DOKEZO Serikali itusaidie wakazi wa Kigogo, fedha wanazotaka kutulipa kupisha mradi haziendani na nyumba zetu

DOKEZO Serikali itusaidie wakazi wa Kigogo, fedha wanazotaka kutulipa kupisha mradi haziendani na nyumba zetu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Habari, poleni na majukumu ya kazi wana JF na ahsanteni kwa habari nzuri na kutupasha Watanzania na wasio Watanzania.

Nimekuja kwenu tunaomba mtupazie sauti sisi ni wakazi wa Kigogo Mbuyuni, Dar es Salaam, toka upande wa Bonde la Msimbazi.

Huku kwetu kuna Mradi wa Bonde la Mto Msimbazi kwa hiyo kuna baadhi ya nyumba zinatakiwa kuvunjwa kupitisha huo mradi.

Kilio chetu ni kuhusu malipo yaliyotoka ni madogo sana kulingana na thamani ya nyumba zetu.

Kuna nyumba zaidi ya 450, kati ya hizo ambazo zimepangiwa kupata karibia Tsh. Milioni 50 hazifiki nyumba 5, nyingine nyingi ni chini ya hapo, mfano Tsh. Milioni 30, 20, 15 na nyingine hadi Milioni 4.

Mfano kuna vyumba ambazo vyoo waliofanya tathimini wanasema thamani ni Tsh. Laki nne, unaweza kujiuliza choo ambacho kuchimba tu gharama yake ni Ths. Laki mbili then mtu anakwambia thamani ya choo chote ni laki moja.

Siyo kwamba watu hatutaki kuhama lakini thamani ya nyumba zinazotakiwa kubomolewa na thamani ya fedha zinazolipwa ni ndogo, nyumba nyingi thamani iliyotajwa ni Tsh. Milioni 15, hapo ni zile ambazo zina sebule, vyumba vitatu au viwili.

Wanaofanya tathimini walipita hawakusema kuhusu masuala ya fedha, lakini wiki mbili zilizopita tulivyoenda kwenye mkutano mwanzoni mwa mwezi huu Machi 2023 ndio wakaanza kutuambia licha ya kuwa tathimin ilifanyika Mwaka 2022 au 2021 kama sijakosea.

Mbunge wetu Abbas Tarimba alikuja kwenye makazi yetu tukamlalamikia shida zetu na malalamiko yetu, akashauri kuwa tukubali kusaini tu wakati huo yeye anapeleka malalamiko hayo kwa uongozi wa juu Serikalini lakini tunajua hizo ni siasa na kutufanya tutulie.

Asilimia kubwa watu wengi wamesaini nyaraka za kuwa wapo tayari kupokea fedha kwa hofu kwa kuwa wanajua wanaweza kuacha kusaini na wakakosa vyote, nyumba na fedha.

Hivyo, wito wetu kwa Serikali iangalie inawezaje kutusaidia sisi wakati wa Kigogo kwa kuwa hatuna mpango wa kukataa kuhama ila thamani ya nyumba ndio changamoto.
 
Pana watu wanalia nyumba za mataa airport ya kwenda ulaya. Zipo nyumba watu binafsi walifika hadi bilioni moja wenye nyumba wakagoma kuuza,

Wamekuja lipwa fidia upanuzi wa barabara KWA ajili ya daraja la kuvuka reli na pia mradi wa mabus ya mwendokasi Chanika posta hakuna aliyepata hata m 150.

Pana mzee aligoma m400 kajalipwa m80, Pana tajiri alifika m 900 mzee anataka afike b moja akaja ambulia m120.

Tathmini ya serikali na mtu binafsi ni tofauti. Mtu binafsi akifika ana pesa nzuri kukuhamisha usijiulize mara mbili mbili, kamata pesa.
 
