Serikali iwajibike kwa Ajali za barabarani zinazomaliza watanzania

Serikali iwajibike kwa Ajali za barabarani zinazomaliza watanzania

Shida ya Traffic nao wengi ni wala rushwa za kulazimisha,ili wafikie malengo ya makusanyo ya Mapato.Kwenye Hili naunga Mkono hoja ya Kinana,hawa wapigwe chini wabaki wachache hawana msaada kama wanavyodai
 
Madereva ni SAwa na mbuzi bila kuchungwa RIP zitakuwa wimbo wa KILA siku
 
Matukio ya ajali za barabarani yanaonekana kushamiri maeneo mbalimbali nchini huku watanzania wenzetu wasio na hatia wakipoteza maisha na wengine kubaki na ulemavu wa kudumu.

Hivi ni kweli amekosekana mtu wa kuwajibika kwenye hili la ajali za barabarani?
  • MTWARA watoto wa shule wameoteza maisha
  • Shinyanga
  • Simiyu
  • Morogoro
  • Mbeya
Na maeneo mengine nchini kila siku watanzania wenzetu wanapoteza maisha tatizo liko wapi?
Hayo ni makafara ya CCM kuendelea kubaki madarakani
 
Ulevi Barabara nzima imejaa Viduka vinavyouza Pombe Madereva wanajua fika wakikutana na Trafiki polisi atawaambia washa taa piga wiper hakuna kipimo cha kutesti pombe.
Kweli kabisa ! Sasa waanze kuwapima ! Ajali zitapungua sana !!
 
KWENYE HIZI AJALI NIT WANAYO KAZI (ROLE) YA KUFANYA KUSAIDIA KUZIPUNGUZA KUPITIA MAFUNZO WANAYOTOA

Sote tunafahamu kuwa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (National Institute of transport) yaani NIT, ndicho tunaweza kusema Chuo Kikuu pekee cha Madereva nchini Tanzania ambacho kinafundisha wataalamu katika Nyanja ya Usafiri na Mawasiliano katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. Ni kwa kutambua umuhimu huu, Serikali ikakipa mamlaka Chuo hiki kufundisha madereva wanaotaka kuendesha mabasi ya abiria(PSV) na hata yale ya mizigo, hata hivyo kimekuwa maarufu sana kwa kufundisha madereva wetu.

Bila shaka kabisa ubora wa bidhaa inayotolewa na Chuo hiki lazima itafsirike sio tu kwenye matokeo ya mitihani bali pia matokeo ya kivitendo barabarani. Iwapo tafiti zetu kwa mfano zitasema, ajali nyingi zinatokea barabarani kutokana na makosa ya dereva ambapo inahusisha upungufu wa mafunzo au ujuzi duni basi, bila shaka NIT watahusika kabisaa pamoja na wale watahini wa Polisi (Driver examiners) ambao wao ndio wenye kazi ya kumuaminisha TRA kwamba huyu mwombaji wa Leseni Pingilinene Mfupi, ana sifa na ujuzi unaotakiwa kuendesha gari katika mazingira yote barabarani, hivyo apewe daraja C.

Chuo chetu cha NIT, kwa namna yoyote ile kinahusika katika kuhakikisha usalama barabarani unaimarika. Hakiwezi kujitoa kamwe kwa kusema tu, chenyewe kazi yake ni kufundisha tu, lazima kiende mbele kuhakikisha inatoa mchango katika kupunguza janga la ajali nchini. Kwa nini? Kwa sababu:
1. Chenyewe ndicho kinachofundisha madereva wanaoenda kuendesha magari ya abiria
2. Chenyewe ndicho kinawafundisha wakaguzi wa magari ambao baadae ndio wanakuwa watahini wa madereva (driver examiners) kule Polisi na pia wakaguzi wa magari (vehicle inspectors).

Ina maana Chuo hiki kikimtoa mkaguzi wa magari ambaye hajaiva vizuri, tafsiri yake ni kwamba huyo mkaguzi wa magari anaenda kuruhusu magari mabovu yaendeshwe barabarani, lakini sio hivyo tu, bali pia anaenda kuruhusu madereva wasio na sifa kuingia barabarani. Kwani, kwa mujibu wa sheria, TRA hawezi kumpa mtu leseni kama Mtahini wa madereva hajasema huyu mpe huyu usimpe. Ndio kusema kwamba Polisi wanapolalamika “madereva wa siku hizi wabovu kweli kweli, kimsingi wanakuwa wanajisema wenyewe kwamba sisi tunaowapitisha siku hizi na sisi ni wabovu kweli kweli.

SASA kwa upande wa NIT, mchango wao kwenye kuzuia ajali au kupunguza vifo na majeruhi ukoje? Maswali yafuatayo, yanalenga kuibua mjadala au kufikirisha tu jinsi ambavyo NIT wanaweza kuwa na nafasi katika kuzuia ajali:
1. Je, kwenye hizi ajali zinazotokea wenzetu NIT wanajifunza nini? Je huwa wanaenda kufanya tafiti kuhusu hivi vyanzo na kuona ni namna gani matokeo ya tafiti hizo yatasaidia kuwanoa madereva? Je, wanatumia picha na video za ajali hizo kama mifano ya kufundishia?

