Serikali iwe makini, isikurupuke kurudisha mtandao wa intaneti

Lini Serikali ilitangaza imezuia mitandao? Wewe huu ujumbe ungeufikisha hapa bila mtandao kufanya kazi? Kwanini usiengeandika OP-ED Kwenye Majira au Mzalendo kupitia SLP tukasoma huko?
Usinipangie.
 
Kwahiyo baada ya hizo leseni nyingi kufutwa ndo unataka kusema hivi sasa hayo madini hayachimbiwi na Wazungu? Unaweza kutaja ni leseni ya kampuni ipi kubwa ambayo ilifutwa?

VERY STUPID!!!
 
Mkuu umefikiria athari zake kwa watu ambao hufanya biashara zao online? Applications za job na hata vitu vingine muhimu vinavyofanyika online ?
Umeuliza maswali mazuri sana. Serikali ina evisa ya watalii na pia epassport application vyote vinahitaji internet. Ni jambo la kusikitisha na kushangaza Karne ya 21 watu wananyimwa internet as means ya kuwa control. Itakuwa ngumu sana kuendesha shughuli za maendeleo bila internet. We are DOOMED !
 
Biashara za kuuza kupitia mtandao bongo? Nyumba hazijapangiliwa na hao ndio huwa wa kwanza huko uswahilini kuuana kwa kusiliza uongo wa kwenye mitandao.

Kusoma kwa kutumia internet ni uvivu wa kusoma vitabu ndio maana ubongo wako unawaza uharo
Wewe ni kichwa maji kabisa ,eti mitandao bongo ? Hivi unajua wangapi wanategemea hiyo mitandao kujipatia kipato ?hao vijana wengi waliomaliza vyuo wakakosa ajira kwa mfumo mbaya wa serikali wamejiajiri kwenye mitandao wanatangaza kufanya biashara mitandaoni ,booking za utalii ,mahotelini ,wanaingiza hela kwa views za video nk wote wameharibiwa kazi ,usifanye mambo kwa kukurupuka dunia inabadilika internet ni muhimu siyo unaongea upumbavu hapa
 

Maendeleo hayazuiliki, tunapolilia maendeleo ni pamoja na miundombinu na teknolojia yenyewe!!

Kama hivi watu walishaanza kufanya biashara za online, unaagiza bidhaa unaletewa hadi mlangoni bila kutoka! Si swala la uvivu bali ndiyo maendeleo yenyewe!!

Ishu si kuzima internet tu, serikali inapaswa kuwa na mikakati ya kuwa na wataalam wa ulinzi katika hizo teknolojia ya mtandao ili kupambana na hao wanaoonekana kuwa vitisho. Ukiwa na ulinzi wa kutosha huna cha kuhofia!!

Nadhani kuna ulazima wa kusomesha vijana wa kizalendo katika maswala ya ulinzi katika internet au cyber security ili kuwa na timu itayoweza kisaidia na wazalendo kama kina Dr. Jabir wa e'goverment ambao wamekuwa wanafanya vizuri sana.

Next time, badala ya kuzima basi tunapambana. Wametia hasara watu, walio apply kazi wameshindwa kupata majibu, tuliokuwa tunaomba scholarships tulishindwa kumalizia, kuna ndugu zetu wa online stock za bidhaa zinaozea ndani!!
 
Mleta mada ana stress,sasa anahamishia stress zake jukwaani!
 
Biashara za kuuza kupitia mtandao bongo? Nyumba hazijapangiliwa na hao ndio huwa wa kwanza huko uswahilini kuuana kwa kusiliza uongo wa kwenye mitandao.

Kusoma kwa kutumia internet ni uvivu wa kusoma vitabu ndio maana ubongo wako unawaza uharo
Itokeshe kusema wewe ni mjinga, ni mjinga wa kuzaliwa kabisa

biashara inayofanyika kwenye mitandao huenda ni kubwa hata mara nne zaid ya hii physical business

hakuna duka leo utaingia hapo town ukute hawana instagram page, hakuna muuzaji anaetegemea mteja tu atoke zake nyumbani anyooshe mpaka dukani kwa muuzaji hapo sinza sijui tabata sijui k/koo , mtu anakuja baada ya kuona bidhaa mtandaon

iwe nguo, iwe mavazi, iwe vyombo vya nyumbani, sijui mafundi ujenzi, sijuo maduka vifaa ujenzi,sijui mapambo, sijui , wauza viwanja, magari, mashamba, elimu ya aina yeyote ile , mabucha, furnitures etc etc, sijui wauza tv, fridge, yaan chochote kile

kwa kifupi, kitu chochote kinachoruhusiwa kutangazwa bila kuvunja sheria ya nchi kinatangazwa na kuuzwa mtandaon huko

nina miaka 2 net sasa hivi mapato yangu yote yanatoka instagram na Facebook yote 100%

dunia ilishabadilika fala ww, hizo biashara za miaka ya 90 hapa mjini hazifanyi kazi leo
 