Kwanini maeneo ya Mchikichini ilala, Sunna Magomeni na Hananasif Kinondoni jijini Dar es Salaam yasitumike kujenga makaazi mapya kwa watakaohamishwa toka bonde la mto Msimbazi jijini Dar es Salaam badala ya kuwalipa fidia ndogo wananchi serikali ibebe jukumu kuwajengea makaazi yaliyopangwa eneo la Mchikichini Sunna na Hananasif

ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI 2020 - 2025:

(c)
Kuboresha maeneo hatarishi ikiwemo bonde la mto Msimbazi jijini Dar
es Salaam ili kudhibiti mafuriko, kuhifadhi mazingira na kuyafanya
kuwa vivutio kwa watalii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali;
(d) Kuimarisha utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Kurasimisha Makazi
yasiyo rasmi katika mikoa 26 nchini ikiwa ni pamoja na kuwezesha
ujenzi wa miji ya kisasa na kupunguza makazi yasiyo rasmi kwa
kuandaa Mipango Kabambe 6 ya miji ya Mpanda, Njombe, Mererani,
Chato, Ifakara na Kahama; na
(e) Kusimamia na kuratibu upangaji upya maeneo yaliyochakaa (re-
development) katika miji mbalimbali nchini.
Nyumba na Makazi
75. Chama Cha Mapinduzi kinatambua kuwa nyumba ni rasilimali ya msingi
na hitaji muhimu kwa maisha ya binadamu. Katika kusimamia hilo, kwa kipindi cha mwaka (2015 - 2020), Chama kimeisimamia Serikali kutoa
huduma stahiki ya makazi bora na kupata mafanikio yafuatayo:-
(a) Kuendeleza uwezeshaji wa watumishi kwa kuwapatia mikopo ya....

TOKA MAKTABA :
29 April 2021
MASWALI BUNGENI
Dodoma, Tanzania

Mheshimiwa TARIMBA G. ABBAS Aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza kazi ya ujenzi wa mradi wa Mto Msimbazi ambao umetajwa katika Bajeti ya mwaka 2021/2022?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) Alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tarimba Gulam Abbas Mbunge wa Jimbo la kinondoni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali na Benki ya Dunia inatarajia kufanya majadiliano ya mapendekezo ya awali ya mradi mwezi Desemba 2021 na kusaini mkataba wa mkopo wa kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 120 ifikapo mwezi Machi 2022 na utekelezaji wa mradi unatarajiwa kuanza mwezi Julai, 2022 baada ya kukamilisha masharti yote ya kutekeleza mradi.

Mheshimiwa Spika, huu ni mradi wa kukabiliana na mafuriko katika bonde la Mto Msimbazi. Mradi huo kwa sasa upo katika hatua za maandalizi ambapo usanifu wa miundombinu husika pamoja na nyaraka muhimu kwa ajili ya masuala ya mazingira na fidia zinaandaliwa.

Mheshimiwa Spika, Kimsingi mradi huu utahusisha pia ujenzi wa daraja jipya la Jangwani lenye urefu wa mita 390; Upanuzi wa mto kwa upande wa chini kuanzia barabara ya Kawawa hadi daraja la Salander ili kuruhusu maji ya mvua kwenda baharini kwa haraka;

Mheshimiwa Spika, Uimarishaji wa kingo za mto msimbazi katika maeneo korofi kwa upande wa juu katika maeneo ya Tabata na Kinyerezi ili kuzuia mmomonyoko wa udongo;

Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa vitega mchanga na vituo vya kuhudumia mto kwa ajili ya kupunguza kiwango cha mchanga kinachotuama eneo la chini la Mto Msimbazi;

Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa matuta kwa upande wa chini wa mto Msimbazi (kuanzia Daraja la Selander hadi Barabara ya Kawawa) yatakayoruhusu matumizi mbalimbali ya ardhi ikiwemo City Park eneo la Jangwani pamoja na maendeleo ya makazi maeneo ya Mchikichini, Sunna na Hananasif; Program za kuboresha usimamizi wa takangumu katika Kata 18 zinazozunguka bonde la Mto Msimbazi; na Kurudishia uoto wa asili katika maeneo yenye mikoko, maeneo yenye ardhi oevu, pamoja na misitu ya Pugu na Kazimzumbu, Wilayani Kisarawe.