2. Je, wenzetu NIT wana jitihada zozote za kuhakikisha wanapata taarifa na kusoma kwa kina aina zote za mabasi au malori yanayoletwa nchini na taratibu za uendeshaji wake, ili dereva anayepita pale kwa kozi ya PSV au HGV aweze sio tu kujua Scania 9XYZ bali ajue pia Zhongtong au Asia Star bus yenye engine ya PXW inaendeshwaje?

3. Je, NIT wamejaribu kutengeneza taratibu mbalimbali za msingi (standard operating procedures) za ukaguzi magari kabla hayajaondoka (pre-departure inspection procedures) ili kuwasaidia madereva au wamiliki kuzitumia, au taratibu mbalimbali za uendeshaji wa magari katika mazingira tofauti tofauti? Mfano, katika mazingira Fulani dereva aendeshaje? Ikipasuka tairi afanyeje nk? Maana vitu vingine tunaambizana mtaani tu.

4. Lakini je, NIT wanafanya tafiti kujua ubora wa madereva wao baada ya kuwa wamehitimu pale? Kwa kufuatilia takwimu za ajali kwa mfano na kufahamu, je madereva wangapi waliopita mikononi mwao walipata ajali na ni ajali za namna gani kwa mwaka au kipindi cha miaka mitatu. ili kusudi wajue wanaboresha nini katika mitaala yao? Na kama zipo je ni nani mlaji wa taarifa hizo? Zinachapishwa wapi? Kama ni kwenye machapisho ya kingereza je, zinatusaidia vipi sisi walaji ambao ni wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili? Maana nchini hapa wengi waliojaliwa hela hawakufanikiwa kwenda vidato sana. Na hata idadi kubwa ya madereva wetu ni shule ya msingi na sekondari zetu za kawaida tu.

5. Je, ni kwa kiasi gani NIT wanatumia uzoefu wa madereva wakongwe katika kufundisha madereva pale ili kupata uzoefu wa barabarani kila siku? Kwa maana ya kuoanisha nadharia na vitendo au uhalisia ulioko barabarani? Je, kwenye kozi za PSV kule NIT madereva wanafundishwa uendeshaji wa usiku? Au wale walimu wao wenyewe washaendesha magari usiku au katika hali tofauti tofauti za hewa na miundo ya barabara?

6. Lakini pia Serikali inakitumiaje Chuo hiki katika kuvikuza na kuvisimamia vyuo vingine vidogo vinavyofundisha udereva wa awali ili kuhakikisha ubora wa madereva hao, ili hata baada ya miaka 3 wakifika huko NIT isiwe kwamba ndio kama wanaanza kujifunza na moja? Labda kwenye hili pia kuna kazi ya kufanya.

7. Je, NIT wanafundisha somo la usalama barabarani au ni ule udereva tu wa kujua kulimudu gari na alama za barabarani? Kwa msingi huo, madereva wetu wanajua dhana nzima ya road safety?

Ndugu zangu, kwa leo tuishie hapa tu kwa haya maswali fikirishi yenye kulenga kuibua mjadala. Karibu wale mliopita katika chuo hicho lakini pia NIT wenyewe tulionao humu.

C&P
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote
17/08/2022
Aliyeandika hili andishi anastahili kuwa mjumbe wa tume ya kuchunguza vyanzo vya ajali na mwarobaini wake.
Kongole sana kwake.
 
Matukio ya ajali za barabarani yanaonekana kushamiri maeneo mbalimbali nchini huku watanzania wenzetu wasio na hatia wakipoteza maisha na wengine kubaki na ulemavu wa kudumu.

Hivi ni kweli amekosekana mtu wa kuwajibika kwenye hili la ajali za barabarani?
  • MTWARA watoto wa shule wameoteza maisha
  • Shinyanga
  • Simiyu
  • Morogoro
  • Mbeya
Na maeneo mengine nchini kila siku watanzania wenzetu wanapoteza maisha tatizo liko wapi?

Na mida hii saa moja iliyopita ajali mbaya imetokea Manyoni kwa basi la Tanzanite lililokuwa kinatika Mwanza kwenda Dar.
 
Ajali hata Ulaya na Marekani zinatokea nyingi ni Pombe sasa wenzetu wana kipimo cha Pombe na Dereva akikamatwa ni Mahakamani vinauzwa Ebay sisi kama Taifa tunashindwa kununua mpaka tuletewe msaada?

Na hata Samia akituma maafsa wake wakamletee bei itakuwa mara 2000 ya Ebay 😂 sisi Wabongo sijui hii laana tulipigwa na nani.
 
