Serikali iwajibike kwa Ajali za barabarani zinazomaliza watanzania

Serikali iwajibike kwa Ajali za barabarani zinazomaliza watanzania

We poti jibidiishe hapo line police lima hata mchicha huwezi kurudishwa barabarani kuja kula rushwa, mTachonga sana😂😂😂
 
Utaratibu wa kudhibiti ajali unahusisha mambo mengi, si sehemu zote askari wa barabarani watakuwepo kudhibiti mwendo au uzingativu wa sheria za usalama barabarani...

1. Umadhubuti wa vyombo vya moto - Hapa hakuna mandatory service kwa magari

2. Umakini wa madereva - Hapa inahusiana na dereva mwenye mafunzo, watu wengi wana leseni na hawana mafunzo

3. Utimamu wa afya ya akili na mwili - Watu wangapi wana shida ya macho na bado wanaendesha magari, watu wangapi wana shida ya magonjwa ya akili na wangali wanaendesha magari?

4. Uchakavu wa Miundombinu ya barabara - Kuna barabara ni chakavu zina mabondebonde naa mashimo shimo ikiwemo hiyo barabara ya Igawa - Mbeya, haswa hayo maeneo ya Inyala ambapo ajali imetokezea majuzi

5. Uhaba wa barabara - Barabara tulizonazo zinachangia ajali kwa sababu ni katika lane hiyo hiyo magari ya kwenda na kurudi hutumia na kinachotenganisha ni mstari wa kuchorwa tu.
Serikali iendelee kuboresha kwa kujenga walau njia moja kwenda na njia nyingine kurudi zilizotenganishwa na eneo pana katikati kama zionekanavyo njia za mjini haswa Dar
 
Unapaswa kushika zamu. Kuombea nchi waombaji ni wachache sana na wengi wa waombaji ni wanung’unikaji sasa relax ajali zote ni za shetani ni juhudi zako binafsi kuomba kwa ajir ya safar na utokapo na kuombea wengine huo ndo upendo.

Mimi nimuhanga wa Ajari mbaya kabisa. Baada ya hapo nilijua Siri nyingi sana baada ya hapo nikaenda kwa Mganga nikaambiwa adui yangu ni Shangazi yangu, lakini nikakutana na Mtumishi wa Mungu ambaye sijawah kumuona na simjui huku nauguza mkono usiopona kwa kuvunjika vibaya tukaomba na mifupa ya Mkono wangu ikaunga na adui yangu akawa Shangazi yangu yule yule.

Na shangazi yangu ni mtaalamu mtaa wote wanamgwaya. Nikachagua nipate ulinzi wa Mungu nikatulia nalikuwa Roma yaan Rc nikaomba Mungu anipe njia nikapata. Kumbe Roho wa Mungu anakusemesha ukiomba unapata. Nikahama Rc nikaanza kupambana kwa msaada wake Mungu Ndipo kweli nlipowaona adui zangu na NDIPO NILIPOGUNDUA ADUI YANGU SIO SHANGAZI YANGU BALI NI ROHO CHAFU NDANI YAKE KWA MAANA YA SHETANI(ndo maana wachawi wanadumu hawafi mapema Mungu anawaacha ili akufundishe kumtegemea Mungu) ni mimi sasa ninae funga nguvu za uchawi zake zisifate familia yangu nakata mikono yake kiroho hana nguvu tena ila ni mchawi.

Nachotaka kusema usipokuwa na ulinzi wa Mungu basi unaulinzi wa shetani mda wowote shetani anaamua kukuchinja tu maana ndie anaekulinda hivo ana maamuzi. Kama kuku tu na mwenye kuku.

Ombea taifa, ombea vijana ila kabla acha kutenda dhambi shika Amri,sheria,hukumu na maagizo ya Mungu Nehemia 1:7 laa subir kuchinjwa.

Haiwezekani usiijue kesho yako. Ni lazima uijue sbb leo umeiombea hiyo kesho. Wengi tunaishi leo tunakosea.

