Serikali kama imeshindwa kutengeneza ajira kwa vijana, ijiandae kujenga magereza mengi

Amen
 
Inawezekana changamoto kubwa ya umasikini inaanzia kwa wazazi. Wanamuandaaje kina na wao
Ndiyo, wazazi wengi wanafanya kazi kwaajili ya pesa hawana ujuzi wa kufanya pesa iwafanyie wao kazi yaani jinsi ya kutumia pesa kuzalisha pesa laiti wangekuwa na ujuzi huu umasikini ungepungua.
 
Life doesn't follow the blueprint of a syllabus.

If one does not know to which port one is sailing, no wind is favorable.

Maisha yamebadilisha kitasa, Elimu sio ufunguo tena.
Mbaya zaidi kuna kundi linaamini bila kufanya kazi haramu hutoboi, wengine wanaamini bila ushirikina hutoboi. Hali ni mbaya sana mitaani
 
Aisee! Umeandika kweli ila kwa machungu mno. Pole broo.
Ninawaangalia vijana wengi hata siwaelewi.
Hivi kweli vijana wanaijua hali yao ilivyo na mustakabali wa maisha yao ya sasa na baadaye? Mbona wamekaza fuvu e.g. wanaambiwa Ajira hakuna mjiajiri wenyewe, lakini bado wanalilia ajira.
1. Vijana wanadanganyana eti mjini ndo mambo yote. Sasa hapo mjini mmefungiwa hapo hamwezi kutoka? Nendeni huko vijijini makajaribu kujitafuta huko.
2. Vijana mliosoma na kufuzu vizuri na cheti mkapata. It is OK. Lakini wakati unasubiri labda fursa itapatikana, jaribuni fursa nyingine. Zipo fursa za kukopa. Sio lazima ukakope pesa-Hapana. Kopa vitu Physical e.g. unaweza kujaribu "Kauli mali" au kukopa shamba kwa muda n.k. Shida ya vijana hapa ni uvivu, uoga na ule uthubutu wa kujaribu. Huku vijijini fursa ni nyingi lakini vijana waliosoma wanajisemea "Why should I go to venture in those dubious activities with my degree? A graduate can't engage in indigenous chicken production......... or tilling the land......... they are selective." Kwa hiyo kaeni na Kiingereza chenu halafu kitaeleweka.
 
soma comment #26 badili mtazamo wako.

Acha kulialia dunia hii hakuna wa kukuonea huruma.

Acha kuwasikiliza wanasiasa maisha ni vile unayaendea🤝
 
Mikopo haitakufikisha mahali sanasana itakufilisi,tafuta ujuzi hakuna mtu mwenye ujuzi analia njaa.

Soma post #26 hujachelewa chukua hatua.

#kupanga ni kuchagua.
 
mi niliingia migodini huko kuchimba, nilisahau mengine kwanza, ikawa ni kukomaa kusaka mtaji,....... maisha hakika ni safari ndefu🙏🙏
 
Kwanza hakuna serikali inayo weza kuajili wananchi wake wote lakini lingine watanzania tujitahidi kuwa waaminifu tukiajiriwa ,nimesikiliza clip moja ya muwekeza aliye ajiri vijana kwenye mashamba yake matokeo yake vijana wanatumia matrekta yake kufanya kazi za nje kwa wizi hadi yameharika, sasa nani atawaajiri nyie kwa tabia za wizi hizi?
 
soma comment #26 badili mtazamo wako.

Acha kulialia dunia hii hakuna wa kukuonea huruma.

Acha kuwasikiliza wanasiasa maisha ni vile unayaendea🤝
Sawa vijana wanatakiwa kuongeza ujuzi ila ukikosa ujuzi kuhusu fedha na jinsi gani utaitumia kuongeza pesa hata kama umesoma veta na macourse mengine bado utaona maisha magumu.
 
Sawa vijana wanatakiwa kuongeza ujuzi ila ukikosa ujuzi kuhusu fedha na jinsi gani utaitumia kuongeza pesa hata kama umesoma veta na macourse mengine bado utaona maisha magumu.
Endelea kujiliza hapo subiri wanasisa waje kukufariji, yaani kijana mzima unataka ufundishwe budgeting na how to maximize profit hivi huko shule mlienda kukariri ujinga😀😀😀

Sasa kama application ya hesabu zile za form 4 au lasaba hauwezi maana mimi nakumbuka form 4 enzi zetu tulifundishwa hesabu ambazo ndo nazitumia mpaka leo maishani. Pia darasa la saba mwalimu wangu wa hesabu alikuwa anasistiza ni bora mtu ujue hesabu utakuwa hata Kondakta akimaanisha ukiijua hesabu wewe pesa haitakusumbua.

Vijana wa leo bure kabisa!! mmebemendwa nadhani, yaani mmelelewa kimayaimayai hambebeki😬😬😬

#Kijana endelea kusubiri embe chini ya mnazi!!!!
 
Watu wasiolia njaa ni wale wenye ujuzi wa kufanya pesa izalishe pesa nyingine vingine ni vya ziada.
Wewe ni muumini wa miujiza,hauna imani kuwa mafanikio ni mchakato.

Nakushauri ungana na matahira wale wa KAWE ukapakwe mafuta ya bukubuku huwenda ndoto zako zikatimia.

#kupanga ni kuchagua!!!
 
ENglish muhimu mkuu. Huoni watu wanavyoangaika kwenye interview au kupata connection ya kufanya kazi na wazungu. Ata kupata fursa nje ya nchi kuzamia marekani, Uarabuni bila kiingereza maisha ni magumu. Bila hiyo lugha ujasiri wa kutoka nje ya mpka kutafta fursa unaupata wap. Tuulize sisi tuliozamia Sauzi enzi za kikwete ujue umuhimu wa hiyo lugha
 
Mkuu ujuzi wa kufanya pesa ikufanyie kazi haina uhusiano wowote na hisabati. Na ni wachache sana wana ujuzi huu kwakuwa haufundishwi mashuleni na pia ujuzi huu unamfanya mtu aingize pesa bila kujichosha.

Make money work for you.
Soma kitabu cha the RICHEST MAN IN BABYLON utanielewa.
 
Washa ibadilisha Betting kama Proffession utawaambia nn
 
Hao mnaita wawekezaji ni makanjanja,mtu anaanzisha mradi anaajiri watu wa hovyohovyo ili awalipe kidogo.Hakuna upuuzi kama huo ajiri watu serious wenye ujuzi husika pia walipe vizuri weka management uone kama ptoject yako haitaenda vizuri.

Ila unaokoteza huko warugaruga unawafanya mashamba boy wako lazima kikurambe tu😄😄😄.

Mafanikio ni mchakato,hakuna shortcut kwenye maisha. Bisha kikurambe!!!

#kupanga ni kuchagua!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…