Kukiwa hamna Internet uchumi ndiyo unakua? Tuache ujinga na upumbavu......ajira hakuna na watu wamejiajiri kwasababu ya Internet kwa online business........ni mtu mjinga pekee ndiye anaweza kuwa na mawazo ya gizani kama haya......
 
Ni lazima kuelewa mihimili (principles) za logic, na morality. Nje ya hizo principles kunakuwepo na malumbano yasiyo na tija.

Mhimili mmoja wa moral principles ni "THE END DOES NOT JUSTIFY THE MEANS"

Kuhifadhi amani ni good END lakini hairuhusiwi kutumia evil MEANS ili kufika huko.

Kufungia Watanzania mawasiliano kwa njia ya mtandao is EVIL. You can't justify doing it as a means of maintaining peace.

Kuainisha kwa mfano mkali zaidi, niseme hivi: ukitumia mbinu ya kupiga risasi Watanzania wowote watakaoonekana barabarani, basi Watanzania wote watajificha majumbani kwao na "nchi itakuwa na utulivu" Wewe mleta mada hii unakubaliana na njia hiyo ya kuleta utulivu?

Kama wengi walivyowahi kusema amani siyo tu kutokuweko na mapigano (peace is not just the absence of war). Kwa sasa hakuna amani Tanzania.

Kufungia wananchi mawasiliano ya mitandao ni kitendo cha kidikteta na kihuni na chenye madhara makubwa sana.
 
internet itabomoa flyovers isiwashwe....nawaza kama CCM
Tena Askofu Rashid alisema corona imesababishwa na 5G, kwahiyo ni muhimu kuzima intanet manake corona inaweza kuhamia kweney 4G na taifa likawa destroyed!!
 
Haya mabingwa wa kuiga vitu vibaya. Vitu vizuri hata hamna muda wa kuiga. Mfano demokrasia na KUACHA kura ndo ziamue kiongozi
 
Si mmesema watanzania sio wajinga hawawezi kufanya fujo wala kuandamana?Woga huu wa nini sasa?
Watanzania wanachukua tahadhari ya kutotokea hivyo nilivyovitaja!!! Usipindishe hoja yangu.
 
Kuzima internet ni expensive sana ukitaka kurudisha maana kuna mikataba ya kibiashara unakuwa umeivuruga. Ila kama ni lazima kwa usalama was nchi inabidi.
 
Watanzania wanachukua tahadhari ya kutotokea hivyo nilivyovitaja!!! Usipindishe hoja yangu.
Watanzania au Jiwe lisilopenda mitandao na lilikuwa linataka malaika waje wafungie mitandao?
Anatumia loop hole ya uchaguzi kufungia mitandao,shame!
 
upumbavu wa kiwango cha lami. nafikiri nguvu wanayotumia kupambana kuionyesha dunia mambo ni safi (hukutechnolojia ikiwaumbua) wangeitumia kuondoa kwanza upumbavu/ujinga wa wafuasi wao.
Tena hiyo ingesaidia sana Lumumba kuwa na Genge la Wafuasi ambao watakuwa wanamsaidia Jiwe kwa maana ya kumsaidia hasa!!!
 

Kwani wewe hata serikali ikiamua kuwa uwe unachapwa viboko 2 kila unapoamka asubuhi si utakuja na uzi kama huu huu wa kuunga mkono?

Tangu lini mkaishiwa mapambio ya kusifu ma-taga na ma-lb7 nyie?
 
Watanzania au Jiwe lisilopenda mitandao na lilikuwa linataka malaika waje wafungie mitandao?
Anatumia loop hole ya uchaguzi kufungia mitandao,shame!
Pole sana. Maana kijiba bado hakijatoka rohoni. Kitatoka, Polepole ndiyo mwendo!
 
Mkuu, nimeandika nikafuta mara kadhaa, lakini itoshe kusema haujui unachokipigania. Swali dogo tu, ikiwa unaipongeza serikali kukata mawasiliano hayo, mbona upo hapa ? Mbona umefanya kila juhudi uwe kwenye mtandao ?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…