MHE. TARIMBA G. ABBAS aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Mto Msimbazi ambao umeainishwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020 – 2025?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira; kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Tarimba Gulam Abbas Mbunge Jimbo la Kinondoni naomba kutoa maelezo yafuatayo kuhusu Mto Msimbazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inatekeleza mradi wa kuendeleza Jiji la Dar es Salaam (Dar es Salaam Metropolitan Development Project) kwa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 300 kutoka Benki ya Dunia.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza DFID, inatekeleza programu ya Tanzania Urban Resilience Programme ambayo imelenga kuzisaidia halmashauri na Serikali Kuu katika kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi. Kwa kuanzia, programu itaanza kutatua changamoto zinazolikabili Bonde la Mto Msimbazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari DFID imeshatenga kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 20 kwa ajili ya Bonde la Mto Msimbazi. Pia Benki ya Dunia, kupitia mradi wa DMDP, imekubali mkopo wa nyongeza wa kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 100 kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za Bonde la Mto Msimbazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira naomba sasa kujibu swali la Mheshimiwa Abbas Tarimba Gulam Mbunge wa Kinondoni:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imepanga kubadili eneo la bonde la Mto Msimbazi kuwa eneo la uwekezaji na fursa mbalimbali. Ili kufikia azma hiyo, usanifu wa mradi huo umekamilika. Utekelezaji wa mradi utaanza baada ya kupata idhini ya Serikali kuhusu matumizi ya fedha hizo za mkopo kupitia Wizara ya Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, ili kupunguza athari za mafuriko kwa sasa, kipande cha Mto Msimbazi cha daraja la Jangwani kinafanyiwa usafi wa mara kwa mara na wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Source : Bunge Polis

habarileo.co.tz
https://habarileo.co.tz › benki-ya-du...
Benki ya Dunia yatoa mabilioni Dar

6 Oct 2022 — BENKI ya Dunia imetoa mkopo wa Dola za Marekani milioni 200 (Sh bilioni 466.387) kugharamia mradi wa Bonde la Msimbazi ili kuepuka mafuriko ...
 
Pana watu wanalia nyumba za mataa airport ya kwenda ulaya. Zipo nyumba watu binafsi walifika hadi bilioni moja wenye nyumba wakagoma kuuza,

Wamekuja lipwa fidia upanuzi wa barabara KWA ajili ya daraja la kuvuka reli na pia mradi wa mabus ya mwendokasi Chanika posta hakuna aliyepata hata m 150.

Pana mzee aligoma m400 kajalipwa m80, Pana tajiri alifika m 900 mzee anataka afike b moja akaja ambulia m120.

Tathmini ya serikali na mtu binafsi ni tofauti. Mtu binafsi akifika ana pesa nzuri kukuhamisha usijiulize mara mbili mbili, kamata pesa.
Dah kwa hii serikali yetu hii [emoji3]
 
Mimi nawashauri msigomee hayo malipo yapokeeni kwanza kisha ndio mfungue kesi ya mapunjo.. Mkichelewa hata hicho kidogo mtakikosa na nyumba zitavunjwa
Ushauri mzuri. Ukiangalia maeneo hayo mengi utakuta hayako au hayakuwepo kwenye mipango miji..wakiendelea kubisha wataambiwa waipatie serikali kibali cha ujenzi kama waliwahi kuruhisiwa kujenga.
 
Nawashauri pokeeni hela ukatafute maisha kwingine kwamaana huna permit ya ujenzi wa serikali umejenga holela huna haki kisheria hapo unatumika ungwana pokea alafu fungua kesi ya mapunjwa
 
1. Notisi ya kutanga eneo la bonde la mto msimbazi kuwa eneo hatarishi (hazardous area) ilitoka mwaka 1979; wakati huo hakukuwa na nyumba hata moja;

2. Watu wakaanza kuvamia hilo eneo na kujenga nyumba miaka ya 90;

3. Kisheria, mtu yeyote hastaili kupata fidia yoyote pale anapojenga bila kibali cha ujenzi au ambae amejenga kwenye maeneo hatarishi, maeneo ya wazi au yaliyopangwa matumizi mengine tofauti na makazi.