Ndo maana mtoa mada analialia unakosea usiyatafakar ya Nyuma tafuta chanzo then chukua hatua
 
Utaratibu wa kudhibiti ajali unahusisha mambo mengi, si sehemu zote askari wa barabarani watakuwepo kudhibiti mwendo au uzingativu wa sheria za usalama barabarani...

1. Umadhubuti wa vyombo vya moto - Hapa hakuna mandatory service kwa magari

2. Umakini wa madereva - Hapa inahusiana na dereva mwenye mafunzo, watu wengi wana leseni na hawana mafunzo

3. Utimamu wa afya ya akili na mwili - Watu wangapi wana shida ya macho na bado wanaendesha magari, watu wangapi wana shida ya magonjwa ya akili na wangali wanaendesha magari?

4. Uchakavu wa Miundombinu ya barabara - Kuna barabara ni chakavu zina mabondebonde naa mashimo shimo ikiwemo hiyo barabara ya Igawa - Mbeya, haswa hayo maeneo ya Inyala ambapo ajali imetokezea majuzi

5. Uhaba wa barabara - Barabara tulizonazo zinachangia ajali kwa sababu ni katika lane hiyo hiyo magari ya kwenda na kurudi hutumia na kinachotenganisha ni mstari wa kuchorwa tu.
Serikali iendelee kuboresha kwa kujenga walau njia moja kwenda na njia nyingine kurudi zilizotenganishwa na eneo pana katikati kama zionekanavyo njia za mjini haswa Dar
Kwanini matumizi ya teknolojia hayaonekani kuwa moja ya suluhisho la kudhihibiti ajali?
Kwanini askari wanang'ang'aniwa sana wawepo barabarani tena makundi kwa makundi?
Kwanini miaka nenda rudi hakuna vitendo ila maneno meeengi kwenye TV na redio?
 
Haiwezekani!
No. 1 ndiye mwenye mamlaka kama raia namba moja ktk nchi.

Ni muda muafaka sasa awajibike yeye. Too much.

Tumechokaa. Kama taifa limeingia maagano ya damu/ kishetani mtuambie.
Waziri angekuwa Mkristo angeshatolewa sahivi ni dini pendwa
 
Masauni hakuna anachokifanya hapo
Hao askari hata iweje hawawezi kudhibiti ajalli, kumbuka kuna wiki ya usalama barabarani still ajali zinatokea huku magari yakikaguliwa kila baada ya 1Km, ajali nyingi ukichunguza ni zinahusisha ubovu wa magari hayohayo wanayokagua kila siku.

Ukizungumzia sheria, wavunja sheria namba moja ni madereva wa magari ya serikali na mabasi au malori ya viongozi serikalini huku magari ya wengine yakiombwa rushwa na askari njiani, mjumuisho wa haya yote ndiyo hizo ajali
 
Kwanini matumizi ya teknolojia hayaonekani kuwa moja ya suluhisho la kudhihibiti ajali?
Kwanini askari wanang'ang'aniwa sana wawepo barabarani tena makundi kwa makundi?
Kwanini miaka nenda rudi hakuna vitendo ila maneno meeengi kwenye TV na redio?

Ni sahihi kuhusisha teknolojia, lakini kwa mtazamo wangu teknolojia inatibu chanzo kimoja tu cha Uzembe wa dereva, wakati kuna vyanzo vingine vingi...
 
Hao askari hata iweje hawawezi kudhibiti ajalli, kumbuka kuna wiki ya usalama barabarani still ajali zinatokea huku magari yakikaguliwa kila baada ya 1Km, ajali nyingi ukichunguza ni zinahusisha ubovu wa magari hayohayo wanayokagua kila siku.

Ukizungumzia sheria, wavunja sheria namba moja ni madereva wa magari ya serikali na mabasi au malori ya viongozi serikalini huku magari ya wengine yakiombwa rushwa na askari njiani, mjumuisho wa haya yote ndiyo hizo ajali
Tatizo rushwa inasababisha haya yote
 
Nani amefanya tafiti na kuja na gunduzi hiyo ya kuwa vyanzo vingi vya ajali ni "vichupa vidogo vidogo vya mvinyo"!!??

