ni Ramadan/quadragesmal
Ilitosha useme kuwa chakula kilibaki kwa sababu katika mwezi huu mtukufu wateja ni wachache!.
Pamoja na kwamba sharia inaruhusu kula mchana anapokuwa safarini lakini waislamu wengi saa nyingine huona haya kula hadharani mchana wa ramadhani kwa khofu ya kutafsiriwa vibaya kwa wale wasiojua kuwa msafiri na mgonjwa wanaruhusiwa kula mchana wa Ramadhani.
 
Ila watu wa Tanga kwa Kula njiani, Kila kituo lazima wanunue Yai, half cake, soda. Yaani ni karaha.

Ila hili la hygiene litupiwe macho
Ushuzi wake hapo mpk macho ukifumbua yanauma kwa ukali wa ushuzi.
 
Ndiyo watanzania tulivyo. Tumezoea ''kuzunguka'' matatizo badala ya kuyaondoa. Ndiyo maana nchi imefika hapa ilipo. Hawa wanadhani kila mtu anayesafiri anakuwa kwenye situation kama zao. Kuna wengine wamelala msibani na hawajala siku kadhaa, kuna wengine wameunganisha magari, yaani dhararu ziko nyingi sana
binafsi naamini kula ni maamuzi ya mtu, hivyo asi ingiliwe ikiwa haleti madhara kwa wengine.

Mimi kusema ukweli huwa nakula haswa, na hufikia hata kuwa chukulia majirani zangu chakula.
 
Shida madereva na makonda wanapata chakura bure kwenye vituo wanavyo wapeleka
 
Back
Top Bottom