Asilimia kubwa ya madereva bongo bi wendawazimu tu
Na huwa nasemaga wabongo wanakufa kizembe sana kila siku

Ova
 
Gari la abiria linatoka kituo A saa 12asubuhi, linafika kituo B saa 12 jion, kesho yake linatakiwa kuondoka kituo B saa 12 asubuhi kwenda kituo A.. Sasa nambieni gari hili linafanyiwa checkup sa ngapi?
 
Sasa ndugu yangu gari limeferi break Nani anawajibika hapo?

Utaonea watu tu
Mara zote gari kufeli breki ni makosa ya dereva ambaye hayuko makini
Aliyeandika hili andishi anastahili kuwa mjumbe wa tume ya kuchunguza vyanzo vya ajali na mwarobaini wake.
Kongole sana kwake.
Ni kweli lakini pia vile vichupa vidogo vidogo vya mvinyo badala ya viroba vimejaa njia nzima kwenye viosk na madukani ! Je hao NIT wanahusikaje hapo ??
 
Gari la abiria linatoka kituo A saa 12asubuhi, linafika kituo B saa 12 jion, kesho yake linatakiwa kuondoka kituo B saa 12 asubuhi kwenda kituo A.. Sasa nambieni gari hili linafanyiwa checkup sa ngapi?
Fanya checkup zako halafu mlevi anakuletea ajali, Matrafiki wanapewa za kubrashia viatu miezi sita wewe wakati huo umefukiwa ardhini unapambana na wadudu.

Mola atunusuru.
 
Matukio ya ajali za barabarani yanaonekana kushamiri maeneo mbalimbali nchini huku watanzania wenzetu wasio na hatia wakipoteza maisha na wengine kubaki na ulemavu wa kudumu.

Hivi ni kweli amekosekana mtu wa kuwajibika kwenye hili la ajali za barabarani?
  • MTWARA watoto wa shule wameoteza maisha
  • Shinyanga
  • Simiyu
  • Morogoro
  • Mbeya
Na maeneo mengine nchini kila siku watanzania wenzetu wanapoteza maisha tatizo liko wapi?
Saivi wajanja wa mjini wamekalia Tanzania wale washamba na malimbukeni wachunga ng'ombe wamepumzika. Na vibaka wamerudi Kama kawa na silaha zitaonekana mtaani jamani kila mtu na kamba yake.
Mie nipewe 20M niuze ama nikodishe ama silaha Ni kwa Nini nisile nilipofungwa? Nyie endeleeni kucheza ngoma Mana tumewapunguza mlitaka kujaazana huku ikulu jamani ngoja wajanja wa mjini wazoefu wa kula maisha kiulaini tuzidi kula. Na hizo Kodi zenu ndio nyie mnafanya kazi sie tunajichotea tu.
 
Shida ya Traffic nao wengi ni wala rushwa za kulazimisha,ili wafikie malengo ya makusanyo ya Mapato.Kwenye Hili naunga Mkono hoja ya Kinana,hawa wapigwe chini wabaki wachache hawana msaada kama wanavyodai
wamepunguzwa au huna taatifa??

siku hizi kero za rushwa zimepungua watu wanakulana vichwa wenyewe.
 
Haya yanawezakana kwa Jamii iliyo civilized.Nje ya hapo sheria ni fursa kwa wasimamizi wa Sheria.
Speed gavana ni ngumu ilifeli hii,mafundi walicheza na adjustment ya pedal ya accelerator. Bora wajaze askari barabarani KILA baada ya kilometa Ili ukijifanya kichwa ngumu unazo pesa tuone kama utaweza honga wote toka dar hadi mwanza na hata ukihonga jumla pesa yote bora upande ndege.
Trafiki wapewe vipimo vya ulevi kila mahali walipo !! Wafanye majaribio kwa miezi sita uone kama ajali zitatokea !!
 
Matukio ya ajali za barabarani yanaonekana kushamiri maeneo mbalimbali nchini huku watanzania wenzetu wasio na hatia wakipoteza maisha na wengine kubaki na ulemavu wa kudumu.

Hivi ni kweli amekosekana mtu wa kuwajibika kwenye hili la ajali za barabarani?
  • MTWARA watoto wa shule wameoteza maisha
  • Shinyanga
  • Simiyu
  • Morogoro
  • Mbeya
Na maeneo mengine nchini kila siku watanzania wenzetu wanapoteza maisha tatizo liko wapi?
RUSHWA na SIASA laghai kwenye maisha ya watu ndio matokeo ya maafa yanayoendelea kutokea Tanzania yakiangamiza uhai wa wananchi wasio na hatia.
 
  • Wanaokufa ni watolewa kafara, watoa kafara wanagonga mvinyo kushangilia mauzo na faida kuongezeka.
  • Wao wanaagiza na kutumia magari yenye usalama 100% , mwenye inji aliwahi sema si rushwa, ni hela ya kubrashia viatu. WHO CARES?
  • Mungu alimuuliza Kaini, kwa nini damu ya nduguyo inanililia ardhini? Tafakari, chukua hatua
 
Back
Top Bottom