Mimi nimeandika kuonyesha umuhimu wa mwenye andiko kuwa mjumbe wa tume ya kuchunguza vyanzo vya ajali iwapo itaundwa.
Kabla ya hiyo tume kuundwa matrafik wapewe vipimo vingi vya kupimia ulevi viwepo kila mahali walipo wao !!
 
Baadala ya kupunguza polisi wa usalama barabarani btungeongeza!
Angalau Kila km 1 kuwe na polisi hii itasaidia hasa kupunguza mwendo kasi,
Kingine kudhibiti na kuondoa magari mabovu,
Kutanua, na KUJENGA miundo mbinu Bora ya barabara.
Kukarabati au kuzitanua Kwa muda zile sehehu korofi mfano Ile ya Mbeya
Na nyinginezo,
 
Dereva anayeendesha ndie mwenye dhamana ya kubeba usalama wa abiria wake na yeye mwenyewe.HAKUNA MWINGINE.
Yeye ndo anajua wapi apunguze nwendo,wapi aongeze,wapi afunge breki,wapi aovertake n.k.
Sio serikali.
 
Kama umewahi kuendesha gari uwez kusema kufeli break ni kosa la dereva Kwa kukosa umakaini

So anakosa umakini mpaka na yy anakufa
Dereva ni lazima uhakikishe gari unaloliendesha liko katika hali nzuri siku zote unapoliendesha, either kufeli kwa breki kutasababishwa na system ya upepo au system ya ya mafuta ya breki !! System hizo kama zinakaguliwa mara kwa mara breki itafeli vipi ghafla kabla dereva hajaviona viashiria vinavyomfahamisha kwamba hii breki itakuja kufeli wakati wowote ? !! Dereva makini anapokuwa anaendesha gari mlio wowote wa tofauti katika gari lake huwa anaanza kuusikia yeye hata mkiwa watu wanne kwenye gari yeye ndiye atakayeusikia kwanza! Na kama akiwa makini ni lazima ataliweka gari pembeni ili ajue tatizo lipo wapi !! Huo ndio udereva wa madereva wa zamani !!
 
Dereva anayeendesha ndie mwenye dhamana ya kubeba usalama wa abiria wake na yeye mwenyewe.HAKUNA MWINGINE.
Yeye ndo anajua wapi apunguze nwendo,wapi aongeze,wapi afunge breki,wapi aovertake n.k.
Sio serikali.
You nailed it!!
 
Masauni hakuna anachokifanya hapo
images.jpeg
 
Ni sahihi kuhusisha teknolojia, lakini kwa mtazamo wangu teknolojia inatibu chanzo kimoja tu cha Uzembe wa dereva, wakati kuna vyanzo vingine vingi...
Hivyo vyanzo vingine ndivyo traffic wameshhindwa kuvitumia vema, kwa mfano, wiki ya usalama barabarani magari yangekagulliwa badala ya kuuziwa stika, tyre za magari zingekaguliwa na kama hazifai garii iingeweka karantini mpaka iletewe tyre mpya na kuvishwa ikiwa yadi tena chini ya usimamizi wa askari waadilifu, madereva wangepimwa alcohol terminals za miji mikuu nk, lakini ilivyo sasa rushwa ndiyo inasababisha haya yote yatokee
 
Sijui wale waliokuwa wanapiga kelele trafiki wapunguzwe barabarani wanasemaje kuhusu ajali kuongezeka?
Mkuu waliokuwa wanapiga kelele wamepokea mapendekeza ya waharifu wenzao ili wapitishe magendo bila bughudha

Kuna aina tatu za visababishi vya hatari yoyote
1. Underlying cause (indirect cause)-external factor,
2. Immediate cause (speeding without consideration to other road users, speeding downhill, speeding knowingly there is a corner ahead)
3. Root cause (corruptive system cartel, mechanical defect & abuse of road traffic regulations)
 
Back
Top Bottom