4. Hivyo Serikali ikihamua inaweza kuwatoa wakazi wote wa bonde la mto msimbazi bila fidia yoyote na kimsingi serikali ndio inatakiwa kuwashtaki wakazi hao kwa kusababisha uharibifu wa njia za maji;

5. Mwisho, mkopo uliotolewa na Benki ya Dunia kuendeleza eneo la bonde haina kipengere za fidia.
 
Habari, poleni na majukumu ya kazi wana JF na ahsanteni kwa habari nzuri na kutupasha Watanzania na wasio Watanzania.

Nimekuja kwenu tunaomba mtupazie sauti sisi ni wakazi wa Kigogo Mbuyuni, Dar es Salaam, toka upande wa Bonde la Msimbazi.

Huku kwetu kuna Mradi wa Bonde la Mto Msimbazi kwa hiyo kuna baadhi ya nyumba zinatakiwa kuvunjwa kupitisha huo mradi.

Kilio chetu ni kuhusu malipo yaliyotoka ni madogo sana kulingana na thamani ya nyumba zetu.

Kuna nyumba zaidi ya 450, kati ya hizo ambazo zimepangiwa kupata karibia Tsh. Milioni 50 hazifiki nyumba 5, nyingine nyingi ni chini ya hapo, mfano Tsh. Milioni 30, 20, 15 na nyingine hadi Milioni 4.

Mfano kuna vyumba ambazo vyoo waliofanya tathimini wanasema thamani ni Tsh. Laki nne, unaweza kujiuliza choo ambacho kuchimba tu gharama yake ni Ths. Laki mbili then mtu anakwambia thamani ya choo chote ni laki moja.

Siyo kwamba watu hatutaki kuhama lakini thamani ya nyumba zinazotakiwa kubomolewa na thamani ya fedha zinazolipwa ni ndogo, nyumba nyingi thamani iliyotajwa ni Tsh. Milioni 15, hapo ni zile ambazo zina sebule, vyumba vitatu au viwili.

Wanaofanya tathimini walipita hawakusema kuhusu masuala ya fedha, lakini wiki mbili zilizopita tulivyoenda kwenye mkutano mwanzoni mwa mwezi huu Machi 2023 ndio wakaanza kutuambia licha ya kuwa tathimin ilifanyika Mwaka 2022 au 2021 kama sijakosea.

Mbunge wetu Abbas Tarimba alikuja kwenye makazi yetu tukamlalamikia shida zetu na malalamiko yetu, akashauri kuwa tukubali kusaini tu wakati huo yeye anapeleka malalamiko hayo kwa uongozi wa juu Serikalini lakini tunajua hizo ni siasa na kutufanya tutulie.

Asilimia kubwa watu wengi wamesaini nyaraka za kuwa wapo tayari kupokea fedha kwa hofu kwa kuwa wanajua wanaweza kuacha kusaini na wakakosa vyote, nyumba na fedha.

Hivyo, wito wetu kwa Serikali iangalie inawezaje kutusaidia sisi wakati wa Kigogo kwa kuwa hatuna mpango wa kukataa kuhama ila thamani ya nyumba ndio changamoto.
Serikali ipi ambayo mnatarajia iwasaidie 🤣🤣🤣??? Hii hii ya kila mbuzi kwa urefu wa kamba yake au kuna nyingine ambayo mnaizungumzia?

Na mkifanya masihara mtaswagwa na kipigo kabisa na hamna mamlaka itakayozungumza lolote 😀 waulizeni wamasai wa Serengeti wana ujumbe kamili.
 
A senseless government, siyo?
 
Back
Top Bottom